Mkuu ugomvi unahusu ujenzi/kutandaza bomba la kusafirisha gesi kwenda Ulaya kupitia Syria, Asaad alikataa mradi huo husipitia mchini mwake maana alijua huo ulikuwa ni mpango mahususi wa Marekani na Qatar kutaka kujuhumu Warusi wasiuze gesi yao kwa wingi huko Ulaya, kinacho shangaza zaidi Wamarekani walitaka kusafirisha gesi kutoka kwao kwa Meli gesi inateremushwa Qatar na kusafirishwakwa bomba mpaka Ulaya, kama mpango huo ungefanikiwa Walaji/Wateja wange inunua kwa bei gani!! Yaani Amerika ilichochea uasi nchini Syria kwa maslahi yake including kutaka kuihujumu Urusi kibiashara/Uchumi.
Raia wa Syria hawakuwa na matatizo yoyote na Rais wao, ugomvi unao endelea hapo ni wa kuchonga tu, inavyo elekea sasa Amerika hipo determined kuigawa Syria na part ya Iraq kutengeneza nchi ya Wakurdi na kuweka mapuppet wa kulinda maslahi yao si ajabu sehemu hiyo ndiyo wanataka bomba la gesi lipitie kwenda Ulaya. Binafsi sioni kama Syria, Iraq, Urusi,Turkey na Iran watakubali upuuzi huo, Turkey kwa mfano haitaki kabisa uanzishwaji wa Nchi ya Wakurdi, kumbuka Wakurd wapo mpaka Iraq, Syria na Iran.
Binafsi ni kitu gani nakiona kinaweza kutokea ndani ya mwezi mmoja au miwili ijayo, Wamerika watawapa waasi makombora mazito yenye multiple roketis kushambulia jeshi la Syria wakiwa na Washauri kutoka Marekani na Israel, ndege za NATO tuseme Marekani zitaendlea kushambulia sehemu ya Syria ambayo wanadai wapiganaji wano ungwa mkono na wao wamejichimbia, sasa kuna mji muhimu kasikazini ambao unakaliwa na ISIS mjio huo unapaniwa na Waasi wa Syria wakisaidiwa na Amerika ili wauteke kwa mawazo yangu nadhani Amerika inataka Syria ikigawanyika basi mji huo ndio uwe makao makuu ya aidha wasi au Wakurdi - Jeshi la Serikali nalo limepania kukomboa mji huo na wako karibu lakini nasikia makombora na wakati mwingine ndege za Marekani na Israel utumika kujaribu kuzuia mji huo usikombolewa na Jeshi la Syria.
Katika sakata hili nina uhakika Urusi na Iran hazitakubali mji huo uwe chini ya mappuppet wa Marekani, binafsi nafikiri ugomvi wa kugombania mji huo ndiyo unaweza kufumua vita vikali sana na possibly WW3, siku za karibuni kwa mfano: Amerika imeonyesha imejiweka tayari kwa vita ndiyo maana unaona inadai kwamba sehemu fulani ndani ya aridhi ya Syria wanamgambo wanao muunga mkono Asaad pamoja na jeshi la Syria hawaruhusiwi kutia mguu, kumbuka hiyo ni aridhi ya Syria na wala Amerika haijapewa kibali na umoja wa Mataifa kuweke jeshi au zana za kivita sehemu hiyo na wala Serikali ya Syria haikuwaalika waje kumsaidia Asaad kupigana na ISIS, wamejiamria tu kutokana na jeuri zao na kiburi. Sakata la Syria naona Amerika inataka kufanya miscalculation na itakuja kuwa-cost Dearly wao wanataka kupigania maslahi lakini Syria, Urusi na Iran watapigana for survival, kama vita avitawafanya walazimike for nuclear exchange baina yao nawahakikishieni Wamerika na washiraka wao watanyukwa kweli kweli, Australia kwa mfano imekwisha nusa hatari hiyo ndiyo maana wameamua kuondoa ndege zao.