Nchi yetu wote, acheni kutuamulia isivyostahili

Nchi yetu wote, acheni kutuamulia isivyostahili

12STONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
1,190
Reaction score
409
Maamuzi yaliyofanywa ya KUUZA BANDARI YETU YA DARESALAAMU kwa siku na miaka isiyokuwa na ukomo (vizazi na vizazi/milele na milele),Yanaondoa uvumilivu,yanaleta jazba na Hali ya kutowaamini kabisa Viongozi wenye Kufanya maamuzi hayo.

Mnauza Bandari/LANGO KUU LA NCHI {TANZANIA} Kwa makusudi,Kisha mnajipanga kuwaweka sawa Wabunge watetee uovu huu Kana kwamba Ni jambo Njema Saana.

Inakera Sana, inasikitisha,inaumiza kuona watu wenye dhamana ya KUILINDA NCHI NA RASILIMALI ZAKE ili zizidi kutunufaisha SISI na Vizazi vyote vya Vitukuu wetu.Ni aibu kuona Mambo Kama yasiyo na hata chembe ya UZALENDO hata kidogo na aliyehusika moja kwa moja Ni Kiongozi wenye ngazi ya juu kabisa (RAIS NA TIMU YAKO YA KARIBU),Hii Ni aibu kubwa ya Milenium (miaka 1000).

RAIS na watu wake tuseme Nini Sasa?
Hakuna mtu mwenye Hekima au mliziba masikio mistake kusikia? Mmejipanga watoto wetu wawe watumwa wa WAARABU Tena,Je! Watoto WENU watahamia UARABUNI?
Kama sivyo, Usalama wa watoto wetu na WENU pia uko wapi kwa mazingira haya ya KUUZA BANDARI?

Kuwa kwenye nafasi yoyote ile ya Uongozi Haina maana hao tunaowaongoza hawajui chochote au lolote.Uongozi Ni Dhamana tu,Inapaswa itumie ipasavyo na kwa halali Tena kwa manufaa ya Wananchi na sio kujinufaisha watu wachache.

Itapendeza Sana Maonii ya Wananchi yasipuuzwe kwa namna yeyote ile.Hakuna haha ya kutumia NGUVU kubwa ya ushawishi wa Wabunge, Vyombo vya HABARI na Baadhi ya Viongozi wa Serikali kuendelea kulisemea suala Hilo OVU Kama vile Ni takatifu kweli kweli.

NASHAURI MKATABA HUU UTUPILIWE MBALI ILI WATANZANIA TUBAKIE KUWA WAMOJA NA WENYE AMANI.NJE NA PALE Endapo mtang'ang'ania na kulazimishia BANDARI IENDE KWA WAARABU,Sishangai kuona itakuwa rahisi Sana Wananchi Kushawishiwa na kushawishika KUANDAMANA NCHI NZIMA MOAKA IKULU.

Kama Hamtawalimda wao na RASILIMALI za nchi,Watatafuta namna ya wao kuwa salama na RASILIMALI zao.

Ni wakati wa kuwa Malini kwa Viongozi kuliko wakati wowote ili TAIFA LISIIINGIE KWENYE MACHAFUKO YASIYO YA LAZIMA.

HEKIMA NA BUSARA ZITUMIKE.
 
WaTz washamba tu, mnakesha kwenye mitandao kulia lia hamtak mali zenu ziuzwe... Kama mpo serious ingieni barabarani waarabu tuwavunje viuno mpate Bedrest hadi kifo
 
Nchi hii sasa inahitaji "neutral factor" nje ya Ukatoliki na Uislamu. Kwa nyakati na vipindi tofauti imani za kidini kwa njia ya hila ilikabidhi mtu atokanaye na mamlaka hizi kuwa ndiye pekee wenye kuweza kuongoza taasisi nyeti ya urais kwa kupokezana kijiti.

Ni lazima kama taifa tutafute ladha nyingine nje ya mtego huu. Tulimkosa Lowasa kwa ajili ya "commitment" hii ya kipuuzi. Ifike wakati mtu mwenye kustahili kuwa kiongozi wa nchi yetu awe hata nje ya wigo na nira mbaya ambazo zimewekwa kwa ghiliba.
 
Wenye maslahi pale bandarini wenye kufaidika na huu uzembe wa miaka yote hawawezi kukubali kuachia maslahi yao yaondolewe na ufanisi utakaokuja na DPW.

