Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 972
- 1,150
Japokuwa sina historia ya kuogofya sana katika Imani, lakini hapo awali nami bila shaka nalikuwa kama wewe.
Kwanza kabisa, ilifika nyakati nikadai hakuna Mungu. Nilijitengenezea Facts zangu zaidi ya kumi kuonesha wasiwasi kuhusu uwepo wa Mungu. Nakumbukanilipokuwa tu kidato cha tano. Udadisi wangu huenda ulichochewa zaidi na kusoma kwangu masomo ya Sayansi kama vile Baiolojia na Fizikia,Kupenda kwangu kusoma Bailojia ilipelekea hali ya kuujua zaidi mwili wa Mwanadamu unavyofanya kazi, hali ya Udadisi zaidi ikachochewa tena baada ya kusoma nadharia haswa za lile somo la EVOLUTION.
Nakumbuka, baadhi ya mwaswali niliyojiuliza ni kama haya;
1)Kama Mungu yupo na Shetani yupo, na kama Mungu ni Mkuu kuliko Shetani, iweje sasa Mungu asimuangamize mara moja Shetani kisha Wanadamu tukaishi kwa Amani na Raha Duniani.?
2)Iweje Mungu awepo kila mahali, yaani awepo Ulaya, Marekani, Afrika,Asia na kwingineko.? Ana ukubwa gani Mungu huyu jama?
3)Mungu anasema siku ya mwisho kutakuwa na moto wa milele kwa wenye dhambi, sasa iweje Mtu aungue bila kuteketea jumla.?
4)Kama Mungu anafahamu kila kitu, ina maana hakujua kama Adam na Eva watakula lile Tunda.? Na kama hakutaka tunda lile liliwe na aliwapenda Adam na Eva, iweje aliliweka Bustanini.?
5)Kama Mungu anafahamu tunayohitaji kabla hata ya kumuomba, iweje sasa atutake tumuombe.? Si ingetosha tu kutupa tunayohitaji.? Kwa nini tusumbuke mpaka kufunga na kuomba kwa bidii.?
6)Iweje wasiomcha Mungu waonekane wana Maisha bora na mazuri kuliko hata wanao Mcha Mungu.?
Hayo ilikuwa ni miongoni tu mwa maswali niliyojiuliza, mwishowe nikajifanyia hitimisho mimi mwenyewe kuwa hakuna Mungu. Bali uwepo wa Mungu Duniani umeletwa ili kupunguza maasi na kuleta Amani.
Kumbe Mungu ana njia zake bwana, Mawazo yake si mawazo yetu, njia zake si njia zetu. Baadae nikaanza kufikwa na changampoto za kiafya, zilizotishia kutoendelea vema kwa masomo yangu. Hapa ndipo ilipokuwa mwanzo wangu wa kumjua Mungu na kumtafuta kwa bidii zaidi. Ikapelekea kutafuta uhamisho wa shule ili kukabiliana na changamoto zile. Nilikuwa nasoma mchepuo wa PCB, imagine nikakaa zaidi ya miezi minne bila kugusa darasani wala kusoma chochote. Waliosoma mchepuo huo bila shaka watanielewa ninachomaanisha.
Hakika Mungu ni mwema, kila wakati. Changamoto kadha wa kadha zikapelekea kukutana na rafiki zangu wenye bidii katika Mungu. Kwa historia mimi nilikuwa wa imani ya kule kwa wazazi. Nilienda Kanisani kama tu kutimiza Utamaduni na Desturi za Jamii niliyopo. Bila shaka nimeeleweka. Changamoto zikaongezeka zaidi, suala la kifedha likawa changamoto kubwa kwangu. Nikapata Rafiki walionitia moyo, wakanishirikisha kuhusu Mungu na kunitaka niambatane nao huko wanakoabudu. Kwa kuwa nilikuwa wa Imani ile ya Wazazi, kwakweli nilikubali tu kwa sababu ya changamoto nilizokuwa nazo, ila Moyoni nilikuwa Mnyonge.
Siku moja Mkuu wa Shule niliyohamia akaniita Ofsini kwake na kuniuliza nitalipa lini Madeni nayodaiwa. Ilikuwa ni Ada na michango mingine. Akanipa siku kadhaa kukamilisha madeni hayo. Na nisipofanya hivyo, basi asingeendelea kunivumilia tena.
MUNGU AKAANZA KUJIDHIHIRISHA.
Kwa kuwa ilikuwa ni mpango wa Mungu, basi alinipitisha katika njia zake ambazo hadi leo hii nikikumbuka nauona Ukuu wa Mungu ninayemwamini. Siku nilipoitwa na Mkuu wa Shule, wakati nimerudi Bwenini na kutafakari nitapata wapi pesa nazodaiwa, akaja Mwanafunzi mwenzangu kuniambia kuwa Mkuu wa Shule ananiita. Kumbe nilipotoka, aliingia mama mmoja ambaye ni Coordinator wa Shirika moja la kuwasaidia watoto wanaoishi ktk mazingira magumu. Mama yule nahisi alisimuliwa na Mkuu wangu wa Shule kuhusu matatizo yangu. Mama yule alienda shuleni hapo kuwatembelea vijana anaowasaidia kimasomo.Yule mama akawa amenilipia gharama zote nilizokuwa nikiadaiwa. Hakika ni Ushuhuda na ukuu wa Mungu. Ikumbukwe jambo hilo lilitendeka baada ya kujitahidi kuanza kumuomba Mungu kwa bidii, kutokana na bidii kubwa zilizofanyika kupitia wale washauri wangu, rafiki na wanafunzi wenzangu ambao mpaka leo sitowasahau.
