Ndege kwa matumizi ya Rais wetu

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Mwaka 2004, kulizuka mjadala mkubwa sana miongoni mwa wananchi, baada ya Serikali ya awamu ya tatu, chini ya hayati Rais Benjamin William Mkapa, kufanya maamuzi ya kununua ndege maalumu kwa ajili ya matumizi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa safari za ndani na nje ya nchi.

Hoja kubwa ya wananchi kwa wakati huo, ilikuwa ni ni gharama kubwa za ndege hiyo, ukizingatia na uwezo wa serikali kwa wakati huo.

Baada ya mjadala kupamba moto, aliyekuwa waziri wa fedha wa wakati huo, marehemu Basil Pesambili Mramba , alitoka hadharani na kutoa kauli, "ni bora watanzania kula hata nyasi lakini ndege ya Rais ni lazima inunuliwe".

Kweli ndege ya Rais ikanunuliwa, ndege aina ya Gulfstream G550 kwa thamani ya takribani bilioni 47 kwa wakati huo, ndege hiyo ilisajiliwa kwa namba za usajili 5H- One, ni ndege ya kisasa kabisa na yenye uwezo wa kusafiria masafa marefu( long range) na kwa Tanzania ina uwezo wa kutua kwenye viwanja vya Dar es Salaam, Zanzibar, Songwe, Kilimanjaro, Mwanza, Dodoma, Chato na Mtwara.

Kwa siku za karibuni, binafsi nimekuwa nikiona mheshimiwa Rais wetu mama Samia Hassan Suluhu, akitumia zaidi ndege yetu ya Airbus 220-300, ambazo kimsingi ni ndege zilizonunuliwa mahusisi kwa matumizi ya kubeba abiria( Commercial plane)

Nilidhani ni vizuri zaidi, ile ndege yetu maalumu kwa matumizi ya mheshimiwa Rais( Gulfstream G550) ingeendelea kutumika kwa matumizi hayo ya safari za mheshimiwa Rais na viongozi wengine wakuu wa serikali ndani na nje ya nchi.

Kwa sababu ndege ile tulinunua kwa fedha nyingi za walipa kodi wa nchi yetu, kama ina changamoto zozote ni vyema changamoto hizo zingerekebishwa na iendelee kutumiwa na mheshimiwa Rais wetu kama ilivyokusudiwa wakati ikanunuliwa.

Hasa ukizingatia mheshimiwa Rais wetu wa sasa, amekuwa akitumia zaidi usafiri wa ndege kwenye kutekeleza majukumu yake ya urais, tofauti na mtangulizi wake, ambaye mara nyingi akitumia zaidi usafiri wa gari.

Kwa sababu, ndege hizo za abiria zikiendelea kutumika mara kwa mara kwa matumizi ya viongozi wetu wakuu, inaweza kuleta changamoto kwa shirika letu la ndege( ATCL) kwa kuzingatia malengo ya muda mrefu na muda mfupi ya shirika hilo kuongeza safari nyingi zaidi za ndani na nje ya nchi yetu, hivyo ndege nyingi zaidi zitahitajika.
 
Matokeo ya ziara zao yamefanya ndege ya kusafiria kutoka Mwanza na Dodoma kuwa admi sana leo hadi alhmai
 
Inashangaza rais kila anakoenda nchini anatumia ndege ya atcl ya ujazo watu zaidi ya 170. Sijui amezungukwa na washauri gani? 😂😂
 
R.I.P makamanda wetu enzi hizo Chief.Mkwawa na wengineo.

Mlipambana na utumwa kutoka kwa mtu mweupe ila leo kuna wenzetu wametugeuka.
 
Mwaka 2004, kulizuka mjadala mkubwa sana miongoni mwa wananchi, baada ya Serikali ya awamu ya tatu, chini ya hayati Rais Benjamin William Mkapa, kufanya maamuzi ya kununua ndege maalumu kwa ajili ya matumizi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa safari za ndani na nje ya nchi.

Hoja kubwa ya wananchi kwa wakati huo, ilikuwa ni ni gharama kubwa za ndege hiyo, ukizingatia na uwezo wa serikali kwa wakati huo.

Baada ya mjadala kupamba moto, aliyekuwa waziri wa fedha wa wakati huo, marehemu Basil Pesambili Mramba , alitoka hadharani na kutoa kauli, "ni bora watanzania kula hata nyasi lakini ndege ya Rais ni lazima inunuliwe".

Kweli ndege ya Rais ikanunuliwa, ndege aina ya Gulfstream G550 kwa thamani ya takribani bilioni 47 kwa wakati huo, ndege hiyo ilisajiliwa kwa namba za usajili 5H- One, ni ndege ya kisasa kabisa na yenye uwezo wa kusafiria masafa marefu( long range) na kwa Tanzania ina uwezo wa kutua kwenye viwanja vya Dar es Salaam, Zanzibar, Songwe, Kilimanjaro, Mwanza, Dodoma, Chato na Mtwara.

Kwa siku za karibuni, binafsi nimekuwa nikiona mheshimiwa Rais wetu mama Samia Hassan Suluhu, akitumia zaidi ndege yetu ya Airbus 220-300, ambazo kimsingi ni ndege zilizonunuliwa mahusisi kwa matumizi ya kubeba abiria( Commercial plane)

Nilidhani ni vizuri zaidi, ile ndege yetu maalumu kwa matumizi ya mheshimiwa Rais( Gulfstream G550) ingeendelea kutumika kwa matumizi hayo ya safari za mheshimiwa Rais na viongozi wengine wakuu wa serikali ndani na nje ya nchi.

Kwa sababu ndege ile tulinunua kwa fedha nyingi za walipa kodi wa nchi yetu, kama ina changamoto zozote ni vyema changamoto hizo zingerekebishwa na iendelee kutumiwa na mheshimiwa Rais wetu kama ilivyokusudiwa wakati ikanunuliwa.

Hasa ukizingatia mheshimiwa Rais wetu wa sasa, amekuwa akitumia zaidi usafiri wa ndege kwenye kutekeleza majukumu yake ya urais, tofauti na mtangulizi wake, ambaye mara nyingi akitumia zaidi usafiri wa gari.

Kwa sababu, ndege hizo za abiria zikiendelea kutumika mara kwa mara kwa matumizi ya viongozi wetu wakuu, inaweza kuleta changamoto kwa shirika letu la ndege( ATCL) kwa kuzingatia malengo ya muda mrefu na muda mfupi ya shirika hilo kuongeza safari nyingi zaidi za ndani na nje ya nchi yetu, hivyo ndege nyingi zaidi zitahitajika.
Samahani,hiyo ndege life span yake ni mda gani?
Naona kama ni ya mda mrefu sasa,na imepata mtumiaji mzuri,kila siku ipo angani.
Napata mashaka kama itakuwa chakavu,ije ishuke na mtu.
 
Back
Top Bottom