Ndimara Tegambwage: Membe anapolia mbele ya Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndimara Tegambwage: Membe anapolia mbele ya Mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Emils, Jun 26, 2011.

 1. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SITAKI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ahubiri siasa za kuomba huruma. Wiki hii bungeni, alilitaka bunge, Watanzania wote na wenye nia nzuri kwa taifa hili, kusimama na serikali kupinga alichoita “udhalilishaji” wa kampuni ya Uingereza. Kampuni ya Uingereza inaitwa BAE (BAE Systems plc). Inatengeneza vifaa vya elektroniki vya ulinzi kwa majeshi na vyombo vya usafiri – ndege na meli. Ni BAE wanaotengeneza rada za kuongozea ndege – za kiraia na kijeshi na mitambo mingine kwa shughuli hizo. Ni BAE waliouza rada kwa Tanzania kwa “bei ya kuruka” zaidi ya sh 40 bilioni. Ni BAE waliogundulika kutoa rushwa kwa baadhi ya watendaji serikalini ili kuwalainisha; ili wakubali kununua rada haraka na kwa bei ya kuruka. Baada ya kashfa hii kufumuka, kuchunguzwa na hatimaye kujua kilichofanyika na waliohusika, BAE wamepewa sharti la kurejesha fedha zinazozidi kwenye bei halisi ya rada hiyo. Fedha hizo, zaidi ya dola milioni 20 za Marekani (dola 1 = sh 1,500), siyo “chenji” kama wezi wanavyotaka tuamini. Ni fedha zilizoibwa kwa kutumia madalali na mawakala ndani ya nchi; ndani ya serikali. Sasa pamoja na BAE kukiri ilichofanya, inasema haitaki kurejesha fedha hizo moja kwa moja kwa Serikali ya Tanzania. Kampuni hiyo inasema inataka kupeleka fedha hizo kwa shirika au mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Uingereza ili kwa kupitia huko, zitumike katika tasnia za kijamii. Membe hataki. Serikali yake haitaki. Wanasema “huu ni udhalilishaji” wa mamlaka ya nchi na raia wake. Wanatutaka kusimama nao kupinga udhalilishaji huo. Kwa jicho la nyongeza, BAE na serikali, wote ni “kashfa tupu.” BAE walitaka kuiba; wakaiba lakini sasa wamepatikana. Dunia inataka warudishe chetu. Lakini walioiba walishirikisha watendaji ndani ya serikali ya Tanzania – kuwezesha au kulainisha au kurahisisha wizi – kwa kutoa ushauri wenye mkengeuko au kunyamazia wizi. Kashfa ni kashfa, lakini kashfa ya serikali inawagusa zaidi na kuwaelemea wananchi. Tangu kufumuka kwa kashfa hii, hakuna lolote la maana ambalo wananchi wameshuhudia serikali yao ikifanya. Baada ya uchunguzi wa jinsi mauzo yalivyofanyika, bei halisi ya rada, waliohusika katika udalali na fedha zilizotolewa, ilitarajiwa serikali ichukue hatua. Bado iko kimya. Shirika la Uingereza la uchunguzi wa makosa makubwa ya jinai (Serious Fraud Office – SFO), lilifanya kazi nzuri. Pamoja na kugundua na kuanika wizi wa kampuni ya nchini mwake; ilitaja Watanzania ambao walishiriki katika wizi huu mkubwa. Serikali haijachukua hatua zozote dhidi ya waliohusika. Hata ilipofahamika kuwa BAE wamekiri ufisadi na kwamba watarejesha fedha hizo Tanzania, bado serikali haijawagusa waliotajwa. Hebu liangalie hivi. Aliyehonga hadi kupata bei kubwa kwa rada ya bei ndogo, amekiri na kutaka kurejesha fedha alizokwapua; serikali ambayo watumishi wake ndio walisaidia wizi, bado iko kimya. Aliyeuza kwa bei ya kuruka anamwangalia yule ambaye watu wake walimsaidia kukwapua mabilioni ya shilingi (serikali ya Tanzania) na kuona hachukui hatua. Anajiuliza: Niwape haohao au zipite kwingine ambako matumizi yake yataonekana? Atakuwa na uhakika gani kwamba fedha hizo zitafika zinakopelekwa? Hapa kuna ukweli na unafiki pia. Ukweli ni kwamba kuna shaka juu ya fedha hizo kufikishwa zinakopaswa kupelekwa na kutumika baada ya kuingia mikononi mwa serikali. Kwa mfano, hadi sasa serikali inasema haijui Kampuni ya Kagoda, iliyoiba zaidi ya sh 40 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT), iko wapi na ni mali ya nani. Lakini wakati huohuo kuna taarifa kuwa serikali ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka Kagoda ili kampuni hiyo isishitakiwe. Serikali ina ndimi mbili. Au, chukua mfano mwingine. Hakuna uwazi wowote kuhusu fedha zilizorejeshwa na makampuni ya kifisadi yaliyoiba kutoka BoT. Maswali ni mengi mno. Nani hao waliorudisha fedha ili wasishitakiwe? Kwani Rais Jakaya Kikwete alisema wakirejesha sehemu ya fedha walizoiba, hawatafikishwa mahakamani. Hapa hoja ni kutofikishwa mahakamani; si kutotajwa hadharani ili watu wajue wezi hao. Hivyo, hatua ya kuweka siri kati ya serikali na wezi, inaiondolea hadhi serikali. Si hivyo tu, hatua hiyo inafanya serikali isigundulike inafanya nini na nani. Inafanyia kazi zake katika giza nene linaloweza kuwa limefunika ufisadi mwingine; labda mkubwa zaidi. Ni mambo haya ambayo yameiweka serikali katika mazingira ya kutiliwa shaka, kutoheshimika na kutoaminiwa. Mlundikano wa kashfa za Meremeta, Deep Green, IPTL, Richmond/Dowans, Kagoda na nyingine nyingi, zinaiacha uchi serikali na kuianika hata kwa wezi wakubwa wanaotumia madalali na “wachonga dili” ndani ya utumishi wa umma. Ni tabia na mwenendo huu vinavyofanya hata mwizi mwingine apate nafasi na ujasiri wa kudharau na hata kunyanyasa serikali. Hapo ndipo tunakuta unafiki wa mwizi wa Ulaya akituhumu “anayelinda wezi” – bila kuwakamata na kuwashitaki ndani ya nchi, kuwa huenda asifikishe kwa wananchi fedha anazotaka kurudisha. Unafiki ni kwamba lini BAE wamegundua umuhimu wa fedha hizo kwa wananchi? Hivi hawakujua hili wakati wanazikwapua? Huu siyo tu mchezo mbaya; ni mchezo mchafu. Katika mazingira haya, Waziri Membe anawataka wananchi kusimama na serikali kupinga “unyanyasaji” wa BAE. Tatizo ni kwamba BAE wanafanya kama wanavyoona serikali inafanya katika maeneo tuliyojadili hapo juu. Wanapata ujasiri. Kama serikali haitaji wezi; haiwi wazi juu ya makusanyo ya fedha kutoka kwa wezi; kama inakaa na watuhumiwa wakuu wa wizi na ufisadi na inakataa kuwakamata na kuwashitaki; basi inajinyima fursa ya kupendwa, kuheshimiwa na kuaminiwa. Serikali inajinyima utetezi wa wananchi wake. Membe anaweza kuacha kulia machozi, akalia damu; lakini ukweli unabaki palepale: serikali yake inafanana na anaowatuhumu kutunyanyasa. Uzalendo hauji tu pale tunapokabiliana na watu au makampuni ya nje. Unapaswa kuwapo wakati wote ndani ya taifa letu na katika mipaka ya nchi. Tayari kuna minong’ono hata ndani ya Bunge kwamba Membe ametoa taarifa yake bungeni kabla ya kushirikisha kamati ya uongozi ya chama chake. Membe anaweza kuwajibu kwa swali: Je, waliokwenda kuiba kwa kuchukua mlungula, waliripoti au kuomba ruhusa kwangu au serikali? Ni ubabe kwa ubabe. Lakini hapo ndipo ulegevu wa serikali ulipofikisha nchi. Hata makampuni ya nje yanakoromea serikali. Hata walioiba wanaweka masharti ya kurejesha fedha. Tumebakiwa na nini? Machozi ya Membe au machozi ya papa? Kwani hata ndani ya Bunge wamo watuhumiwa wa mlungula wa rada. Serikali inawabusu. Inawafuta jasho. Uko wapi uzalendo ambao Membe anataka umsaidie kutunisha kifua kupambana na BAE? Uko wapi?Source: Mtanzania daima
   
 2. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Membe amebebeshwa garasha bila kujua, alipaswa kumshauri mkuu wa kaya kwamba kabla hatujawadai tukamate wezi wetu tuwafungulie mashitaka naamini BAE wangetoa ushirikiano hata wa ushahidi na wahusike wangekuwa keko leo
   
 3. g

  gambatoto Senior Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SITAKI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ahubiri siasa za kuomba huruma.

  Wiki hii bungeni, alilitaka bunge, Watanzania wote na wenye nia nzuri kwa taifa hili, kusimama na serikali kupinga alichoita “udhalilishaji” wa kampuni ya Uingereza.

  Kampuni ya Uingereza inaitwa BAE (BAE Systems plc). Inatengeneza vifaa vya elektroniki vya ulinzi kwa majeshi na vyombo vya usafiri – ndege na meli.

  Ni BAE wanaotengeneza rada za kuongozea ndege – za kiraia na kijeshi na mitambo mingine kwa shughuli hizo. Ni BAE waliouza rada kwa Tanzania kwa “bei ya kuruka” zaidi ya sh 40 bilioni.

  Ni BAE waliogundulika kutoa rushwa kwa baadhi ya watendaji serikalini ili kuwalainisha; ili wakubali kununua rada haraka na kwa bei ya kuruka.

  Baada ya kashfa hii kufumuka, kuchunguzwa na hatimaye kujua kilichofanyika na waliohusika, BAE wamepewa sharti la kurejesha fedha zinazozidi kwenye bei halisi ya rada hiyo.

  Fedha hizo, zaidi ya dola milioni 20 za Marekani (dola 1 = sh 1,500), siyo “chenji” kama wezi wanavyotaka tuamini. Ni fedha zilizoibwa kwa kutumia madalali na mawakala ndani ya nchi; ndani ya serikali.

  Sasa pamoja na BAE kukiri ilichofanya, inasema haitaki kurejesha fedha hizo moja kwa moja kwa Serikali ya Tanzania.

  Kampuni hiyo inasema inataka kupeleka fedha hizo kwa shirika au mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Uingereza ili kwa kupitia huko, zitumike katika tasnia za kijamii.

  Membe hataki. Serikali yake haitaki. Wanasema “huu ni udhalilishaji” wa mamlaka ya nchi na raia wake. Wanatutaka kusimama nao kupinga udhalilishaji huo.

  Kwa jicho la nyongeza, BAE na serikali, wote ni “kashfa tupu.” BAE walitaka kuiba; wakaiba lakini sasa wamepatikana. Dunia inataka warudishe chetu.

  Lakini walioiba walishirikisha watendaji ndani ya serikali ya Tanzania – kuwezesha au kulainisha au kurahisisha wizi – kwa kutoa ushauri wenye mkengeuko au kunyamazia wizi.

  Kashfa ni kashfa, lakini kashfa ya serikali inawagusa zaidi na kuwaelemea wananchi. Tangu kufumuka kwa kashfa hii, hakuna lolote la maana ambalo wananchi wameshuhudia serikali yao ikifanya.

  Baada ya uchunguzi wa jinsi mauzo yalivyofanyika, bei halisi ya rada, waliohusika katika udalali na fedha zilizotolewa, ilitarajiwa serikali ichukue hatua. Bado iko kimya.

  Shirika la Uingereza la uchunguzi wa makosa makubwa ya jinai (Serious Fraud Office – SFO), lilifanya kazi nzuri.

  Pamoja na kugundua na kuanika wizi wa kampuni ya nchini mwake; ilitaja Watanzania ambao walishiriki katika wizi huu mkubwa.

  Serikali haijachukua hatua zozote dhidi ya waliohusika. Hata ilipofahamika kuwa BAE wamekiri ufisadi na kwamba watarejesha fedha hizo Tanzania, bado serikali haijawagusa waliotajwa.

  Hebu liangalie hivi. Aliyehonga hadi kupata bei kubwa kwa rada ya bei ndogo, amekiri na kutaka kurejesha fedha alizokwapua; serikali ambayo watumishi wake ndio walisaidia wizi, bado iko kimya.

  Aliyeuza kwa bei ya kuruka anamwangalia yule ambaye watu wake walimsaidia kukwapua mabilioni ya shilingi (serikali ya Tanzania) na kuona hachukui hatua.

  Anajiuliza: Niwape haohao au zipite kwingine ambako matumizi yake yataonekana? Atakuwa na uhakika gani kwamba fedha hizo zitafika zinakopelekwa?

  Hapa kuna ukweli na unafiki pia. Ukweli ni kwamba kuna shaka juu ya fedha hizo kufikishwa zinakopaswa kupelekwa na kutumika baada ya kuingia mikononi mwa serikali.

  Kwa mfano, hadi sasa serikali inasema haijui Kampuni ya Kagoda, iliyoiba zaidi ya sh 40 bilioni kutoka Benki Kuu (BoT), iko wapi na ni mali ya nani.

  Lakini wakati huohuo kuna taarifa kuwa serikali ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka Kagoda ili kampuni hiyo isishitakiwe. Serikali ina ndimi mbili.

  Au, chukua mfano mwingine. Hakuna uwazi wowote kuhusu fedha zilizorejeshwa na makampuni ya kifisadi yaliyoiba kutoka BoT. Maswali ni mengi mno.

  Nani hao waliorudisha fedha ili wasishitakiwe? Kwani Rais Jakaya Kikwete alisema wakirejesha sehemu ya fedha walizoiba, hawatafikishwa mahakamani.

  Hapa hoja ni kutofikishwa mahakamani; si kutotajwa hadharani ili watu wajue wezi hao. Hivyo, hatua ya kuweka siri kati ya serikali na wezi, inaiondolea hadhi serikali.

  Si hivyo tu, hatua hiyo inafanya serikali isigundulike inafanya nini na nani. Inafanyia kazi zake katika giza nene linaloweza kuwa limefunika ufisadi mwingine; labda mkubwa zaidi.

  Ni mambo haya ambayo yameiweka serikali katika mazingira ya kutiliwa shaka, kutoheshimika na kutoaminiwa.

  Mlundikano wa kashfa za Meremeta, Deep Green, IPTL, Richmond/Dowans, Kagoda na nyingine nyingi, zinaiacha uchi serikali na kuianika hata kwa wezi wakubwa wanaotumia madalali na “wachonga dili” ndani ya utumishi wa umma.

  Ni tabia na mwenendo huu vinavyofanya hata mwizi mwingine apate nafasi na ujasiri wa kudharau na hata kunyanyasa serikali.

  Hapo ndipo tunakuta unafiki wa mwizi wa Ulaya akituhumu “anayelinda wezi” – bila kuwakamata na kuwashitaki ndani ya nchi, kuwa huenda asifikishe kwa wananchi fedha anazotaka kurudisha.

  Unafiki ni kwamba lini BAE wamegundua umuhimu wa fedha hizo kwa wananchi? Hivi hawakujua hili wakati wanazikwapua?

  Huu siyo tu mchezo mbaya; ni mchezo mchafu. Katika mazingira haya, Waziri Membe anawataka wananchi kusimama na serikali kupinga “unyanyasaji” wa BAE.

  Tatizo ni kwamba BAE wanafanya kama wanavyoona serikali inafanya katika maeneo tuliyojadili hapo juu. Wanapata ujasiri.

  Kama serikali haitaji wezi; haiwi wazi juu ya makusanyo ya fedha kutoka kwa wezi; kama inakaa na watuhumiwa wakuu wa wizi na ufisadi na inakataa kuwakamata na kuwashitaki; basi inajinyima fursa ya kupendwa, kuheshimiwa na kuaminiwa.

  Serikali inajinyima utetezi wa wananchi wake. Membe anaweza kuacha kulia machozi, akalia damu; lakini ukweli unabaki palepale: serikali yake inafanana na anaowatuhumu kutunyanyasa.

  Uzalendo hauji tu pale tunapokabiliana na watu au makampuni ya nje. Unapaswa kuwapo wakati wote ndani ya taifa letu na katika mipaka ya nchi.

  Tayari kuna minong’ono hata ndani ya Bunge kwamba Membe ametoa taarifa yake bungeni kabla ya kushirikisha kamati ya uongozi ya chama chake.

  Membe anaweza kuwajibu kwa swali: Je, waliokwenda kuiba kwa kuchukua mlungula, waliripoti au kuomba ruhusa kwangu au serikali? Ni ubabe kwa ubabe.

  Lakini hapo ndipo ulegevu wa serikali ulipofikisha nchi. Hata makampuni ya nje yanakoromea serikali. Hata walioiba wanaweka masharti ya kurejesha fedha.

  Tumebakiwa na nini? Machozi ya Membe au machozi ya papa? Kwani hata ndani ya Bunge wamo watuhumiwa wa mlungula wa rada. Serikali inawabusu. Inawafuta jasho.

  Uko wapi uzalendo ambao Membe anataka umsaidie kutunisha kifua kupambana na BAE? Uko wapi?

  Membe anapolia mbele ya mafisadi
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ulitaka kwa nafasi yake kama Waziri wa Mambo ya Nje afanye nini? Vyombo vya uchunguzi na mashtaka vimepewa meno ya kuuma na wako kimya. Je, yeye aende akakamate watu? Ndiyo wajibu na mamlaka yake?

  Amefanya kile ambacho kitafanikisha kile alichotumwa kukifanya ambacho ni kuhakikisha fedha hizo zinarejea kwa msingi na utaratibu unaolinda heshima ya nchi yetu, na si vinginevyo.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  <BR><BR>

  Havina uhusiano na wala hicho unachosahuri kikifanyika hakitaondoa haki ya kuheshimiwa kwetu na kutaka haki yetu ije kwetu kwa namna tunayotaka sisi. Kwa hilo Ndimara sijui kama amelifikiria vizuri au ameamua tu kuwa critical!
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hii hela sio haki yetu wameturuzuku kwa misingi ya watu wao kutofunguliwa mashitaka nchi uingereza lakini kama BAE wangewananga watu wao sisi tusingepata kitu maana tulinunua bila kulazimishwa na mtu.

  hisitoshe hatukuwalipa bilioni 78 wao wameamua tuturudishia zaidi na rada juu

  ndio maana na sisi tunatakiwa kulupa ghalama kama waliyolipa wao kwa wala rushwa wetu.
  kuna watu wanapotosha ya kwamba hii kesi iliamuliwa na mahakama hiyo sio kweli haya ni makubaliano kati ya BAE na SFO na kusainiwa mahakamani sasa sisi haki yetu kupewa hela na rada hiko wapi kama sio fadhila, lakini tunashindwa kushika wezi tunakalia kulilia heshima
  nani anaye heshimu ili taifa
  hao kenya majira tu wanatuvuluga kila siku
   
 7. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijaona mapungufu ya Ndimala kwenye taarifa hii zaidi naona tu Serikali ilivyoshindwa kuonyesha nia ya kumkwamua Mtanzania na kujidhihirisha moja kwa moja kua hawapo kwa maslahi ya TAIFA .....Sijui ni nini kimewapata hawa CCM Yaani hadi mlipaji yupo tayari kulipa na serikali haijui nini ifanye ..........dah!!!
   
 8. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  membe anataka kutumia kashfa ya rada kuisambaratisha kambi fulani ya urais kuelekea 2015 anajua lazima mwisho wachafuke, yeye kachokonoa tu, ccm mbio za uraisi umeanza mapema
   
 9. N

  Nzogupata Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uingereza watunyime tu hiyo hela kwani walipoidhinisha ujenzi wa nyumba 25000 za wlimu walijenga ngapi? leo wanakuja na orodha ndefu yakuombea hela kwa ajili ya elimu? kama BAE systems wasingekwapua hela ya madawati na vitabu wangetoa wapi
   
 10. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Membe, Ndimara hajakosea hata kidogo. Ulionekana kulopoka kama mtu asiyefikiri kuna mtu mwenye uchungu na nchi yake pale bungeni hasa nyie mlioshika hatamu? Watanzania tulikuangalia tu na kunyamaza lakini kama sauti zetu zingeweza kupenyeza wakati ule ule usingemalizia.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tuache kusoma siasa, na hasa siasa za 2015 katika masuala ya kitaifa kama haya. Ulitaka hizi fedha zidaiwe na Waziri wa Jinsia, wanawake na watoto ndiyo ujue kwamba hakuna uhusiano na siasa za uchaguzi? Mimi sioni kudai fedha zirejeshwe serikali kunasambaratish vipi kambi fulani, unless unataka tuamini kwamba kambi hiyo inahusika katika kufanya BAE wafikie maamuzi haya yanayopingwa.
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sakata la BAE kuwasolishwa bungeni ni mwendelezo mwingine wa kuwaengua chenge na Rostam.......na membe ametumwa na mkuu wake wa Kaya ili kulileta Bungeni.........tusubiri mtaona,kwa sababu BAE haitojadiliwa bila kutaka kuwabaini wahusika.......nyie tusubiri
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sioni mantiki ya hoja ya Ndimara. Kazi ya Membe ilikuwa ni kuwataka wawakilishi wa wananchi kuungana katika harakati za kulinda heshima ya nchi yetu dhidi ya huu uhuni wa watu wanaodhani wana haki ya kutupangia kitu cha kufanya kwa kile ambacho ni haki yetu.
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,489
  Trophy Points: 280
  Anajiweka sawa aonekane ili apate urais 2015, "SIDANGANYIKI"
   
