kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 753
Ni wakati sasa nchi za Africa kutafuta mfumo thabiti wa kiutawala utakaozinasua nchi nyingi za kiafrika kutoka kwenye machafuko yanayoletwa na hii dhana ya democracy ambayo barani Africa bado haijaelewaka sawa sawa na kujikuta kila siku ni mapigano tu na sababu ikiwa eti demokrasia haijafuatwa.
Lakin pia hata kwenye nchi kama Tanzania ambako inasemekana demokrasia inafuatwa bado kuna changamoto nyingi ikiwemo kutokuwa na uelekeo mmoja kama taifa hasa pale kiongoz anapokuwa na jitihada za kuikwamua nchi kutoka kwenye hali duni iliyokuwepo na kuipeleka mbele kimaendeleo. Hapo wataibuka wanaojiita wakosoaji kwa mwavuli wa demokrasia ili kuwaaminisha wananchi tofauti na uelekeo wa Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Sasa kwa kuwa demokrasia hii tuliikopi kwa wazungu na tusijue kwamba hao wazungu kabla ya hiyo demokrasia wame ishi miaka mingi sana na mifumo mingine ya kiutawala hasa mifumo ya kifalme na umalkia, kupitia mifumo hiyo nchi zao zilifikia hatua fulani ya kimaendeleo ndipo wakaileta demokrasia lakin hata hiyo demokrasia inavyotekelezwa na wao ni tofauti sana na huku afrika na zaidi inaleta machafuko na kudumaza maendeleo yetu wana wa afrika.
Kama hiyo haitoshi hizo hizo nchi za wazungu tulikochukua huu mfumo wa demokrasia wamekuwa wakija kutuingilia katika kufanya maamuz kwenye tawala zetu na ikionekana wanapata ugumu watatumia vikundi vya watu vitakavyopinga Serikali kwa makusud na Serikali ikivichulia hatua kali basi wazungu wanaweza kuja wenyewe na kuitoa Serikali madarakani (rejea libya kutolewa kwa ghadafi) kwa kisingizio kuwa demokrasia haifuatwi katika nchi husika, lakini hapo kikubwa ni wao waendelee kupata kile wanachokitaka kiulaini.
Kutokana na hayo pendekezo langu ni kwamba Afrika itafute mfumo wa kiutawala utakaoendana na tamaduni zetu za afrika na utakaotufanya tujinasue kutoka kwenye huu mnaso wa kimaendeleo angalau na sisi siku moja tufikie japo robo kama sio nusu ya yale maendeleo ya huko ughaibuni. Huo mfumo tunaweza hata tukauita DEMOAFRICA, AFRODEMOCRACY, au jina lolote ambalo litafaa lengo likiwa ni kutufanya tuwe na sauti moja kuyafikia maendeleo yanayotakiwa.
===================
........... Wako katika kazi............. ==================
Kalenga kidamali