Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jun 28, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,029
  Likes Received: 37,794
  Trophy Points: 280
  Ktk maisha kuna msemo malipo ni hapa hapa duniani.Kwa maana ya uovu utakaofanya dhidi ya binadamu mwenzako malipo ni hapa hapa duniani.Nchi ambayo sina haja ya kuitaja kwa sasa inakabiliwa na mfululizo wa matukio ambayo kwa kweli hayaishi na unaweza kujiuliza mbona mambo hayo hayafikii ukomo.Kila kukicha ni matatizo ambayo kwa akili ya kawaida yangeweza kupatiwa ufumbuzi ila bila shaka kutokana na laana ambayo kwa sasa viongozi wanaitumikia bila kujijua wamejikuta wanakosa busara na maarifa ya kuyatatua na badala yake ni kama wanatia pili pili kwenye kidonda.Kinachowasumbua ni hii laana wanayoitumikia kutokana na dhuluma,uonevu,unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya watu wao wenyewe na sasa haya ni matokea ya kilio cha watu hawa ambapo mwenye mamlaka kuliko wote sasa amesika kilio chao na ameshusha laana hii inayowafanya wakose busara na sasa wanajikuta wanashindwa kuongoza na kinachofuata ni wao kuanguka ktk utawala wao.

  Ushahidi wa haya niyasemayo ni wao kukosa busara ya kuyashughulikia na badala yake wanaumbuka kila kukicha.Kwa kifupi mwenye mamlaka kuliko wote kawashushia laana na wanajikiuta wanakosa dira na mwelekeo.Hawa watu unaweza kuwafananishi na wale waliokuwa wanajenga ule mnara maarufu ktk vitabu vitakatifu unaoitwa mnara wa babeli kwa lengo la kumfikia huyu mwenye mamlaka.Aliwashushia laana wakajikuta hawaelewani ktk lugha na hivyo kusambaratika.Sasa hawa jamaa nao kaamua kuwaadhibu kwa staili ile ile ila tofauti ni kuwa kawaacha na lugha yao moja ila alichokifanya ni kuwanyima busara na hekima ya kutatua matatizo na mwisho wa siku watajikuta wanaelemewa na kuanguka.

  Maovu waliyoyafanya kwa watu wao ni mengi mno mfano kuuza maliasili za watu wao,kuwapora ardhi yao,kuwanyanyasha na mengine mengi.Matokea yake sasa ni nchi ile kujikuta ikiachwa na mashimo na uharibifu wa mazingira baada ya wao na washirika wao kupora maliasili za watu wao.

  Hatua waliofikia naifananisha na ule msemo wa kiswahili unaosema siku ya kufa nyani miti yote huteleza.Wamefikia kikomo na sasa wanatapatapa tu kama mfa maji.Laana hii ndio inawafanya watoe kauli za kuwarudi wao wenyewe na kuongeza matatizo na sio kauli tu bali hata matendo yao nayo yanawagharimu kila kukicha.

  Kila kitu kina mwanzo na mwisho.
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,029
  Likes Received: 37,794
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone nini kitajiri.
   
 3. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,295
  Likes Received: 1,215
  Trophy Points: 280
  na bado...mass resignation inakuja,stay tuned
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,029
  Likes Received: 37,794
  Trophy Points: 280
  Ok,mkuu nimekusikia.
   
 5. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  haya bwana.MUNGU TUNUSURU
   
 6. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Sorry. nilikuwa nakusaidia tu ku-edit ili usomeke.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Atunusuru sisi na siyo hawa wanyang'anyi wa haki za waTz
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena ila na sisi kama waTZ yafaa tujitambue na kujua haki zetu kama sasa huduma za afya hatupati yafaa tutumie njia thabiti ya kuingia barabarani na kuikataa serikali hii iliyoshindwa kuiongoza hii ktk nyanja zote!
   
 9. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,029
  Likes Received: 37,794
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu.Nimekusikia.
   
 10. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono mawazo yako.
   
 11. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa!
   
Loading...