Investigation Unit
JF-Expert Member
- Nov 26, 2023
- 357
- 399
Rais Samia atumia TZS120.56 kujenga Meli ya MV Mwanza itakayobeba Tani 400, magari 20 na Malori 3 pamoja na abiria 1,200 kwa wakati mmoja.
Kwa msiofahamu, MV Mwanza ni mradi wa kimkakati wa kitaifa unaoonyesha dhamira ya Rais Samia katika kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa majini, kuongeza usalama, kupanua uchumi wa Ziwa Victoria, na kujenga uwezo wa Uchumi Kitaifa. Gharama ya mradi huu ni TZS120.56bn, Mradi huu ni uwekezaji mkubwa na wenye tija kwa taifa na kipato cha mtu mmoja mmoja kwa sasa na baadae.
TZS120.56bn ni thamani ya meli ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu”, inayojengwa kwa gharama ya serikali chini ya Rais Samia. MV Mwanza ni meli kubwa zaidi mashariki mwa Afrika, ikijengwa Mwanza, Tanzania. Meli hii ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 kwa Pamoja, Mizigo tani 400, Magari madogo 20 na malori makubwa matatu (3), Meli hii inaurefu wa takribani 92.6 m, upana 17 m, na urefu wa kulia 20m,