Ndio Shida ya Kuoa Mzaramo!!

Ndio Shida ya Kuoa Mzaramo!!

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,915
Reaction score
30,027
Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kuongea na Mkewe na kwenda kazini. Kurudi kazini jioni kamkuta mkewe kavaa kanga imeandikwa, Ukisusa wenzio wala.


Ilipofika usiku, mke kachukuwa karata aina ya "K" (mzungu wa 4) na kuiweka kwenye mto anaolalila Jamaa.

Asubuh jamaa anatoka kwenda kazini kakuta mke kavaa kanga imeandikwa.
Ukitoka mwenzio anaingia....


Jamaa akagoma kwenda kazin ili amdhibiti mkewe, mara mke akabadili khanga na kuvaa ingine imeandikwa, Hamniwezi nimemdhibiti ndoyo mana hatoki.

Jamaa kufikiri, akaona aende kuomba ushauri kwa rafiki yake akamwambia twenda nyumbani walipofika nyumbani wakamkuta mke kavaa kanga imeandikwa, Kikulacho Ki-Nguoni mwako.

Na kabla hajatafakari ghafla Mkewe kaingia ndani na kutoka na Khanga ingine imeandikwa shemeji utaendelea kula kaka yako kasusa.

U
ngekuwa wewe ndio jamaa ungefanya nini hapo?

 
Back
Top Bottom