Ndoa bado ni jambo la manufaa na hekima

Ndoa bado ni jambo la manufaa na hekima

Mchanya

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,062
Reaction score
1,713
Nothing good is easy! Pamoja na changamoto zote mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika ndoa, kati yenu kama na mke na mume, ndoa bado ni jambo la maana sana na hekima kulifanya mwanadamu.

Kuoa au kuolewa ni uamuzi wa busara, wa manufaa, wa maana na wa muhimu unaopaswa kufanywa na kila binadamu mwenye akili timamu na anayefikiri sawasawa. Kuwepo kwa changamoto katika ndoa hakumaanishi kwamba ndoa ni jambo baya au tusiingie katika ndoa, ni lazima tuingie na kukabiliana na kila aina ya changamoto zitakazojitokeza.

Ni kweli kwamba baadhi ya wanandoa wamekumbana na hali ngumu sana katika ndoa, lakini hiyo haina maana na si haki kushawishi wengine kwamba (eti) ndoa ni jambo baya. Kwamba wewe umepata uzoefu mbaya katika ndoa haimaanishi kwamba, basi na wengine watapata uzoefu mbaya kama wako. Ni sawasawa kuendesha gari na kupita katika shimo ambalo limeharibu gari lako, haina maana kwamba wengine wenye magari wasipite njia uliyopita wewe, bali wapite kwa tahadhari, tena wewe ndio uwe wa kwanza kuwaambia 'unaweza kupita ila uwe mwangalifu, usipite namna nilivyopita mimi'.

Poleni nyote mlio katika ndoa zenye matatizo lakini msiwapotoshe wanaotaka kuingia, kwani kuna wengi wengine walio katika ndoa zinazovutia, wanazifurahia na wasingependa watoke katika ndoa hizo au kuachana na wenza wao. Kwa wale wote wanaotaka kuoa au kuolewa, endeleeni kufanya uamuzi huo wa busara na kila mnapohisi kwamba kuna changamoto au ugumu fulani, ni vema kuuliza maswali au kuomba ushauri wa watu sahihi, ili muweze kufurahia ndoa zenu.

Ni vema uingie katika ndoa ukiwa na mtazamo kwamba itadumu milele, na utaipigania ndoa hata pale zitakapojitokea changamoto mbalimbali. Tena siku za mbeleni za ndoa yako, utajivuna kwamba tumetoka mbali, haikuwa rahisi, lakini sasa tunafurahia ndoa yetu.
 
Back
Top Bottom