Watagawa sana pesa kwa watu wa kila sekta, kila taasisi ilimradi tu ujinga wa pale port uweze kulindwa na nchi iendelee kudumaa kwa faida yao wachache tu. Lakini no way, hawa tutapambana nao mpaka mwisho liwalo na liwe.
 
Nchi hii sasa inahitaji "neutral factor" nje ya Ukatoliki na Uislamu. Kwa nyakati na vipindi tofauti imani za kidini kwa njia ya hila ilikabidhi mtu atokanaye na mamlaka hizi kuwa ndiye pekee wenye kuweza kuongoza taasisi nyeti ya urais kwa kupokezana kijiti.

Ni lazima kama taifa tutafute ladha nyingine nje ya mtego huu. Tulimkosa Lowasa kwa ajili ya "commitment" hii ya kipuuzi. Ifike wakati mtu mwenye kustahili kuwa kiongozi wa nchi yetu awe hata nje ya wigo na nira mbaya ambazo zimewekwa kwa ghiliba.
Cha muhimu ni ufanisi wake hayo masuala ya dini ni tafsiri potofu za binafsi za mitandaoni.

Kama ni mwaminifu anakuwa mwaminifu kama ni mpigaji ni mpigaji tu.
 
Kanisa Moja Takatifu la Mitume
Nadhani mambo kama hayo ingefaa watanzania wote wangeshirikishwa kwenye kutoa maamuzi na sio kikundi Cha watu wachache, la sivyo watanzania hawatakubali kunyanganywa Mali zao na kupewa waarabu. Hili ni jambo la aibu na linapaswa kukemewa kwani tukiyaruhusu haya yaendelee ni wazi kwamba tunarudi kwenye utumwa tuliko toka
 
Kuna kiongozi huko Zanzibar kama sijakosea anaitwa Jussa! Huyu kiongozi mkubwa pale ACT Zanzibar

Juzi juzi alikuwa akiwahutubia wanachama wa chama Chake, aliongea mengi, lakini Mimi nilichodaka ni hiki, na ambacho baada ya kukaa na kutafakari sana,

Nimepata maswali mengi sana!

Aliuliza, Zanziba tulikuwa na Jeshi, leo tunajeshi? Wananchi kwamsisitizo, Hakunaaaa

Tunapolice, HatunaaaAA

JE, tuna katiba, Hatunaaaaaaazzz
JE, tunabendera,,,Hatunaaaazzz

Akasema, sababu ni nani?? Wananchi, Tanganyikaaaaaaazzzz

Tumeonewa sana sisi, tumedhulumiwa sana sisi,

Sasa, hawa wa Tanganyika, kuna jambo limewapisha kelele saana, tena jambo lenyewe ni doooogo, ukilinganisha na walichotutenda sisi, unajiuliza, kumbe mkuki kwa Nguruwe!

Wanamsema Raisi Samia kwa kitu kidoogo sana, Je wao wangekuwa wazanzibari wangehimili huu uonevu tulionao sisi? Kama muungano umewachosha, semeni tugawane mbao, sisi tuko tayari!

Maswali!

Inamaana huyo Jussa na Rais wetu, Lao ni moja?

Nasema hivyo kutumia kile amekisema Jussa, kwamba, wao kutendewa kitu kidogo tu, makelele meeengi!!

Kutendewa kwetu huko anakokusema Huyu Jussa, ilikuwa ni lazima tutendewe vile ili kuonwa uvumilivu wetu ama?
 
Kwa kuwa awamu hii ni vilaza hawawezi kuendesha bandari basi wanadhani na viongozi watakaokuja baada ya miaka 30 nao watakuwa vilaza ndiyo maana wanasaini mkataba wa milele!


Mkataba ungekuwa unasema hivyo kama anavyosema waziri mkuu Kassim Majaliwa tusingelalamika.

Sasa hivi ufafanuzi unatolewa mwingine na mkataba unasema mengine, sisi watanzania hatutasikiliza chochote ambacho hakipo kwenye mkataba ,yatakuwa ni matumizi mabaya ya masikio yetu.
Hata chifu Mangungo wa Msovera alipewa maelezo mazuri sana

Kuna gunduzi nyingi sasa hivi kama magari ya kutumia umeme, gesi na mwarabu anategemea mafuta kwa hiyo walishaona mbali sana ndiyo maana ya mikataba ya milele.

Next generation biashara ya mafuta inaweza kuja kuwa ya kawaida sana lzm waandae pa kukimbilia
Naungana nawe kwamba ni matumizi mabaya ya masikio yetu, tukiwasikiliza hawa waunga mkono mkataba.
 
Back
Top Bottom