Ndio Maana sishabikii siasa za Bongo ...

Dec 26, 2016
9
3
*MAAJABU YA SIASA ZA BONGO*

Ni Bongo pekee ambapo viongozi wa *Chama Tawala* ambao badala ya kuisimamia Serikali na Viongozi wake ili watimize majukumu yao, wao kazi yao ni kusifu tuu kwa nyimbo na mapambio. Wao kila kitu ni 100%. Wamejitia hofu ikawaingia mpaka wakasahau kuna *Chama kushika hatamu* Kiongozi anayejaribu kukosoa huonekana msaliti na kuambiwa *sio mwenzetu, ametumwa au huyu siku hizi haelewekieleweki*

Ni Bongo hiii hii ambayo *Viongozi wa vyama vya Upinzani* badala ya kutoa Sera mbadala, kazi yao ni kubeza kila kitu tena kwa matusi na lugha za kuudhi. Wana hasira kuliko wananchi. Kwao hakuna chochote chema kilichofanyika ila kile walichosema wao. Akitokea mmoja akasifia utasikia aah humjui huyo *huyo ni mamluki, wakala au amenunuliwa. Come-on*

Ni Bongo pekee ambako watu hawaangalii hoja ili kuiunga mkono au kuipinga , bali huangalia nani kaisema ili kuipinga au kuiunga mkono.

Ndio maana mkiambiwa haya mavyama hayana chochote muwe mnaelewaga ‍♀‍♀‍♀
 
Back
Top Bottom