wadau,kuna mshikaji mmoja alikuwa na mpenzi wake ambao kwao walikuwa masikini sana...mkaka yule alikuwa anampenda kweli mpenzi wake yule, tena kwa dhati...akachukua jukumu la kumsomesha yule mwanamke anzia form one, kwani kwa yule mshikaji kulikuwa na hela, hivyo kwa utu wema alishirikiana na kaka yake mkubwa na kumsomesha mpenzi wake yule mapaka dada ule akafanikiwa kumaliza advncd dploma, yote kwa gharama za mpenzi wake yule..baada ya kumaliza advanced dploma, msichana ulee alifanikiwa kupata kazi na kulipwa vizuri, akainua na uchumi wa nyumbani kwao..mpenzi wa dada yule ambaye wakati msichana wake anasoma na yeye pia alikuwa akisoma alikuwa na imani kwamba ule ndiye mke aliyeletewa kutoka mbinguni, alimpenda, akamheshimu na kumuamini na kuwa mwaminifu...pindi akiwa chuoni, kaka ule akapata taarifa..taarifa ambayo ilimuhuzunisha na kumfanya aone kama amepungukiwa...alipokea taarifa iliyomchoma moyo,alipata msiba mkubwa alipopata taarifa kwa njia ya kadi ya mualiko wa harusi, kwamba mpenzi wake ule anaolewa mwezi unaofuata......alihudhuria harusi na alikuwa akilia mwanzo mwisho....akabadilisha mwenendo wake wa maisha na kuwa mnywaji na mchezea wanawake....hataki kusikia kabisa neno kuhusu mapenzi....kutokana na mwanamke, ndio maana akabadilika...msaidieni ndugu huyu...walau kurudisha imani na mwenendo wake uwe kama awali....