Nchi yetu ni tajiri, ni Donor Country, tunajenga kwa Pesa yetu

Hayati Rais Magufuli, yawezekana ndiye alikuwa mtu jasiri kuliko mwanadamu yeyote nchini Tanzania.

Kusema kitu ambacho hakipo, huku ukijua kuwa ukweli utakuja kujulikana lakini ukang'angania kuulinda uwongo, kunahitajika ujasiri wa pekee ambao mtu mwenye mwenye hekima, hata ile ya kawaida kabisa, hawezi. Marehemu aliweza.

Tuliaminishwa kuwa nchi yetu ni tajiri sana, ila watu walikuwa wanaiba hela, na kwamba wajati wa uongozi wake wizi ulikuwa umedhibitiwa, ndiyo maana ananunua ndege kwa cash kutokana na makusanyo yetu maxuri ya kodi, tunajenga reli ya kisasa kwa pesa yetu, tunajenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme kwa pesa yetu, tunajenga daraja la Busisi kwa pesa yetu.

Watanzania ambao hawana uwezo wa kuona mambo hata kwa umbali wa mita mbili, ikawa ni vigelegele kila kona, na kunena kuwa, huyu ndiye tuliyeletewa na Muumba wetu ili atutoe kutoka kwenye lindi la umaskini na kutupeleka kwenye utajiri wa kutukuka.

Tena marehemu akatuaminisha kwamba sisi siyo wa kupewa misaada bali wa kutoa misaada. Yaani sisi ni donor country.

Baada ya huyu mwenzetu kututoka, kwanza ikatoka kauli ya Rais Mh. Samia kuwa sasa hivi anafanya kazi ya kuifungua nchi. Sote tukashangaa, nani aliifungia nchi yetu? Mbona hatukuambiwa?

Mara Rais Samia akasema kuwa, mambo ya katiba mpya, yasimame, kwanza tufufue uchumi. Duh, nani alikuwa ameua uchumi wetu? Yaani nchi inayotekeleza miradi mikubwa kwa cash na kwa pesa yake yenyewe, nchi inayotaka kuanza kutoa misaada kwa mataifa mengine, halafu uchumi wake uwe mfu??

Hatujakaa sawa, Rais akatuambia kuwa ukuaji wetu wa uchumi umedondoka toka 7% mwaka 2015 mpaka 4%. World bank wakasema umedondoka mpaka 1.9%!! Maajabu makubwa!

Sahizi tunaambiwa kuwa awamu ya Hayati Magufuli ndiyo iliyoliletea Taifa deni kubwa kwa muda mfupi kuliko awamu yoyote, tena hela ikikopwa na kutumika kama hela ya familia. Mh. Nape katoa kauli yake Bungeni kuwa utawala wa marehemu ulikopa zaidi ya trillion 20 bila uwazi, na ameomba uchunguzi ufanyike ili ijulikane hiyo pesa ilofanya kazi gani.

TUJIULIZE:

1) Kwanini marehemu aliamua kuwadanganya Watanzania kuwa tunajenga miradi yetu kutokana na makusanyo mazuri ya kodi, wakati haikuwa kweli?

2) Kwanini atudanganye kuwa nchi yetu ilikuwa tajiri wakati nchi ilikuwa inachechemea, na kuishi kwa kukopakopa?

3) Kwanini atudanganye kuwa tutembee vifua mbele kwa sababu ukuaji wa uchumi ulikiwa unapaa, kumbe ulikuwa unashuka?

4) Kwanini atudanganye kuwa kipindi chake pato la mtu mmoja mmoja lilipanda sana mpaka kutupeleka kwenye uchumi wa kati, ilihali yeye katika uongozi wake, wastani wa pato la mwananchi liliongezeka kwa dola 80 tu, wakati watangulizi wake waliongeza kwa zaidi ya dola 280 katika kipindi cha miaka 10?

Kwa kweli tulidanganywa sana, tulihadaiwa sana, tulifanywa mambumbumbu sana. Hayo yamepita. Ni shule tosha. Tujiulize, kutokana na utawala wa awamu ya 5 kuwa utawala wa ghiliba, tumejigunza nini? Tumeweka mfumo upi utakaozuia kiongozi kuwadanganya wananchi?
Uwongo huo ndio unapendwa sana na CCM watawala.
 
Hii nchi ni tajiri ina kila kitu kuanzia madini...rasilmali..utalii...maji ya kutosha...ardhi yenye rutuba...nk lakini watu wake ni maskini au fukara...ukielewa hii utaona ulichoandika hapo juu ni utumbo na JPM alikuwa sahihi.ukitambua fahari ya nchi yako ndo unaweza kujua kinachosababisha ufukara katika dimbwi la utajiri...1.elimu na ufahamu wa watu upo chini..elimu bure+mikopo ya elimu ya juu 2.Rushwa na ubadhirifu...kesi za uhujumu uchumi na Takukuru 3.biashara isiyo rasmi...ruksa kufanya biashara popote mpaka serikali itakapoainisha maeneo ya kufanyia biashara..4.Serikali kupitia watumishi kushindwa kutatua matatizo ya watu...kuondoa watumishi wenye vyeti feki au kughushi vyeti..etc etc etc
 
Back
Top Bottom