Nchi yetu ni tajiri, ni Donor Country, tunajenga kwa Pesa yetu

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Hayati Rais Magufuli, yawezekana ndiye alikuwa mtu jasiri kuliko mwanadamu yeyote nchini Tanzania.

Kusema kitu ambacho hakipo, huku ukijua kuwa ukweli utakuja kujulikana lakini ukang'angania kuulinda uwongo, kunahitajika ujasiri wa pekee ambao mtu mwenye mwenye hekima, hata ile ya kawaida kabisa, hawezi. Marehemu aliweza.

Tuliaminishwa kuwa nchi yetu ni tajiri sana, ila watu walikuwa wanaiba hela, na kwamba wajati wa uongozi wake wizi ulikuwa umedhibitiwa, ndiyo maana ananunua ndege kwa cash kutokana na makusanyo yetu maxuri ya kodi, tunajenga reli ya kisasa kwa pesa yetu, tunajenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme kwa pesa yetu, tunajenga daraja la Busisi kwa pesa yetu.

Watanzania ambao hawana uwezo wa kuona mambo hata kwa umbali wa mita mbili, ikawa ni vigelegele kila kona, na kunena kuwa, huyu ndiye tuliyeletewa na Muumba wetu ili atutoe kutoka kwenye lindi la umaskini na kutupeleka kwenye utajiri wa kutukuka.

Tena marehemu akatuaminisha kwamba sisi siyo wa kupewa misaada bali wa kutoa misaada. Yaani sisi ni donor country.

Baada ya huyu mwenzetu kututoka, kwanza ikatoka kauli ya Rais Mh. Samia kuwa sasa hivi anafanya kazi ya kuifungua nchi. Sote tukashangaa, nani aliifungia nchi yetu? Mbona hatukuambiwa?

Mara Rais Samia akasema kuwa, mambo ya katiba mpya, yasimame, kwanza tufufue uchumi. Duh, nani alikuwa ameua uchumi wetu? Yaani nchi inayotekeleza miradi mikubwa kwa cash na kwa pesa yake yenyewe, nchi inayotaka kuanza kutoa misaada kwa mataifa mengine, halafu uchumi wake uwe mfu??

Hatujakaa sawa, Rais akatuambia kuwa ukuaji wetu wa uchumi umedondoka toka 7% mwaka 2015 mpaka 4%. World bank wakasema umedondoka mpaka 1.9%!! Maajabu makubwa!

Sahizi tunaambiwa kuwa awamu ya Hayati Magufuli ndiyo iliyoliletea Taifa deni kubwa kwa muda mfupi kuliko awamu yoyote, tena hela ikikopwa na kutumika kama hela ya familia. Mh. Nape katoa kauli yake Bungeni kuwa utawala wa marehemu ulikopa zaidi ya trillion 20 bila uwazi, na ameomba uchunguzi ufanyike ili ijulikane hiyo pesa ilofanya kazi gani.

TUJIULIZE:

1) Kwanini marehemu aliamua kuwadanganya Watanzania kuwa tunajenga miradi yetu kutokana na makusanyo mazuri ya kodi, wakati haikuwa kweli?

2) Kwanini atudanganye kuwa nchi yetu ilikuwa tajiri wakati nchi ilikuwa inachechemea, na kuishi kwa kukopakopa?

3) Kwanini atudanganye kuwa tutembee vifua mbele kwa sababu ukuaji wa uchumi ulikiwa unapaa, kumbe ulikuwa unashuka?

4) Kwanini atudanganye kuwa kipindi chake pato la mtu mmoja mmoja lilipanda sana mpaka kutupeleka kwenye uchumi wa kati, ilihali yeye katika uongozi wake, wastani wa pato la mwananchi liliongezeka kwa dola 80 tu, wakati watangulizi wake waliongeza kwa zaidi ya dola 280 katika kipindi cha miaka 10?

Kwa kweli tulidanganywa sana, tulihadaiwa sana, tulifanywa mambumbumbu sana. Hayo yamepita. Ni shule tosha. Tujiulize, kutokana na utawala wa awamu ya 5 kuwa utawala wa ghiliba, tumejigunza nini? Tumeweka mfumo upi utakaozuia kiongozi kuwadanganya wananchi?
 
Tatizo la Ufipa mmejazana HGL na HGK watupu.

Kama unakopa hela ya nje nenda wewe benki kakope bila dhamana!
 
Alieweka Tanzania kwenye uchumi wa kati alikuwa nani? World Bank au BOT? dhana ya sisi ni donor country ilitoiana na kama taufa tuna Rasimali nyingi ambazo zinaweza kulifanya taifa letu liwe donor country issue ni kuzisimamia tu na kutokubali kunyonywa.
 