Ili kufupisha story,itoshe kusema kuwa, kaunzia wakati huo kila hatua katika maisha yangu hadi leo hii ni Ushuhuda. Mbali ya changamoto za hapa na pale ambazo ni kawaida katika Maisha ya Mwanadamu, lakini kila hatua nayopitia kufikia leo hii, hakika ni ushuhuda Mkuu. Na kama nikisernma niandike kitabu basi ukubwa wa Kitabu hicho itakuwa sawa na kile kitabu cha Bailojia cha A - Level kinachoitwa Biological Science (B.S).
Sasa basi, kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza, hapo Mwanzo kwakuwa sikuwahi kuwa katika kiwango hiki cha Imani. Kwakweli niliwapuuza na kuwashangaa sana watu waliopo katika kiwango hiki cha Imani.
Nilishangazwa na mambo haya..
1)Iweje Mtu amwabudu Mungu kufikia kiwango hata cha kutoa machozi? Japokuwa kutoa Machozi si ishara ya kuonesha kuwa u Mcha Mungu, ila ni kiwango kimojawapo cha juu katika Imani.
2)Iweje watu waimbe na kucheza Kanisani. Niliamini kuwa huko ni kumdhihaki Mungu na kuwa sawa na watu wanaocheza Miziki ya kidunia.
3)Iweje watu waombe hadi kwa sauti kubwa Mfululizo na kwa muda mrefu? Niliamini huko ndiko kule YESU alisema tusipayuke Payuke ovyo.Kumbe sivyo, kupayuka alikosema sivyo inavyosemwa.
4)Iweje Mtu apate nguvu za Kuomba na kufunga kila mara.? Kwa kweli nyakati zile sikuwa kabisa na Msukumo wa kuthubutu kufunga na kuomba kama sasa.
Sikuwahi kufanya haya.
1)Sikuwahi kabisa kuguswa na Mahubiri yoyote yanayohubiriwa mitaani.Lakini leo hii nikisikia tu Mahubiri mahala, lazima nisimame na kusikiliza ujumbe unaohubiriwa.
2)Sikuwahi kabisa kusoma BIBLIA kila siku. Nilikuwa nimeathiriwa na social media, kuchat na kutumia muda mwingi kujadili mambo yasiyo ya msingi sana katika maisha.
3)Sikuwahi kabisa kuvutiwa na jumbe zinazohusu Mungu.Yaani ilikuwa nikiona tu ujumbe unaohusu Mungu, kisha na-scroll down na kuupita kama sijauona.
4)Sikuwahi kabisa kuvutiwa na maongezi ya Watu wanaojadili habari za Mungu. Mawazo yangu yalijikita katika kusikikliza motivation speeches za namna ya kufanikiwa na kuwa Tajiri hapa Duniani.
Lakini leo hii, hali imekuwa tofauti kabisa, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, ndivyo navyojishangaa namna navyobadilika na kuwa karibu na Mungu. Najiona nikiwa mzito wa kumseng'enya mtu, najiona nuikiwa mzito wa kushiriki Uzinzi, najiona nikiwa mzito wa kudanganya, najiona nikiwa mzito wa kukasirika, najiona nikiwa mwepesi wa kusamehe, najiona nikiwa mwepesi wa kuwa na huruma, najiona nikiwa mwepesi wa kutumika kwa ajili ya Mungu. Nisipofanya maombi najihisi kabisa kuna kitu kimepungua mwilini mwangu. Haraka sana narudisha mawazo kwa Mungu na kufanya maombi mda huo. Hekima na Busara zimeongezeka zaidi. Uwezo wa kufikiri umeongezeka na kuweza kuchanganua mambo kwa ufahamu mkubwa. Kwakweli, nina kiu kubwa ya kutumika kwa ajili ya Mungu.
Hivyo basi..
Hivyo rafiki unayesoma ujumbe huu. Jinsi ulivyo mzito katika masuala ya Mungu, siyo hali yako ya kawaida. Ni hali inayochangiwa na wewe kutofanya juhudi za kumtafuta Mungu. Kumbuka kuwa, usipokuwa karibu na Mungu basi utakuwa karibu kwa Shetani. Neno la Mungu linasema " Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii Wataniona" Hapo kuna maneno " wanitafutao kwa bidii" Ni bidii ndiyo itakayokufanya kuwa karibu na Mungu wala si kingine. Neno haliishii tu kesma "wanitatafutao wataniona", bali kuna nyongeza ya neno kwa bidii. Hivyo basi, inakupasa kuchukua hatua siku ya leo ili uuone uwepo wa Mungu katika Maisha yako.
Yawezekana unajitaabisha sana ili kupata MALI za Dunia hii, na kumsahau Mungu. Au unajitaabisha kwa nguvu kubwa ili kupata Mali lakini unatumia nguvu kidogo kumtafuta Mungu. Neno la Mungu linasema, "Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo, na haki pia". Kumbe basi, hata ukitaka Mali zinazodumu na si hizi zisizodumu, inakupasa kumtafuta Mungu kwa bidii kwanza. Hebu tazama maneno haya ya Yesu "Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa". Kumbe, imetupasa kuutafuta kwanza uso wa Mungu kwa bidii kuliko jambo lingine lolote.
Hivyo basi, siku ya leo imekupasa kuchukua hatua moja ya kumrudia Mungu na kumtafuta kwa bidii zaidi. Mungu akubariki na kukuongoza katika kuufikia Ufalme wake. AMINA.!