Ndege yaanguka...

Kanyafu Nkanwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2010
Posts
850
Reaction score
103
Kinachonishangaza hapa ni hii habari kuwa abiria wa ndege bado hawajaokolewa toka ndege ianguke! Huku Africa, ukiwa mzima shukuru Mungu wako sana.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/3587-ndege-yaanguka-morogoro

Geofrey Nyang'oro

NDEGE ndogo ya Kampuni ya Safari Linck iliyokuwa imebeba watalii kuwapeleka Mbuga ya wanyama Selous, imeanguka.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa Usama wa kampuni hiyo, Azizi Abdallah ambaye ni rubani, alisema tukio hilo liitokea jana katika eneo la Matombo, mkoani Morogoro.

Abdallah alisema ndege hiyo ilikuwa imebeba watalii wawili ambao walikuwa wanakwenda kuangalia wanyama katika mbuga ya Selous, mkoani humo na kwamba ndege hiyo, ilikuwa ikiendeshwa na rubani kutoka Norway.

"Ndege hii ndogo yenye namba ya usajili 5HMG1 imeanguka leo (juzi) saa 10:00 jioni, mpaka sasa haijaokolewa na tunaendelea na juhudi za uokoaji," alisema Abdallah.

Abdallah alifafanua hadi jana abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo, walikuwa hawajaokolewa.
 
Navyo hivi vindege vidogo jamani hata usalama wake sijui huwa unahakikishwaje. Nimeshapanda mara ukakuta rubani ndege imeanze kusogea hata mlango hajafunga (mzungu tena), mara vikipaa juu hakuna hewa ndio mkitua tu wanakuja haraka kuwafungulia mlango oksijeni iingie. Unapanda tu hiyo basi lakini inasikitisha sana.
 
Vindege vidogo vya huku kwetu ni makaburi yanayotembea
 
Vindege vidogo vya huku kwetu ni makaburi yanayotembea

Yes. Nahisi hamna service na pia wengi wanachukulia kama sehemu ya kujifunzia kwa kuwa hakuna umakini mamlaka ya Anga TZ kama zilivyo nchi jirani zingine. Kuna siku nimepanda kimoja cha kampuni ya Tropical Air. Mwenye ndege, babu mmoja hivi kama muhindi/mswahili, alikuwa na rubaki mwingine mwanamke. Kumbe yule babu alikuwa anamfundisha yule mwenzake huku wamechukua abiria 13! On landing pale Dar, ile ndege ilibamiza chini, haikutua kama tulivyozoea. Tunafika lounge ya terminal one, tunakuta gumzo, kuwa,,,, bado hajajua yule angalia alivyoishusha! Hii ni mbaya sana na nadhani iko kwa nchi kama bongo tu.
 
"mpaka sasa haijaokolewa na tunaendelea na juhudi za uokoaji," alisema Abdallah.

I like the statement sorry i meant tz!
 
usalama wa anga kwa nchi za africa ni kutegemea mungu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…