Kwani ni mara ya kwanza TEC kutoa waraka kama huu? Mfano, mwaka 1953 Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanganyika walitoa waraka unaoitwa "Africans and the Christian Way of Life" Mwaka 1972 walitoa waraka unaoitwa "Peace and Mutual Understanding". Mwaka 1993 walitoa waraka unaoitwa "Good Conscience, Vision and Our Nation". Na nyaraka zote hizo walikuwa wakikosoa mambo fulani, lakini kila mwaka wameendelea kutoa nyaraka hizi. Hata manabii na mitume walihubiri neno la Mungu enzi hizo, leo hawapo, lakini neno la Mungu bado lipo. Kanisa likikosoa jambo fulani siyo kwamba limesema kila jambo ni baya na hivyo linajitenga na mamlaka ya nchi hapana. Kukosoa ni kwamba what is 'bad can be made good; good can be made better na better can be made best'. Katika watu wengi ni wazi kwamba kuna watu watasifia jambo fulani na wengine watakosoa na kusifia au kukosoa hakuna maana kwamba kuna mtu mwema na mbaya maana msifiaji anaweza kuwa mbaya na mkosoaji kuwa mwema au msifiaji kuwa mwema na mkosoaji kuwa mbaya. It all depends on the intention behind kusifia au kukosoa.