Ndoa ni pale wawili wanapopendana na kuamua kuishi wote kama mume na mke na kupata baraka za wazee/wazazi/walezi wa pande zote mbili kwa makubaliano yao...wengine ni mahari na wengine ni maneno tu na kutoa baraka zao inategemea na mila na desturi zilizopo..na ndo maana mwanamke ukimtolea mahari au kutambulishana pande zote mbele na kukubaliana then ukamuacha yule ndo mke wako na ukioa mwingine hata kwa kanisa bado unazini sababu kibiblia ukichukua mfano mmoja tu wa ibrahim kumposea isaka mke hakukuwa na sehemu walioenda church kufunga ndoa but ilikuwa ni baraka tu kwa wazee na kutimiza masharti/makubaliano waliojiwekea..
Lakini kwenda kanisani /msikitini au mahali popote penye lengo la ibada inaleta radha zaidi sababu kama mkristo uliolelewa na kanisa au muislam uliolelewa na imani ya dini yako...kubariki ndoa mbele ya uwepo wa Mungu ni jambo lenye baraka kubwa sana but ndoa kama ndoa ulishaifunga tangu siku ile mlipokubaliana na kupata baraka za wazee.