Elections 2010 Nchi yetu na Ulinzi wa Majini

H6MohdH6

Member
Oct 8, 2010
43
3
Jamani, hivi mnaona kwamba tangu Shehe Yahya amwahidi Bw Kikwete ulinzi wa majini, yaani mashetani, JK hajaanguka tena? Hii inaonyesha kuwa JK alilikubali pendekezo la Shehe Yahya na amelipokea kwa mikono miwili kwani hata alipotakiwa kulikataa pendekezo hilo la Shehe Yahya hakusema halitaki.

Shetani anapokupa kitu hakupi bure, lazima anadai malipo, na kawaida ni roho yako. Kwa hiyo shetani anapomfadhili mkuu wa nchi malipo yake ni roho ya nchi nzima. Yaani sote tutakuwa ni watumwa wa shetani.

Cha ajabu ni kwamba, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, uchaguzi mwaka huu unafanyika tarehe 31 Octoba ambayo ndiyo siku ya Mashetani duniani (Halloween day).
Siku hiyo Ibilisi atakuwa anasubiri kupewa zawadi ya nchi nzima. Je apewe asipewe?
 
Ndiyo maana tangu mwaka 2005 vifo vya maalibino ni vingi, na wahusika hawachukuliwi hatua, wengine wanapewa hadhi ya kugombea ubunge huko Kigoma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom