Ndesamburo ashitukia mgawo wa umeme

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Ndesamburo ashitukia mgawo wa umeme

2009-04-02 11:31:36
Na Simon Mhina

Mbunge wa Moshi Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Philemon Ndesamburo, amesema kuna kila dalili kwamba mgawo wa umeme unaoendelea ni hujuma zenye lengo la kuwafanya Watanzania waikubali Dowans.

Kwa jinsi hiyo amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Dk. Idris Rashid kutoa maelezo ya kina.


Akizungumza na Nipashe jana, Ndesamburo alisema yeye anahisi kwamba mgawo unaoendelea `umetengenezwa` kwa makusudi na watendaji wa Tanesco, baada ya jaribio lao la kununua mitambo chakavu ya Dowans kugonga mwamba.


``Tunataka Mkurugenzi wa Tanesco atueleze kwamba vile vitisho vyake alivyotoa kwamba nchi itaingia gizani, ndio hivi vimeshaanza kufanya kazi kwa mtindo wa reja reja?``

Alihoji Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro. Alisema wakati fulani Rais Jakaya Kikwete aliutangazia umma kwamba kutokana na kukamilika kwa miradi kadhaa ya nishati, suala la mgawo litakuwa historia, hivyo watendaji wanatakiwa kueleaza kwa nini wanakwenda kinyume na ahadi ya mkuu wa nchi.

Alisema taarifa alizonazo ni kwamba mabwawa yote ya kuzalisha umeme kote nchini yamefurika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kila pembe.


``Zamani walikuwa wanasema mabwawa yamekauka, sasa kila mahali mvua inanyesha, kwa nini umeme haupatikani?`` Alihoji Mbunge huyo.

Alisema inavyoonekana ni kwamba kuna watu walishapanga zoezi la ununuzi wa mitambo hiyo na kudhani wamefanikiwa, hivyo wameamua kuwaadhibu wananchi.

Hata hivyo, Ndesamburo alionya kwamba hujuma yoyote dhidi ya Tanesco haitavumiliwa na wananchi, ambao kwa kiasi kikubwa wameshafahamu njama zinazofanyika.


SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom