Nelson Kileo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 3,054
- 3,263
Akiwa anaongea kwenye mahojiano moja kwa moja na mtangazajiwa BBC SAHILI Charles Hillary ...
Dk Mkumbo ameonekana akiutetea ushoga na kusema Museven kajivika ubabe aisiokua na uwezo nao .. Ni baada ya kuulizwa anaonaje issue juu ya Uganda na misaada iliyozuiwa na world bank baada yakupitishia sheria kali ya kuzuia ushoga ..
Kitila mkumbo kwa jinsi aliivyoongea ananyesha kabisa kwamba ni lazima nchi za Africa kuukubali ushoga .
============================
Ufafanuzi toka kwa Dr. Kitila Mkumbo
============================
Dk Mkumbo ameonekana akiutetea ushoga na kusema Museven kajivika ubabe aisiokua na uwezo nao .. Ni baada ya kuulizwa anaonaje issue juu ya Uganda na misaada iliyozuiwa na world bank baada yakupitishia sheria kali ya kuzuia ushoga ..
Kitila mkumbo kwa jinsi aliivyoongea ananyesha kabisa kwamba ni lazima nchi za Africa kuukubali ushoga .
============================
Ufafanuzi toka kwa Dr. Kitila Mkumbo
============================
Tusipotoshe. Katika mazungumzo yangu sikutetea wala kupinga ushoga kwa sababu hiyo haikuwa mada. Nilichosema:
i) Misaada kutoka nchi za magharibi huambatana na masharti. Masharti mengi yanalenga katika kuchochea utawala bora hasa ukilenga kukuza demokrasia ya kimagharibi na kulinda haki za binadamu. Moja ya haki ambazo zinalindwa sana na nchi za kimagharibi ni haki za wapenzi wa jinsi moja.
Kwa hiyo ilitarajiwa kwamba nchi hizo zingeikatia misaada nchi ya Uganda pale ambapo Rais Museveni angesaini sheria inayotoa adhabu kali kwa wapenzi wa jinsi moja. Nikasisitiza hakuna njia ya kukwepa masharti haya kama nchi za kiafrika zitaendelea kutegemea misaada kutoka magharibi. Hatuwezi tukala keki na tukawa nayo at the same time.
ii) Viongozi wa kiafrika wanapenda kujivika ujasiri bandia katika mambo yasiyo na tija. Katika bara la Afrika kuna matatizo mengi na makubwa zaidi kuliko ushoga. Lakini wanatumia kadi ya ushoga kwa sababu ni swala gumu katika bara la Afrika ili kujipatia umaarufu hewa. Ushoga haliwezi kuwa tatizo kubwa kuliko rushwa na wizi wa raslimali unaoendelea bara la Afrika.
Rais Museveni ana matatizo makubwa ya kiutawala na hali yake kisiasa si njema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2016 na anatumia hili la ushoga ili kujikweza na kujiweka sawa katika kuwasaulisha waganda matatizo ya kisiasa na kiuchumi yaliyosababishwa na utawala wake. Anatumia pia kadi ya ushoga ili aendelee kugombea kiti cha urais wakati alipaswa kuondoka juzi.
Bahati mbaya mawasiliano yalikatika na nikaishia hapo.