FisadiKuu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 8,167
- 13,443
Habari wanabodi...
Mnamo tarehe 30.3.2016 Waziri Mbarawa aliwaambia wadau kwamba serikali imekubaliana na Shirika la kutengeneza ndege la Canada na ndege hizo zingeingia nchini ndani ya siku 60 kutoka tarehe 1.4.2016.
Cha kushangaza ni kwamba jana nimesoma habari wanasema wamekubaliana na shirika la Urusi na ndege zitanunuliwa kutoka Urusi na zitaingia nchini mwishoni mwa mwaka huu.
Je hapa tunachezewa akili au tunadanganywa kama watoto?? Ni kweli wanataka kulifufua shirika au wanasema kufurahisha watanzania tu??
Mh. Rais alisema ATCL kuna majipu, sasa je kama kweli wanataka kuleta ndege mbona hayo majipu hayajaondolewa ili shirika libaki na watu safi??
Nilikuwa na imani sana na hii serikali lakini kwa kauli hizi za uongo uongo nimeanza kupoteza imani yangu kwao.