Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Ameyasema hayo wakati anafungua Mkutano wa Utatu wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama jijini Antananarivo, Madagascar Agosti 15, 2025.
"Licha ya changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi wanachama na ulimwengu kwa ujumla, eneo letu limebaki kuwa himilivu, likiendelea kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kuyafikia malengo ya kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya watu wetu", Balozi Shelukindo alisema.
Alisema ili lengo hilo liweze kutimia, alihimiza nchi wanachama kulipa kipaumbele kwa kujijengea uwezo katika kuhamasisha jitihada za kuzuia migogoro, usuluhishi wa migogoro, kujenga na kulinda amani.
Allhitimisha hotuba yake kwa kuzitakia kheri nchi wanachama zinazojiandaa na uchaguzi mkuu ambazo ni Malawi, Ushelisheli na nchi yake Tanzania. Alisema Tanzania inasubiri kwa hamu kubwa kupokea timu ya waangalizi ya SADC ambapo maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 yanaendelea.