Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,239
Sina hakika kama Waafrica ni jamii halisi ya binadamu walioumbwa na Mungu yule aliyeumba jamii nyingine , hii ni kwa sababu hawajawahi kuwa na sifa za ubinadamu .
Nchini Tanzania , nchi ambayo ni mwenyeji wa mkutano wa SADC (kundi la nchi zisizo na tija yoyote) , mwaka huu kunafanyika Uchaguzi wa Serikali za mitaa , ikiwa imesalia miezi miwili tu kufanyika kwa uchaguzi huo vyama vya upinzani vimedhibitiwa na kutoruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa huku chama cha mapinduzi kikitamba na kufanya kitakavyo nchi nzima , kinyume cha Katiba ya Nchi , na kinyume kabisa cha makubaliano yaliyomo kwenye mikataba ya kimataifa .
Hoja yangu ni kuwashangaa viongozi wa SADC ambao hakuna wasichokifahamu kuhusiana na kuuawa kwa Demokrasia nchini Tanzania , kunyamaza kwao kunamaanisha kwamba hawana habari na ustawi wa Demokrasia kwenye nchi zao , ni viongozi madikteta wanaoshindwa kuhoji udikteta unaofanywa katika Tanzania , wamesahau kwamba Hakuna maendeleo pasipo na demokrasia , wamejisahau wakaamua kulewa madaraka .
Kwa hali hii Hivi kuna mtu anayeweza kuwaamini viongozi wa kiafrica , kama wamekalia kimya ukandamizaji , kutekwa , kukamatwa hovyo na mauaji ya viongozi wa Upinzani yanayofanywa nchini Tanzania ni wapi pengine wanaweza kuhoji ?