Ndanda FC Yatishia Mgomo

Dark Angel

JF-Expert Member
Sep 12, 2013
212
220
Wachezaji wa timu matata ya Ndanda FC waazimia kugoma,kushinikiza walipwe malimbikizo ya mishahara yao.

Timu yetu imekumbwa na ukata hali inayotishia umahili wetu,alisema mmoja wa wana ndanda.

#MT
 
Asee, hii timu inayumbishwa na watu wachache wapenda sifa na ulaji.
Ila kuna Mbunge wa jimbo la Tandahimba Katani A. Katani juzi aliwapa fedha baada ya kuifunga timu ya Mwadui,. Hata ile game ambayo walicheza na Azam baada ya kupata sare aliwapa fedha taslimu Sh.500000/=, na ameahidi kuendelea kutoa Mil 1 kwa kila mechi ambayo watakuwa wanashinda.
Ndanda timu ya nyumbani ila huwa inaniboa sana namna ya uchezaji wake hasa inapokutana na MIKIA.
 
Wakukaya!! Labda wanalambishwa asali kidogo ili walegeze wanapokutana na baadhi ya mechi. Maana wanakuwaga njema sana wakiamua. Chunguza game za Yanga na Azam walivyogangamala.
 
Simba ni timu ya kijamaa, ndada ni timu ya kijamaa, kamwe hatuwezi kubaguana, ni kusaidiana tu kulingana na nafasi na uhitaji wa matokeo kwa timu hizi..

Timu nyingine za kijamaa ni Majimaji FC, Coastal Union, n.k

Ila, Yanga ni timu ya kibepari hivo haiwezi changamana na Ndanda Kuchele wala timu yoyote nyingine ya kijamaa, Toto Africans ni Mabepari pia.

Azam inatumia mifumo yote miwili.. Ujamaa robo na ubepari Robo tatu.
 
Back
Top Bottom