Kura za maoni kwa watia nia ilikuwa live kila jimbo.Wajumbe kila kona furaha
Kujadili wa mpeperusha Bendera chini yake live ilikuwa giza.
Magu nitamkumbuka kwa mengi
 
Utawekaje mfumo wakati walioshikilia nchi wanaamini katika uongo?
 
Alieweka Tanzania kwenye uchumi wa kati alikuwa nani? World Bank au BOT? dhana ya sisi ni donor country ilitoiana na kama taufa tuna Rasimali nyingi ambazo zinaweza kulifanya taifa letu liwe donor country issue ni kuzisimamia tu na kutokubali kunyonywa.
Magufuri
 
Ujinga wa Jiwe kwa wafuasi wake bana.JK aliacha GNI Ni $980,jiwe kwa miaka 5 na mbwembwe zake kaongeza $120 tu ikafikia GNI $1100 ndio tukaingia uchumi wa Kati.

JK kaitoa nchi kutoka GNI ya $486 mpk kaifikisha kwny $980,na ajira kamwaga Kama zote na ufisadi wa kutosha,yaani JK kwny utawala wake aliongeza GNI kwa $494.

Jiwe na kujifanya mzalendo,kuteka,kunyanganya watu pesa zao lkn hata nusu ya JK hajafikia kwny awamu yake.
 
Alieweka Tanzania kwenye uchumi wa kati alikuwa nani? World Bank au BOT? dhana ya sisi ni donor country ilitoiana na kama taufa tuna Rasimali nyingi ambazo zinaweza kulifanya taifa letu liwe donor country issue ni kuzisimamia tu na kutokubali kunyonywa.
Eti aliyeweka Tanzania kwenye uchumi wa kati! ila wewe,punguza basi kamba.Anyway,hizo zilikuwa wenge tu za yule muhuni hakuna cha uchumi wa kati wala wa nyuma, tulikuwa tu tunapiga hatua kadhaa mbele na kurudi nyuma kwa kasi.Ngoja nkwambie kitu home boy,kama unatumia reference ya ripoti ya WB nadhani utapotea ndugu,ukweli ni kwamba wale watu mkikaa meza moja wanaweza kuwekea mambo sawa na wakakupumbaza pia.Rejea kipindi cha Kikwete kipindi mahusiano yake na Wamarekani yalipokuwa mazuri walivyokuwa wakimuwekea vizuri figures za uchumi.

Ni kweli taifa letu lina rasilimali nyingi mojawapo ni watu,sasa kama watu wenyewe ndio wa aina hii wanaoamini kwamba tulikuwa uchumi wa kati then,baada ya mchumi mwenyewe kufa ukaporomoka in just a second,kweli tutafika kama rasilimali watu iko hivi?
 
Ndio mjifunze, mwehu akiwa msafi mnaweza kumpa cheo chochote kile nchini

Huo usafi mbona hakuwa nao ni basi tu Watanzania ni mazuzu. Angekuwa msafi angegawa nyumba zetu kwa mahawara zake kama njugu? Na kile chuma chakavu cha matilioni alichokihamishia jeshini kutuziba midomo? The list is endless hakuwahi kuwa msafi yule mkuu huwezi kuwa dictator halafu bado ukawa msafi never.
 
Eti aliyeweka Tanzania kwenye uchumi wa kati! ila wewe,punguza basi kamba.Anyway,hizo zilikuwa wenge tu za yule muhuni hakuna cha uchumi wa kati wala wa nyuma, tulikuwa tu tunapiga hatua kadhaa mbele na kurudi nyuma kwa kasi.Ngoja nkwambie kitu home boy,kama unatumia reference ya ripoti ya WB nadhani utapotea ndugu,ukweli ni kwamba wale watu mkikaa meza moja wanaweza kuwekea mambo sawa na wakakupumbaza pia.Rejea kipindi cha Kikwete kipindi mahusiano yake na Wamarekani yalipokuwa mazuri walivyokuwa wakimuwekea vizuri figures za uchumi.

Ni kweli taifa letu lina rasilimali nyingi mojawapo ni watu,sasa kama watu wenyewe ndio wa aina hii wanaoamini kwamba tulikuwa uchumi wa kati then,baada ya mchumi mwenyewe kufa ukaporomoka in just a second,kweli tutafika kama rasilimali watu iko hivi?
Hujanielewa! Vigezo vya uchumi wa kati viko kwa mujibu wa Worldk Bank nawao ndo wanaweka nchi katika wigo kadri wanavyoona inafaa kulingana na hesabu zao sio Magufuli hivo issue ya uchumi wa kati walaumu World Bank sio Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom