Habari ya kweli; Jirani yangu mmoja alikuwa na familia nzuri tu, mke na mtoto mmoja, tukakaa nao karibu tu kwa muda halafu mama akawa mja mzito. Jamaa alikuwa na gari muda mrefu tu, wana kazi wote wawili, mke alipokaribia kujifungua akamwomba mke wangu amfichie kahela kake. Akamwomba kuwa hata akija ana shida gani asimpe mpaka siku ya kwenda kujifungua.
Alipomwuliza kwa nini shoga? Akamjibu kuwa hiyo ni hela ya kukodisha gari la mumewe siku atakaposhikwa uchungu. Ikaja siku ghafula akaona ka ndio uchungu, kumbe haukuwa wa kweli, lakini alipelekwa hospitali na ilikuwa usiku, asubuhi akaja omba ile hela shs Elfu hamsini. Aliichukua analia kabisa. Mke wangu alipo muuliza kwa nini akasema ameambiwa alipe kwa kukodisha gari hilo .
Wiki iliofuata ukawa uchungu wa kweli, na ile hela imeshatumika, ikawa kilio, gari haitoki mpaka atoe nauli, mbona ilibidi nitoe gari yangu kumpeleka hospitali mama wa watu. Alipojifungua ikabidi tuwakalishe kikao kwa nguvu na matishio kuwa bwana asipokuja tunamhamisha mtaa.
Ilikuwa aibu ya mwaka mama alivyoeleza jinsi anavyo nyanyaswa na hilo lidubwana. Hata kwenda kazini lazima alipe nauli ya mwezi kabla. Ofisi zipo karibu lakini hata lunch hampi. Matumizi ya home wachangie sawa kwa sawa.
Dada, angalia, huyu wako asijekuwa ni wa dizaini hii. Kaa chonjo, usikimbilie harusi ujekuta ni dubwana badala ya bwana.