Nchi zilizostaarabika, DPP angefukuzwa issue ya Lema

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,314
72,740
Kwa ile kauli ya mahakama ya rufaa juu ya sakata la kusigina sheria lililofanywa na ofisi ya DPP ni wazi ili kulinda heshima ya ofisi mkuu wake ilibidi ajiuzulu au afukuzwe.

DPP anapaswa kuonyesha kufuata sheria na sio njia chafu na zenye mateso kwa raia.

Iweje msimamizi wa sheria awe mvunja sheria?
 
Kabisa alipaswa ajiuzulu

Na ukae ukijua DPP anapata kiburi kutoka kwa AG wa Tanzania.

Na Ukumbuke hii ndio nchi pekee ambayo Mkulu / Sizonje au Faru John anaingilia hadi Mahakama na kutoa amri zake hasa ya kuwanyanyasa na kuwaonea wapinzani bila kujali vifungu vya sheria vinasemaje

Nchi hii hatujawahi kuwa na Haki na Demokrasia ya kweli kwanza hatuvijui.
 
Kama amefanyiwa hivyo Lema ambaye ni kuongozi anayefahamika na ngazi za juu jamani sipati picha mwananchi mnyonge asiyekuwa na nyuma wala mbele. Hadi machozi yananitoka maana ni wengi wamenyimwa haki yao.

Inabidi mwenye hiyo nafasi ajitathimini kama kweli hiyo nafasi inamfaa tena kuendelea kukaa. Maana sina uhakika kama raia ambaye hajui sheria na hana uwezo wa kuweka mawakili kama atapata haki chini ya mtu kama huyu. Tunachohitaji jamani kwenye hivi vyombo siyo kumpendelea mtu, haki itendeke.

Mungu tu atusaidie, maana hii hali siyo kabisa. Ila nina imani Rais wetu ni kiongozi wa wanyonge hatakubali kuona wanyonge wanaonewa na atachukua hatua stahiki juu ya DPP.
 
Ofisi hiyo ya DPP imechangia uongozi wa Rais wetu kuonekana ni ya kidikteta hata bila sababu za msingi. Na leo wale waliowadhihaki watetezi wa haki wako kimyaa kama hawapo. akina Stroke, Wakudadavua, Lizaboni, Mwasita, Jingalao etc mjue watu wote waTz wanaipenda nchi hii si mpaka unyanyasaji !!!.
 
Kama amefanyiwa hivyo Lema ambaye ni kuongozi anayefahamika na ngazi za juu jamani sipati picha mwananchi mnyonge asiyekuwa na nyuma wala mbele. Hadi machozi yananitoka maana ni wengi wamenyimwa haki yao.

Inabidi mwenye hiyo nafasi ajitathimini kama kweli hiyo nafasi inamfaa tena kuendelea kukaa. Maana sina uhakika kama raia ambaye hajui sheria na hana uwezo wa kuweka mawakili kama atapata haki chini ya mtu kama huyu. Tunachohitaji jamani kwenye hivi vyombo siyo kumpendelea mtu, haki itendeke.

Mungu tu atusaidie, maana hii hali siyo kabisa. Ila nina imani Rais wetu ni kiongozi wa wanyonge hatakubali kuona wanyonge wanaonewa na atachukua hatua stahiki juu ya DPP.
Hatuwezi kupiga kura ya kutokuwa na imani na ofisi ya DPP?
 
Hata nchi zilizostaarabika kusingekuwa na vichaa kama lema kuwa viongozi..wala rais kutabiriwa vifo..
 
Kwa ile kauli ya mahakama ya rufaa juu ya sakata la kusigina sheria lililofanywa na ofisi ya DPP ni wazi ili kulinda heshima ya ofisi mkuu wake ilibidi ajiuzulu au afukuzwe.
DPP anapaswa kuonyesha kufuata sheria na sio njia chafu na zenye mateso kwa raia.
Iweje msimamizi wa sheria awe mvunja sheria?
Kungekuwa na Tanganyika Law Society inayojitambua ndio masuala yake haya kuyashughulikia! La hapa limelala eti mtu anataka kugombea tena
 
Back
Top Bottom