Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Hii ni habari kwa mujibu wa ITV ambayo mimi binafsi nimechelewa kuisikiliza ila ni habari inayosomeka katika maandishi yanayopita chini ya screen wakati taarifa ya habari inaendelea.
Ni matengeno gani? Aliyesikia atujuze.
=======
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege nchini(ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi amekanusha taarifa kuwa, ndege ya Dreamliner 787-8 ina hitilafu na kwamba ilisitisha safari yake ya Mwanza - Dar kuanzia juzi.
Amesema katika ndege nne za ATCL (3-Bombardia na 1-Dreamliner), Bombardia zinaendelea na safari bila matatizo ila Dreamliner imesimamishwa ili ifanyiwe marekebisho
Marekebisho hayo ni kama ya WIFI na mengine madogo madogo yanayohusu uendeshaji wa ndege maana safari za ndege hiyo kwa sasa ni za majaribio kwa Marubani
Ameeleza kuwa walipanga marekebisho hayo kufanyika baada ya wiki tatu baada ya kuanza safari zake, ila kilichopelekea marekebisho yafanyike sasa ni mafundi walioomba yafanyike mapema kwa kuwa wanaondoka nchini
Marekebisho hayo yaliyoanza juzi yanatarajiwa kukamilika leo na hivyo ndege hiyo kuanza safari zake kama kawaida hapo kesho
Habari zaidi, soma=>Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner imeharibika kuanzia jana jijini Mwanza abiria tumeshindwa kuendelea na safari leo - JamiiForums