Kumekuwepo na Kipande cha Video kinacho sambaa kwenye Mtandao wa Facebook kikimuonesha Nchimbi akisema Samia Must Go huku akieleza kuwa Dhamira ni Kupinga Masuala ya Utekaji Nchini Tanzania.
Je video hiyo ina Ukweli kiasi gani.
Je video hiyo ina Ukweli kiasi gani.
- Tunachokijua
- Mtumiaji mmoja wa Instagram alichapisha kipande cha video kinachomuoenesha mgombea mwenza kwa nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akikeme masuala ya utekaji huku sehemu ya maneno kwenye video hiyo ikisikika ikisema "Samia Must Go'. Aidha video hiyo iliambatana na grafiki yenye ujumbe unaosomeka "NCHIMBI AMSHUKIA SAMIA KUTEKWA KWA POLEPOLE"
Uhalisia wa video hiyo
JamiiCheck imepitia kwa kina video hiyo na kubaini kuwa kilichoandikwa kwenye grafiki hiyo kinapotosha uhalisia.
Ufuatiliaji umebaini kuwa maneno yaliyotamkwa na balozi huyo kaika kipande hicho cha video ni halisi ingawa yameharirirwa na kutolewa baadhi ya maneno na hivyo kutengeneza ujumbe mpya wenye lengo la kupotosha.
Balozi Nchimbi aliyazungumza maneno hayo Septemba 13, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri kwa niaba ya chama chake akiwa kama katibu mkuu kuhusu masuala ya utekaji yaliyokuwa yakiendelea ikiwemo lile la kifo cha kikatili cha Mzee Ali Kibao. Mazungumzo hayo yalirushwa na vyanzo mbalimbali tizama hapa na hapa.
Katika mazungumzo hayo ndipo alipoitaja slogan ya wakati huo iliyokuwa imetolewa na vijana wa BAVICHA ya 'SAMIA MUST GO', ambapo Balozi Nchimbi alisema ni kitu kisichowezekana kwa kuwa Rais yupo kwa mujibu wa katiba.
Rejelea hapa kuanzia dakika ya 13:52 ambapo Balozi Nchimbi alitamka;
"Zimetoka kauli za vijana wa CHADEMA wanaitwa BAVICHA nadhani mmewasikia juzi jana na slogan mpya, kaulimbiu yao mpya inasema Samia Must Go na ukishasema hivyo wanashangilia sana. Unajua kuna vitu ukisema unavyojua kabisa havizwezekani"
Hivyo video hiyo ni halisi na haijatengenezwa wala kuharirirwa na kwa Teknolojia ya Akili Unde kama wengi walivyodhani na badala yake imekatwa baadhi ya vipande kutoka katika video halisi ya Septemba 2024, na haihusiani na tukio la kutekwa kwa Balozi Polepole (2025).