Ndio mapenzi ya kisasa au ananipotezea muda?

Ndio mapenzi ya kisasa au ananipotezea muda?

Habari ya kweli; Jirani yangu mmoja alikuwa na familia nzuri tu, mke na mtoto mmoja, tukakaa nao karibu tu kwa muda halafu mama akawa mja mzito. Jamaa alikuwa na gari muda mrefu tu, wana kazi wote wawili, mke alipokaribia kujifungua akamwomba mke wangu amfichie kahela kake. Akamwomba kuwa hata akija ana shida gani asimpe mpaka siku ya kwenda kujifungua.
Alipomwuliza kwa nini shoga? Akamjibu kuwa hiyo ni hela ya kukodisha gari la mumewe siku atakaposhikwa uchungu. Ikaja siku ghafula akaona ka ndio uchungu, kumbe haukuwa wa kweli, lakini alipelekwa hospitali na ilikuwa usiku, asubuhi akaja omba ile hela shs Elfu hamsini. Aliichukua analia kabisa. Mke wangu alipo muuliza kwa nini akasema ameambiwa alipe kwa kukodisha gari hilo .
Wiki iliofuata ukawa uchungu wa kweli, na ile hela imeshatumika, ikawa kilio, gari haitoki mpaka atoe nauli, mbona ilibidi nitoe gari yangu kumpeleka hospitali mama wa watu. Alipojifungua ikabidi tuwakalishe kikao kwa nguvu na matishio kuwa bwana asipokuja tunamhamisha mtaa.
Ilikuwa aibu ya mwaka mama alivyoeleza jinsi anavyo nyanyaswa na hilo lidubwana. Hata kwenda kazini lazima alipe nauli ya mwezi kabla. Ofisi zipo karibu lakini hata lunch hampi. Matumizi ya home wachangie sawa kwa sawa.
Dada, angalia, huyu wako asijekuwa ni wa dizaini hii. Kaa chonjo, usikimbilie harusi ujekuta ni dubwana badala ya bwana.

dah hadi moyo umeniuma...mbona watu wanamioyo ya kikatili hivi?yani mwanamke kakubebea kiumbe chako miezi Tisa zawadi yake nikumkodishia gari lako(lenu) siku ya kujifungua???Mungu nisamehe lakini i rather stay alone than with an evil man like him.
 
Mja asili haachi asili yake,tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili-zitathmini hizo methali kwa mapana yake u will knw what to do.
 
Mja asili haachi asili yake,tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili-zitathmini hizo methali kwa mapana yake,
 
Mja asili haachi asili yake,tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili-zitathmini hizo methali kwa mapana yake,.
 
Salamu kwa wana jf wote!!

Leo nimekuja na hili,

Nina mpenzi wagu ambaye tumepanga kuoana ndani ya mwaka huu, jamani tunaishi kama kaka na dada, yaan hatufanyi mapenz, mpenz wangu yupo bize sana na kazi na biashara, kwa mtazamo wangu naona kama hanijali kama ninavyomjali mimi, hanisaidii kwa chochote yaani toka tumejuana hata sent tano yake siijui, hana time ya kusema hata aninunulie zawadi even ch..u..p ya elfu moja! Ana gari lakini ila mimi sina cha a. jabu nikienda kwake nikishuka kituoni ananiambia chukua tax afu kwa hela yangu sio kwamba atalipia.









Simuelewi maana kama ni hela analipwa mara mbili yangu na biashara anapata laki 6 kwa siku. Zaidi yupo makini sana na simu yake hakubali hata niishike, hata akiingia kuoga sijui anaificha wapi, mara nyingi anachat tukiwa wote nikimuuliza anasema ni watu wa biashara.

Hebu nisaidieni wandugu wenye wapenzi ndivyo mnavyoishi? Naombeni ushauri wenu nin cha
















Angalizo; yeye sio mchaga.

asanteni,
Mmmmmh, sijui nianzeje au niulize huyu ndio mchuchu wako wa kwanza? Au kupendwa hujui maana yake? Hujawahi kupendwa mwanzo? Ebu anza kujipenda mwenyewe kwanza halafu wengine watafatia, akaaaaah!!!! Kwa lipi kubwa mpaka akakufanya hivyo? Wewe ndio ulie mtongozaa mwanzo au wewe? Au sio rizki Huyo kijana ? Ebu nambie kwani ukimuona mambo zake amekamilika kiume ? Manake kuvaa suruali sio uwanaume ivooo...
 
Wafanyibiashara wanakuwa na stress za kupata hasara mshauri awe anapata muda wa kupumzika pia akirudi hom mpetimpeti basi jiweke kimtego mhagi tabasamu ongea nae kwa upole mbona kibamia kitasimama tu! Acha lawama uzembe ni wako tu!
 
We vunga kwani si kuna wengine waendelea kukugegeda na yeye atafungua mzigo wake baada ya kupata pingu ya maisha
 
Kwani kwake umefuata mapenzi au pesa?
 
Huyo jamaa bado ana roho nyingi kwa maana ya kuwa na wapenzi wengi! Bado ana tamaa ya fisi! Biashara gani hadi anaenda na simu bafuni!! Tafakari chukua hatua!!!
 
Mh, hapa pagumu! ngoja waendelee kupita akina iron lady, kongosho. lara 1, king'asti na maswahiba wao watakusaidia kwa hili.
 
Wafanyibiashara wanakuwa na stress za kupata hasara mshauri awe anapata muda wa kupumzika pia akirudi hom mpetimpeti basi jiweke kimtego mhagi tabasamu ongea nae kwa upole mbona kibamia kitasimama tu! Acha lawama uzembe ni wako tu!

mmmh, lazma wao wajue kubalance biashara na mapenzi, kama nje ya ndoa tu hivi je akishaolewa si ataisoma namba tena wakati huo na watoto ndio itakuwa balaa. anaekupenda hata awe busy vipi lazma atakujali kwa namna moja au nyingine.
 
Huna chako hapo bi dada....jipange upya...ana gari hata kukurudisha kwako anashindwa???wengine wana miguu tu na wanasindikiza wapenzi wao!!

umeona eeeeeeeh!!! huyu hana chake, mwache aendelee tu kujishikiza. yaani mwanaume asipokupenda hatokujali hata kidogo, huyo kaka ana wake ampendae wanaspend tu. lol
 
umeona eeeeeeeh!!! huyu hana chake, mwache aendelee tu kujishikiza. yaani mwanaume asipokupenda hatokujali hata kidogo, huyo kaka ana wake ampendae wanaspend tu. lol
pengne hata neno "nakupenda" hajawahi skia.
 
Tatizo hapo wengine wanawapa hata ambao hawana mpango wowote wa kuwa nao in the future.
Mwishowe ni mimba na kuzitoa maana we unajua ndie na mwenzio still scanning.

no simaanishi kila ajaye mbele yako ufike naye huko bali yule anayeonyesha nia ya kuoa zaidi na muwe mshafika either stage ya kutambulishana etc
 
Tatizo hapo wengine wanawapa hata ambao hawana mpango wowote wa kuwa nao in the future.
Mwishowe ni mimba na kuzitoa maana we unajua ndie na mwenzio still scanning.

no simaanishi kila ajaye mbele yako ufike naye huko bali yule anayeonyesha nia ya kuoa zaidi na muwe mshafika either stage ya kutambulishana etc
 
Back
Top Bottom