Ndege aina ya Bombardier Q400 kuanza safari zake za kuruka na kutua katika Uwanja wa ndege Songea

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Serikali imesema ndege aina ya Bombardier Q400 itaanza safari zake za kuruka na kutua katika Kiwanja cha ndege cha Songea ifikapo Septemba mwaka huu ili kufungua fursa za kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameyasema hayo akiwa mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi kukagua hali ya miundombinu ya barabara, madaraja na kiwanja cha ndege, ambapo ameridhishwa na hatua zilizofikiwa za ukarabati wa kiwanja hicho, ikiwemo uboreshaji wa barabara ya kutua na kuruka yenye urefu wa mita 1740, maegesho ya ndege na taa za kuongozea ndege.

Waziri Kamwelwe ameongeza kuwa, ukarabati na uboreshaji wa kiwanja hicho unagharamiwa na fedha za ndani kwa kiasi cha shilingi bilioni 37 na unatarajiwa kukamilika Desemba, 2020.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Lazeck Alinanuswe, amesema mpaka sasa mkandarasi amefikia asilimia 60 ya kazi ya ujenzi wa tabaka jipya la lami katika uwanja huo.
 
37 fcuking billion?

A single regional airport?

With probably 1 flight a day?

Impact yake kiuchumi ni kubwa kiasi hiko kweli? Were there no better things to do?

kwahio hawana haki ama unamaanisha nn? are you a racist?
 
si ndo maaana kuna usafiri wa afadhali, duniani kote ndege ni usafiri ghali kwa apa tz kidogo its becomming cheap ila ni kawaida sana kua expensive: kama ni ghali kwako means pull up your socks uweze kumudu


Superfeo weka pembeni
 
Back
Top Bottom