Ndoa hizi, kweli yataka uvumilivu wapendwa

bmk

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
571
857
Za Asubuhi?!

Jamani mimi ni mwanaume mume wa mrembo niliyekubali kuishi naye mpaka kifo changu.
Nina miaka kama minne ya ndoa. Mke wangu amekuwa akisisitiza sana kuwa tuinvest kwenye ardhi, lakini katika mipango yangu mara zote huwa nawaza kuinvest kwenye biashara.

Sasa kwa sababu ni mke wangu, ili kuheshimu mawazo yake..Miezi sita hii nilijidunduliza weeee nikapata ka hela kwa kusave kiasi fulani hivyo nikaanza mchakato wa kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kujenga. Nimepata mbezi kimara. Nikafanya mchakato wee mpaka nikakamilisha kulinunua, tena nikaandika la Mr and Mrs.. Sasa malengo yangu nimsuprise..

Juzi nikiwa katika maandalizi, kwanza nikamtengenezea mazingira mazuuri toka asubuhi ili jioni hata nikimsuprise awe katika hali ya furaha, binafsi nilitegema atashtuka na kufurahi sana...Dah kilichonitokea ni kufokeana kwanini ulifanya kimya, kwa hiyo ukaona mimi sifai kuhusishwa kwenye mchakato?! yaani lawama kibao. Lakini nikamwambia mbona nimeandika jina letu sote, lengo langu ilikuwa ni kukusuprise..

Pamoja na kumwambia maneno hayo bado lawama zilizidi mpaka kunichukia hatuongei mpaka leo. Kila nikimsalimia anajibu kama hataki mbaya zaidi mzigo ndo sijapewa nina siku ya tano sasa.

Sasa nawaza kosa langu hasa ni nini? Kwa sababu hiyo hela ningeweza kwenda kula starehe ama kuhonga, ama kununua ka Rav4 kangu new model yard au kufanyia jambo lolote lile. Sasa nimepeleka kwenye ardhi na hajatoa hata shillingi lakini nimeandika majina yetu wawili bado napewa lawama kweli?!!

Naona ndoa hii sijui imeanza kuleta uchungu.Nimewaza wee nikasema ndo maana wanaume wanakuwaga na michepuko nje khaaaaa?!!!!


Naombeni ushauri wanaume wenzangu, pamoja na wadada wote kwa pamoja. Niko na masikitiko sana hapa.

Ahsanteni!
==========
Michango

Bado hujamtambua mkeo vizuri,kina wanawake wengine hawatambui maana ya suprise,ila ungefanya kumuhusisha labda hakutaka hata uandike jina lake ila alikua anataka ajisikie ile feelings ya kuhusishwa kama mke kwa kila hatua (hi wanawake huwa wanaipenda sana),hata biashara hata kama ushaianzisha muda kwa juhudi zako we mwambie nataka kufanya biashara flani atoe mawazo ake alafu mwisho umwambie ile biashara imefanikiwa nawe umetoa mchango mkubwa mno(msifie ajiihisi wamuhimu), atakupenda hata kama ni mke wa mtu unambeba vizuri

Cha msingi we jishushe mwambie umekosea sana (jiconderm mpka aone aibu jilaumu sana kwake),mwambie kile unahisi anataka kusikia then mtoe uko kiaina kuhusu madhara ya kuuza kile kiwanja na kununua upya ni pesa ngapi itapotea

Cha zaidi ni uvumilivu,msome zaidi ,muhusishe kwa kila jambo kama unaona ni kubwa muhusishe kiana,

bmk,

Kama ulipita shuleni kwa kiasi hata kidogo Karl Marx ana theory of conflict inasema hivi "...society is in a state of perpetual conflict because of competition for limited resources. It holds that social order is maintained by domination and power, rather than consensus and conformity".

Kubaliana na mimi kwamba hakuna mahali watu wanaishi bila conflict, conlicts make people think even beyond looking for solutions and that is what result into development (But not necessalily). Masuala ya ndoa yanahitaji mwanaume mwenye akili. Tafakari tu, just think that, not every misunderstanding may be a conflict, sometimes can be defined as outlook differences

Mkeo mmetofautiana tu mitazamo, wakati wewe ulitaka kum-supprise probably yeye ameliona hilo kama attempt ya kutaka ku-subortage, au ameona kama huthamini mawazo yake katika kufanya mipango pamoja. Think roudly my friend. Hawa binadam ni wa kuhandle with care, they are so fragile.

Mi nafanyia kazi mkoa fulani lakini familia ipo mkoa mwingine. Huwa inatokea tusipowasiliana usiku, kesho yake unaulizwa, jana ulilala wapi mpaka ukashindwa kunipigia simu? Au unapiga simu mapema zaidi unaulizwa mbona umepiga mapema hivi unahofu nini kunipigia usiku zaidi? Just think of these complications.

