Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Inaitwa HAV304. Imetengenezwa na kampuni inayoitwa Hybrid Air Vehicles. Inaweza kukaa angani kwa muda wa wiki 3 na nusu. Itauzwa kwa bei ya paundi millioni 30. Itaweza kubeba abiria 50 na tani 50 (kilogramu 50,000) za mzigo.
Itakuwa na uwezo wa kutua kwenye barafu, kwenye maji na nchi kavu. Itakuwa na sehemu za helicopter na ndege ya abiria ya kawaida. Hivyo haitahitaji uwanja wa ndege ili kutua.
Baadhi ya kampuni za ndege zimeonesha kwamba zinataka ndege hiyo, lakini bado haijapata wateja wengi.
Mambo yakienda sawa, hii ndiyo itakuwa ndege kubwa zaidi duniani. Kwa sasa, ndege aina ya Airbus A380-800 ndiyo ndege kubwa zaidi duniani. Ina uwezo wa kubeba aibiria zaidi ya 250!