Ndoa chungu, ndugu wamezidi, nishauri nifanyeje?

hii kali ya kufunga mwaka .tafuta chuo mbali mwambie unataka ukasome kama mwaka hivi umuachie waumini wake hapo
watu 15 nani anasonga ugali?
Huko chuo atakwenda na mwanae..?? Kwa kumwacha mwanae home au kwa bibi kutamfanya huko chuo asifanye vizuri...

HUYU ANATAKIWA AFANYE HAYA..
1. Atafute watu wazima awaeleze hali halisi
2. Hao watu wazima waende kwa wazazi wa mume na kuwaeleza namna ambavyo ndugu watasidiwa wakiwa makwao
3. Hao watu wazima waseme na mumewe juu ya kuwasaidia ndugu wakiwa kwao
4. Bila shaka wazazi na mume wanaweza wakagoma wazo hilo. Sasa hapo hata akiondoka kwenda kupanga roho inweza isimsute.
 
Nashindwa hata kushauri leo, nahisi kama nakufahamu labda

Hofu ya Mungu imekujaa ndio maana unashindwa chukua maamuzi

Mungu akupe hekima tu jinsi ya kudeal na hao watu.
 
Mhhhh mkazie dada hata kama ni ugomvi...mtu wa miaka 24 na watoto juu,not fair..otherwise kama hataki u need a long term plan,mfano
Weka dada wa kazi wawili mmoja wa kwako,mumeo na mtt wenu,mwingine wa wageni woote,..nyumba inategemea Ina ukubwa gani but km servant quarters zipo wengine waishie huko,japo muwe mnasalimiana vizuri, ndugu ukiwaendekeza utachukia maisha yako
I know two families, wamama waliamua kuishi kwa style hio,asubuhi chai na wali,mchana ugali na nyama au maharage jioni wali maharage January to December
We nyumba Ina watu 20 kwa mfano au 15 mchezo, mtapika nini mfurahie,..but main house huku kuna dada anawapikia main family ndo wanabadili chakula na watoto wanaenjoy kuishi kwao,
 
Na kuishi na ndugu napo uangalie,nani anagharamia??punguza kujitoa mana ndugu wakusaidiwa wengi wao hawanaga hata shukrani... Weka wazi atakaehitaji chochote amface baba mwenye nyumba ampe..gharama za vyakula nk agharamie baba mwenye nyumba, maybe then ataona uzito wake...we mtu chakula kipo ndani hajatoa hata sumni na wala hapiki yeye ana shida gani
Kingine ndugu hao wasiishi tu kama wapo hotelini,mama mwenye nyumba pangia kazi kila mtu ikupe wepesi kuwamanage,mfano awepo wa kufanya usafi, ndani,nje,wa kwenda sokoni,wa kupika,wakutuma sehemu nk,
Mkigawana kazi maisha ya home mepesi..
 
Na kama hivo unajishughulisha na kilimo wabebee kwenda shambani wakusaidie..watu wasilale lale ovyo nyumbani, Uwe mkali kabisaaa na uonyeshe kwa mfano mana we mwenyewe hulali unajishughulisha
 
Z
Nikiwapeleka shamba hawamalizi wiki wanatoa kila aina ya visingizio mpaka watarudi tu home, kwa kifupi hawataki kazi za shamba wao kwa akili yao wanaona mradi wa shamba ni wangu mimi, hivyo wanaona kama vile watanifaidisha mimi ilihali hicho ndicho chakula wanachokula
Ukiuza weka akiba benki,fungua kabisa akaunti ya malengo ambayo hutoi hela,peleka kiasi kidogo tu home the rest agharamie mwenye ndugu
 
Wandugu Salaam,

Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa, yaani ndio star kwao.

Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza.

Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe.

Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisa.

Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na ninaomba ushauri wenu ndugu wana MMU; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home.

Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.

Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.

Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!

Msaada jamani!

Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress.
Duh, hii dunia ina mitihani yake. Pole sana dada angu. Mi mwanaume lakini najua shida unayokutana nayo. Ukikomaa kumwambia mumeo asiwasaidie ataona wewe ni problem. Tatizo mumeo anafikiri ipo siku atamaliza shida za ndugu zake, wote which is impossible. Halafu shida kubwa ni kwamba kwa mtindo huo wa maisha mtakuwa hata akiba hamuweki. sasa, siku mkija kupigika sana kimaisha, hao hao anaowasidia wataanza kuhoji hela zote amepeleka wapi. Mimi pia nilikuwa na mtazamo kama huo wa mumeo ulinitokea puani. Cha msingi acha alete ndugu kadri anavyotaka. ila sasa wewe kazi yako iwe kubuni miradi wakuzalishie pesa. Anzisha vimiradi kibao kibao vya mitaji midogo midogo wakusaidie. Wasiofanya miradi yako hakikisha wanakusaidia kazi zooooooote hapo home. Kufua, kupika, kudeki, etc. Usijali jinsia zao we wapangie kazi tu na mumeo aelewe kuwa hawatakiwi kuja hapo kukunja nne na kusubiri menyu. Tatizo la watu wa kusini akienda kukaa kwa ndugu hataki afanye kazi hata moja, anataka akunje tu nne halafu ale chakula, kazi kwao ni mwiko. Ndio maana wengi ni maskini sana. Pole lakini. TAFUTA CHA KUWAFANYISHA, WENGINE WATAONDOKA WENYEWE, NA WAPYA HAWATAKUJA. Ishu ni kwamba wazalishe, hizo pesa hata wao zitawasaidia.
 