Tuliambiwa kwenye maandiko, mwanaume ukae kwa akili na mwanamke maana ni mdhaifu. This means, what happens to women thinking, comes from their weakness, it can be their way to defines situation and events. Siku ukijua hilo hutahangaika nao

Fanya hivi, mchukue mkeo leo au kesho, mpeleke kariakoo, just hold Tshs 30,000 in your pocket, mkifika huko mwambie huwa unatamani avae vazi fulani (mwambie hili hapa)_then achague langi anayotaka maana wao wako interested na rangi. Mkitoka hapo pateni kinywaji sehemu, then mtake radhi kwa kilichomuudhi, hakika nakwambia, jioni hutomwomba ibada ya ushirika, ataiandaa na kukupa yote na tofauti zitaishia hapo

See the nature of your wife first then decide the style you can make living with her. Usilazimishe unalotaka wewe. Japo yapo mambo kwa mwanaume huhitaji kumshirikisha, unayapeleka kwa njia ya "power of man" na akileta za kuleta unamkolomea na kumpiga stop aache uzezeta because that is you power of authority in the house. Hapa ndipo theory ya Karl Marx inatumika kwa kipengele hiki "....It holds that social order is maintained by domination and power, rather than consensus and conformity".

Mwanamke lazima akujua in black and white ili kwa baadhi ya mambo hata hapaswi kukuhoji maana kwanza ni mazuri hata kama akiyahoji haina maana kwa maana yeye hawezi kuyafanya kwa nature mnayoishi kwenye familia yenu.

Otherwise, context ya ndoa huamua style ya maisha na maamzi
 
Ni dhahiri huyo katika kukushauri kwake kuwa muwekeze katika ardhi tayari alikuwa na plan zake. Aidha ana mtu ambae alishapanga nae upigwe hela (kuuziwa kwa fedha ya juu zaidi) ama tayari alikuwa na sehemu kwahiyo ungenunulishwa mali yake, kwahiyo angepata faida.

Kwa kifupi hili lililotokea linapaswa kuwa ni fundisho kuwa unaishi na mtu wa aina gani, jiongeze kama una nia ya kujenga basi jenga kivyako tofauti na hapo utakuja kulia kinywa wazi.
 
Kuna kitu umekosea hapo ambacho ni ushirikiano ambao ni mojawapo ya misingi mikuu wa (mingine ni upendo, uvumilivu, ucha Mungu, mawasiliano na uaminifu).

Ushirikiano ni jambo muhimu sana haswa kwenye maswala yanayohusu Maisha yenu ambayo ni ya kudumu. Unaweza ukafanya surprise kwenye vitu vidogo vidogo ambavyo havina life span ya muda mrefu na wala haviwezi kuathiri Maisha yenu. Kwenye Ardhi huwezi kufanya surprise kwa mkeo simply sababu kama ni sehemu mnataka mjenge na kuishi, kwa nini hukushirikiana nae kutafuta eneo ambalo mtakubaliana wote wawili?

Vipi kama yeye alitaka kukaa Mbezi Beach au Mkuranga wewe ukaenda kununua Mbezi ya Kimara? Kwenye hilo suala umefeli sana na hiyo adhabu ya kunyimwa unyumba ni ndogo sana ilibidi akumwagie maji ya moto nyetini ukiwa umelala
 
Bado hujamtambua mkeo vizuri,kina wanawake wengine hawatambui maana ya suprise,ila ungefanya kumuhusisha labda hakutaka hata uandike jina lake ila alikua anataka ajisikie ile feelings ya kuhusishwa kama mke kwa kila hatua (hi wanawake huwa wanaipenda sana),hata biashara hata kama ushaianzisha muda kwa juhudi zako we mwambie nataka kufanya biashara flani atoe mawazo ake alafu mwisho umwambie ile biashara imefanikiwa nawe umetoa mchango mkubwa mno(msifie ajiihisi wamuhimu), atakupenda hata kama ni mke wa mtu unambeba vizuri

Cha msingi we jishushe mwambie umekosea sana (jiconderm mpka aone aibu jilaumu sana kwake),mwambie kile unahisi anataka kusikia then mtoe uko kiaina kuhusu madhara ya kuuza kile kiwanja na kununua upya ni pesa ngapi itapotea

Cha zaidi ni uvumilivu,msome zaidi ,muhusishe kwa kila jambo kama unaona ni kubwa muhusishe kiana,
 
Hao ndivyo walivyo tumeambiwa kwenye maandiko tuishi nao kwa akili,huwa hawana wema,unaweza kujikuta umefanya jambo kwa wema lakini mwisho wa siku unaambulia kashfa na matusi,jamaa yangu ilimtokea hii,kaenda kwenye graduation ya mtoto wao siku hiyo hakwenda kazini wakakubaliana mke yeye aende kazini ,mke kurudi nyumbani jioni anamwambia mumewe anatembea na h.girl wake kisa jamaa aliporudi nyumbani kajifungia ndani na bahati nzuri huyo h.girl mwenyewe alikuwa kaenda kanisani kwenye ibada,mzozo juu ya mzozo hakuna maelewano mpaka ikafikia jamaa akaanza kujutia hata kwanini alienda kwenye hiyo graduation badala ya kwenda kazini,kwahiyo mkuu ukisikia watu wanaachana au magomvi ndani ya ndoa au wanaume wengine anaamua kuhamia baa ni mavitu ya aina hiyo...
 
Mkuu, hapo wewe jenga bila yeye kujua...akikuuliza kuhusu icho kiwanja mwambie umekiuza umerudisha hela ulipo kuwa umekopa...kisha endeleeni na taratibu za kutafuta sehemu nyingine mkishirikiana pamoja

Ukimaliza kujenga kamsapraizi tena anune vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom