Namshangaa Makonda anavyohangaika na mateja wachache wanaotumia cocaine na heroine anawaacha hawa walio wengi walioathirika na madawa ya kulevya aina ya dini.
Ukisoma huu Uzi utaona mleta mada ni mwoga wa maisha aliyepitia vichangamoto vidogo vyenye kutatulika halafu anavihusisha na uwepo wa Mungu.
Huu Uzi unatoaje uthibitisho wa uwepo wa Mungu? Aliyemsaidia ni Mungu au ni mtu? Matatizo mengi yanasababishwa na watu, hivyo yote yanatatuliwa na watu.
In anyway, a man without God is called an Atheist, while a God without man is nothing.
Naam, tunasoma na kujifunza kuwa, tangu uasi wa Mwanadamu ulipoanza kutendeka, tangu hapo, Ndani ya Mwanadamu kumekuwa na nia ya kutaka kuwa mungu, yaani kuwa mwenye mamlaka yote juu ya maisha yake, na kuishi kama apendavyo mwenyewe na sio kuwa chini ya mamlaka ya mwingine. Nia ya kutaka kuwa mtawala wa maisha yake na kutenda apendavyo yeye mwenyewe. Nia ya kutaka awe mkuu juu ya mwingine kila inapowezekana. Nia ya kujiinua juu ya Mungu.
Kwa muktadha huo, Wanadamu asili yako si wageni tena wala wa kushangaza. Imebidi muwepo ili kudhihirisha upande wa pili wa yule adui wa Maisha ya Mwanadamu.
Katika kitabu kiitwacho BIBLIA kilichoandikwa kwa muda wa miaka takribani 1600 na waandishi mbalimbali wapatao 40 kuanzia miaka 1500KK mpaka mwisho wa karne ya kwanza, ambacho kinakubalika na watu Duniani zaidi ya Bilioni tatu sasa. Kinatueleza kuwa, kulikuwako na watu wenye Mioyo migumu ya kuamini kuhusu uwepo na Ukuu wa Mungu pengine kuliko hata wewe uliyezaliwa katika karne hii ya 21.
BIBLIA inatueleza kuwa, alikuwako mtu au Kiongozi wa Nchi ya Misri aitwaye Farao, na kwamba, pamoja na makuu aliyoyatenda Mungu lakini bado moyo wake ulikuwa Mgumu kukubali ukweli. Kwa mfano, baadhi ya matendo yaliyotendeka ni pamoja na Maji kubadilika kuwa damu, Nchi ya Misri kujaa vyura, Mvua kubwa ya mawe iliyoathiri mifugo na mimea ambayo haikupata kuwako huko Misri, Nzige kuvamia mashamba na kula mimea yote kitu ambacho haikuwahi kuwako hapo kabla. Wazaliwa wote wa Kwanza kufariki katika Misri, pamoja na mengine mengi lakini kwa uchache tu hayo ni baadhi ya yalliyotukia.
Pamoja na maajabu hayo yote, lakini bado Farao alikuwa na moyo mgumu na hakukubali ukuu wa Mungu. Ooooh, YES, iweje sasa upate urahisi wa kumuamini Mungu kutokana na jambo unalodhani ni dogo sana nililoeleza kwenye andiko langu.? Hakika kutokuamini kwako ni jambo lililo bayana.
Kama hiyo haitoshi, katika BIBLIA, tunaelezwa kuwa walikuwako Wakuu wa Makuhani, Waandishi, Mafarisayo na Masadukayo waliokuwa Viongozi wakubwa na Wasomi katika Uyahudi huko Mashariki ya kati enzi za YESU Duniani katika hali yake ya mwili. Tunaendelea kuelezwa kuwa, pamoja na YESU kutenda mambo makubwa ya ajabu lakini bado WASOMI hao na VIONGOZI hawakumuamini.
Baadhi ya miujiza aliyotendeka ni pamoja na Kufufua wafu, kuponya wenye ukoma, Vipofu kupata kuona, Viziwi kusikia, Mabubu kuongea, Samaki wawili na Mikate mitano kuweza kulisha watu wapatao 5000, Kukemea pepo na kuwatoa, kukemea pepo za Bahari, kulaani Mti na kunyauka. Pamoja na hayo yote, lakini walikuwako ambao hawakuweza kuamini.
Tunaendelea kuelezwa kuwa, YESU alijitabiria kuhusu kifo chake. Na siku ya KIFO chake ilikuwa ni majira ya saa sita mchana lakini Nchi ikatiwa giza kwa muda wa saa 3 mpaka saa 9. Kama hiyo haitoshi, Kulitokea tetemeko kuu na makaburi yalifunguka, Baada ya siku tatu alifufuka, na Askari waliokuwa wakilinda kaburi lake wakastaajabu na kuamini hakika mtu yule hakuwa wa kawaida, lakini, kwakujua hilo wale Mafarisayo, Masadukayo na Wakuu wa Makuhani wakawapa rushwa wale Askari walioshuhudia yote yale ili ionekane kuwa YESU hakufufuka bali Waseme kuwa Wanafunzi wake walimuiba.
Na ikawa hivyo, na tangu wakati huo mpaka sasa katika jamii ya Uhayudi, wapo wanaoamini Uongo huo. Sasa kama yote hayo yamefanyika, iweje nawe uamini sasa.? Hivyo, we si wa kwanza, walikuwako na watakuwako wa aina yako ili kutimiza yote yaliyoandikwa. Tena imeandikwa kuwa..
"Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu, wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, hakuna atendaye mema".
Naam, bila shaka pia utasema Maelezo hayo yote hapo juu si kitu kwa maana nimeyatoa kwenye kitabu usichokiamini. Sasa katika mazingira yetu ya kawaida, Je unaweza kunipa chanzo halisi cha mifano michache hapa chini.
1)Bila shaka wiki chache zilizopita ulisikia huko Mwanza katika upanuzi wa Barabara ya Airport maeneo ya Pasiansi kuwa kuna mti uligoma kukatwa na ukawa unazungumza, kama hujasikia jaribu kufatilia maana iliripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Je unaweza kuelezea chanzo cha hayo yote kuwa ni nini.?
2)Katika ujenzi wa Barabara, kumewahi kusikika kuwa, kuna baadhi ya mawe yalishindikana kuondolewa kwa mfano eneo la Sekenke huko Singida mpaka yalipofanyika matambiko maalumu. Je unaweza kuelezea chanzo cha hayo yote.
3)Je unaweza kuelezea aina ya Sayansi au maarifa yanayotumiwa na Wana Mazingaombwe? Mara wanamfanya mtu kusinzia ghafla bila kujitambua, mara wanabadili maji kuwa soda, mara karatasi zinakuwa pesa.?