 15. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80

  We mbopo naona you just dont get it. Unasisitiza "heshima" ya nchi yetu watu hapa wanabaki kukushangaa. Unazungumzia heshima gani kama serikali yenyewe, at the first place, ndio imesaidia nchi kupoteza heshima mbele za jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuchukua hatua mebele za watumishi wake waliofacilitate huu ufisadi wa rada na mwingineo mwingi?

  Pesa sawa ni haki yetu. Lakini kitu ambacho watanzania wanastahili sana kama haki yao ya kwanza kabisa sio hizi pesa billioni thelathini. Ni haki ya kuhakikishiwa kwamba watuhumiwa wa ufisadi wa rada waliomo kwenye serikali ya membe wanapata justice yao. Membe aseme anavyosema hivi sasa baada ya kuwa mafisadi wa rada wapo mahakamani. Hapo ataleta sense.
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Membe is not the head of PCCB, nor is he the Police Chief, Attorney General or the Director of Public Prosecutions. Anazungumzia kile ambacho kinahusiana na docket yake. Kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa wizi huo siyo condition precedent ya kulipwa fedha hizi. After all hao BAE nao ni watuhumiwa wa ufisadi. Kwa nini wapange masharti tofauti na yale ambayo Jaji aliyatoa?
   
 17. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Well, point hapa ni kwamba membe anasimama kama msemaji wa serikali katika suala hili la malipo ya rada. Na tunafahamu kwamba hii ni intergrated governement: wizara hii inahusiana na wizara hii kuhakikisha kwamba kile kinachotoka nje ni makubaliano ya serikali kwa ujumla. Sasa kama membe si prosecutor general haisaidii kuongeza credibility ya serikali mbele ya wananchi na jumuia ya kimataifa katika suala hili. We take it serious that this government has no claim power whatsoever on this money until it takes it seriously first things first. Sasa serikali inapata wapi audacity ya kuclaim kwamba hizi hela zipitie kwake wakati haijafanya chochote on the ground kuthibitisha kwamba inastahili kupewa hizi hela?
   
 18. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe Bwana mdogo Mbopo unaongea pumba pumba pumba pumba tu. Unalilia heshima gani ambayo kwa ujinga wako umeipoteza mwenyewe?? Hapa wakuwaona wa maana ni hawa wazungu ambao angalao wametuonea huruma baada ya hela zetu kufisadiwa na wajanja wachache wa nchi hii. Wangeamua kukaa kimya wasizirudishe hizo hela mngefanyaje, mngewashitaki?? Leo hii wamewahurumia na kuamua kuwarejeshea angalao kidogo mnawawekea masharti, na masharti yenyewe ili mpewe hizo hela mgawane na jamaa zenu?? wale wanajua kitakachotokea wakiipa serikali hizo hela na ndiyo maana wanataka wawape taasisi ifanye kitu kitakachoonekana mbele ya ulimwengu kwamba ile hela iliyorudishwa imefanya hiki na kile ambapo wakipewa serikali ya Tanzania zitaishia mifukoni mwa wajanja. Acheni upuuzi huo. Anachoongea Membe ni kutufunya watanzania hatuna kitu kichwani kabisa. Acheni pumba hizo.... mtaelimika lini wadanganyika?????????
   
 19. p

  plawala JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi kabisa ni hivi,haki ya kwanza ni kushitakiwa kwa wezi,haki ya pili ni kurudishiwa fedha zilizoibwa,tujiheshimu kwanza ili tuheshimiwe,tusijidhalilishe kwanza ili tusidhalilishwe kama nchi
  Ndimara uko sahihi
   
Loading...