Ndege za Japan zajibu "tisho" la Uchina

Ndege za Japan zajibu "tisho" la Uchina

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,483
Reaction score
167,073
Japan imeziamuru ndege zake za kivita zipae angani baada ya ndege ya serikali ya Uchina kuingia katika anga ya visiwa vya Bahari ya Mashariki mwa Uchina kwa muda, duru rasmi zimesema.
Msemaji wa serikali Osamu Fujimura alisema kuwa Japan iliamuru ndege za kivita za aina ya F-15 zipae angani wakati ndege hiyo ya Uchina ilipoonekana.
Tukio hilo lilipotokea tu, Japan "iliilalamikia" Uchina “mara moja”, shirika la habari la Kyodo lilimnukuu akisema.
Visiwa hivyo, vinavyojulikana kama Senkaku nchini Japan na Diaoyu nchini Uchina, vimegombaniwa na nchi hizo mbili kwa muda mrefu sasa.
Safari ya kawaida
Walinzi wa baharini wa Japan nao pia walisema kwamba meli za Uchina zinazofanya uchunguzi nazo zilionekana karibu na visiwa hivyo mapema siku hiyo.
Kwa upande wake, Uchina imesema kwamba safari ya ndege yake hiyo ni jambo la kawaida.
Japan ndiyo inayomiliki visiwa hivyo, ambavyo pia Taiwan inadai ni vyake.
Bahari inayozunguka vi

siwa hivyo ina samaki wengi na pia inadhaniwa kwamba ina mafuta.
Mmiliki
Japan ilitwaa visiwa vitatu kutoka kwa mmiliki Mjapani wa kibinafsi mnamo mwezi Septemba, lakini kitendo hicho kilizua malalamishi ya kidiplomasia na kutoka kwa raia nchini Uchina.
Tangu hapo, meli za Kichina zimekuwa zikionekana katika eneo la visiwa hivyo, jambo ambalo limeisababisha Japan kutoa onyo mara kwa mara

Ndege za Japan zajibu "tisho" la Uchina - BBC Swahili - Habari

Hapo kumekucha, Ila kiukweli ni Rahisi China kupigana na USA kuliko Japan, na Ni rahisi JApan kupigana na URUSI kuliko China

Hizi nchi ni kama Binadamu na Damu yake, Japani Ndo partner namba 1 wa biashara wa China, so China Inaitegemea sana Japani katika biashara, Na Japani inaitegemea sana China, Inauza China kuliko kwingineko, kupigana kwao kutamnisha China inaweza kujikuta ni ya 5 kwa uchumi badala ya 2 na hivyo hivyo kwa JPN
 
Ur totally wrong, wrong....!!!

It seems ur international diplomatic & military know-how... is 00%, ndio maana exams people get 00% whatever the subject is, MOST DON'T KNOW....!!!

Godbless u...!!

Yah tnx kwa kuwahi kumwambia what i wanted to tell him
 
Ur totally wrong, wrong....!!!

It seems ur international diplomatic & military know-how... is 00%, ndio maana exams people get 00% whatever the subject is, MOST DON'T KNOW....!!!

Godbless u...!!

if the man is telling lies then give us the truth
 
if the man is telling lies then give us the truth

Mkuu jamaa huyu nimekwisha muona mara nyingi akiwaponda wenzake kwa lugha za ajabu, lakini kwa bahati mbaya sijawahi kuona anatoa majibu mbadala!! We jaribu kumfatilia majibu yake utashangaa sana.
 
Vita yao itakuwa mbaya sana na wazungu lazima wataisadia Japan, ndio mwanzo wa kuimaliza China
 
Back
Top Bottom