Nchi za Afrika tutafute aina yetu ya demokrasia

Nchi za Afrika tutafute aina yetu ya demokrasia

Ni wakati sasa nchi za Africa kutafuta mfumo thabiti wa kiutawala utakaozinasua nchi nyingi za kiafrika kutoka kwenye machafuko yanayoletwa na hii dhana ya democracy ambayo barani Africa bado haijaelewaka sawa sawa na kujikuta kila siku ni mapigano tu na sababu ikiwa eti demokrasia haijafuatwa.

Lakin pia hata kwenye nchi kama Tanzania ambako inasemekana demokrasia inafuatwa bado kuna changamoto nyingi ikiwemo kutokuwa na uelekeo mmoja kama taifa hasa pale kiongoz anapokuwa na jitihada za kuikwamua nchi kutoka kwenye hali duni iliyokuwepo na kuipeleka mbele kimaendeleo. Hapo wataibuka wanaojiita wakosoaji kwa mwavuli wa demokrasia ili kuwaaminisha wananchi tofauti na uelekeo wa Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Sasa kwa kuwa demokrasia hii tuliikopi kwa wazungu na tusijue kwamba hao wazungu kabla ya hiyo demokrasia wame ishi miaka mingi sana na mifumo mingine ya kiutawala hasa mifumo ya kifalme na umalkia, kupitia mifumo hiyo nchi zao zilifikia hatua fulani ya kimaendeleo ndipo wakaileta demokrasia lakin hata hiyo demokrasia inavyotekelezwa na wao ni tofauti sana na huku afrika na zaidi inaleta machafuko na kudumaza maendeleo yetu wana wa afrika.

Kama hiyo haitoshi hizo hizo nchi za wazungu tulikochukua huu mfumo wa demokrasia wamekuwa wakija kutuingilia katika kufanya maamuz kwenye tawala zetu na ikionekana wanapata ugumu watatumia vikundi vya watu vitakavyopinga Serikali kwa makusud na Serikali ikivichulia hatua kali basi wazungu wanaweza kuja wenyewe na kuitoa Serikali madarakani (rejea libya kutolewa kwa ghadafi) kwa kisingizio kuwa demokrasia haifuatwi katika nchi husika, lakini hapo kikubwa ni wao waendelee kupata kile wanachokitaka kiulaini.

Kutokana na hayo pendekezo langu ni kwamba Afrika itafute mfumo wa kiutawala utakaoendana na tamaduni zetu za afrika na utakaotufanya tujinasue kutoka kwenye huu mnaso wa kimaendeleo angalau na sisi siku moja tufikie japo robo kama sio nusu ya yale maendeleo ya huko ughaibuni. Huo mfumo tunaweza hata tukauita DEMOAFRICA, AFRODEMOCRACY, au jina lolote ambalo litafaa lengo likiwa ni kutufanya tuwe na sauti moja kuyafikia maendeleo yanayotakiwa.
===================
........... Wako katika kazi............. ==================

Kalenga kidamali
Mfumo Mzuri wa KIDEMOKRASIA Ni kila mtu kuishi Maisha yake anavyoona inafaa, huku Kiongozi mkuu akibaki kuwa baba! Tusiwe na Police (Hii Ni Colonial n imported from outside), JWTZ ifutwe tubaki na Morani (Historia yake hili liliundwa na Wakoloni), Elimu tuitupe hukoooooo(Haya yote ya Wazungu), Tusiwe na Serikali (tubaki na Serikali ya familia tu, hizi nyingine tumekopi kwa hao Wazungu na Waarabu), Makanisa na Misikiti tuvichome Moto (vyote hivi asili yake sii Afrika)! Nadhani mfumo uliokuwepo Stone Ages ndio mzuri kuliko Sasa! Tuachane na Serikali hizi, tubaki kifamilia TU itatosha! Hizi Serikali zinakusanya Kodi, Ni gharama Sana kuziendesha, halafu tunawapa Washamba na Malimbukeni (kwa Mujibu wa Zitto) kuongoza Nchi!

Naamini huu mfumo utakuwa mzuri!
 
Kama nia yenu ni kutawala tuu bila kutegemea kuhojiwa kama mnatawala misukule vile, then hilo halikubaliki katu.

Hayo ndo baadaye mnaturejesha kwenye zile zama za u-chief ambapo chief aliweza kumnyang'anya mtu mkewe kisa kampenda na wala asifurukute.!

Tuko kwenye "Global Village" ambapo mataifa yaliyoendelea ndio tunawatumia kama dira ya kutuongoza kwa mambo mengi sana kiasi kwamba ndoto kama hizo za kutaka kutuletea udikteta kwa kisingizio cha maendeleo haikubaliki kabisa.

Uongozi lazima ubaki dhamana na lazima ieleweke kuwa kila moja anakosea (Infallibility of Human Being) na kwa msingi huo sharti ukubali kukosolewa na mwisho tukubali matakwa ya watu.

We must have the lawful and unequivocal mandate to govern and not the dubious one obtained through manipulation of vote and the intimidation of the electorate. In light of the above, the author needs to go back to the drawing board to learn the basics of democracy in regard to its elements.
 
kwa kutumia mfano wa gadafi, afrika imeanza demokrasia yake waangalie kina mseveni,kagame na uwasikilize akina nkamia hiyo ndiyo demokrasia ya afrika lkn kumbuka kabla ya kuja wazungu afrika ilikuwa inafuata aina hii hii ya utawala na mtwala alikuwa hahojiwi au kuulizwa chochote na watawaliwa maendeleo tuliyokuwa nayo unayajua.

Kutohojiwa kwa kiongozi hakuleti umaskini. Mbona Gaddafi alikuwa hahojiwi lakin walikuwa juu kimaendeleo? Unataka kusema wazungu wameendelea kwa sababu wana viongozi wanaohojika?

Afrika ukipata viongozi wenye uwezo, maono na waadilifu na wenye kujiamini tutatoka tu. Haijalishi kama marais wetu watakaa madarakani miaka 20 au 5 mpaka uchaguzi mwingine. Cha muhimu ni hayo mambo hapo juu

Nguvu na kiasi cha pesa kotumikacho kwenye michakato ya kufanya chaguzi ni sumu ingine kwenye maendeleo ya afrika
 
Labda tuite jina lingine...democracy has one meaning...freedom of economically,politically and culturally for all citizens....
 
Back
Top Bottom