Kwenye hili umma unapaswa kusimamia ukweli, tukichagua kuwaogopa, wanasiasa wataendelea kutuburuza maisha yetu yote. Msimamo ni kuwa hatupigi kura na sababu za msingi tunazo na mifano halisi tunayo. Tutakuwa taifa la ajabu iwapo tutendelewa kutiwa vidole vya macho na bado tuwaogope wahuni eti kisa wana madaraka.
Hapo walipo hii hali ya kususia kupiga kura imewatisha, ni juu yetu kutumia njia hii ya amani kuleta mabadiliko tunayoyataka bila kutegemea mwanasiasa yoyote, kwani wao inaonekana wameshindwa. Hatuna tume huru ya uchaguzi, hatuna katiba mpya na hela zimeshaliwa kwenye mchakato, kisha mwanasiasa mmoja anasema hataki katiba mpya na bado tunaendelea kushiriki chaguz za dhuluma, kama sio wendawazimu huo ni nini?