Ahsante kwa ushauri, Mungu akubariki sana
 
Mhhhh mkazie dada hata kama ni ugomvi...mtu wa miaka 24 na watoto juu,not fair..otherwise kama hataki u need a long term plan,mfano
Weka dada wa kazi wawili mmoja wa kwako,mumeo na mtt wenu,mwingine wa wageni woote,..nyumba inategemea Ina ukubwa gani but km servant quarters zipo wengine waishie huko,japo muwe mnasalimiana vizuri, ndugu ukiwaendekeza utachukia maisha yako
I know two families, wamama waliamua kuishi kwa style hio,asubuhi chai na wali,mchana ugali na nyama au maharage jioni wali maharage January to December
We nyumba Ina watu 20 kwa mfano au 15 mchezo, mtapika nini mfurahie,..but main house huku kuna dada anawapikia main family ndo wanabadili chakula na watoto wanaenjoy kuishi kwao,
Ahsante dear kwa ushauri
 
mmeo ana pepo, tena lile pepo kuu anawasiliana nalo daily......huyo binti wa bar unamfahamu vyema.....mke mwenzio huyo bila shaka....eti wanadai ndoa tamu duh....ushauri,,, beba mwanao nenda kwenu.....kuwa na msimamo kamilifu....aamue kuishi na nduguze au wewe....pole sana.
 
Dah pole dada maana kuishi na watoto wasio wako kuna mengi...mueleweshe kwa upole maana hao watu ni wengi kama vipi awasaidie wakiwa kwao maana hapo kazi zitazidi na kuishi na mtu mzima mwenzio kazi maana ataona vya baba yangu.Mungu akusaidie upite salama
Mnajichelewesha wakikuwa hawana msaada nanyi
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Hapo sasa
 
Jaribu kumtafuta rafiki wa mumeo mwenye ushawishi mweleze ili akamshauri namna bora ya kuhandle ndugu, asikutaje lakini, iwe kama yeye nae kanoti mnavyolemewa
 
Hili jambo la ukoo mzima kumtegemea mtu mmoja ni jipu linaloitafuna Afrika, japo wapo watu wachache walojitambua tayari.
Lakini tatizo kubwa naliona kwa wanandoa wenyewe hasa mwanaume ambaye ndiye kiongozi wa nyumba.

Moja ya jambo ambalo wanandoa wanatakiwa walifanye ni kuweka wazi misimamo yao katika ndoa, na misimamo hii yawapasa ndugu na jamaa waijue na wajue kwamba mnaisimamia ipasavyo hasa mwanaume.

Mfano kwangu, inajulikana wazi kama umekuja ni mgeni wa muda utapumzika na kufurahi kisha utaondoka, lakini kama umekuja kukaa utakula kile ulichofanyia kazi na hii ni kwa pande zote upande wangu na upande wa mke wangu. Haiwezekani naamuka usiku naenda kutafuta kumbe kuna viumbe wamekuja wanasubiri kula kazi hawataki kufanya.

Kusaidiana ndugu na jamaa ni jambo zuri sana na linafaa, lakini lifanyike kwa busara siyo mtu mmoja ahudumie ukoo mzima.
ni kweli wanandoa mkikosa misimamo ktk kuindesha familia yenu..hasa baba akiwaanaendeshwa na nduguze hata maendeleo kuyapata inakuwa ngumu sana,kuna baadhi ya ndugu hawapendi kuona ndoa za nduguzao zinaamani
 
mnamlaumu mumuwe bure, jamaa yuko kwenye msukumo toka kijijini kwao. maana ye ndo anaonekana ana nafuu kimaisha ivyo jukumu la kulea familia (ukoo ni yeye)

akikataa kumpokea mtu ukoo unakaa kikao na kumsema anaona bora awapokee tu. ama jamaa ana tabia ya kujionesha mambo mazuri ili hali choka mbaya.

kwa uzoefu toka familia yangu, hapo mwisho wenu ni umaskini wa hali ya juu
hii yakujionyesha mambo safi wakati huna kitu nayo sio nzuri kwakweli
 
Yaani kama ulikuwepo vile, coz kuna wengine wakubwa nawazidi labda miaka mitatu hv; basi wanataka nao wajipangie utaratibu wao; mwingine anataka anywe chai lita nzima pekeake, mwingine msosi anataka arudie full plate hata mara tatu, nikisema niwapeleke shamba wanapiga simu kwa Mr ati wanaumwa wanataka kurudi, nabaki napiga kazi mwenyewe, basii duuuh, stress za kila rangi!
Aiseeee umenikumbusha mbali pole sana apo naona tatizo lipo kwa jamaa we unamoyo sana sasa jitoe ufahamu mbebeshe mzigo wa kuwalisha hao watu ataanza kulalamika mwenyewe
 
Back
Top Bottom