mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa Tanganyika,
maana ya neno Tanganyika, siijui,
Tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui?
kama ni usawa kwenye revenue kwa kweli wasahau watapata kwa proportionality tu not otherwise hakuna haja ya kufavourana hapa so what? Usawa wa kisiasa huo wanao tena nadhani unaona wanvyotamba huku tanganyika
mimi sio mtanganyika,
sikuzaliwa tanganyika,
maana ya neno tanganyika, siijui,
tanganyikailitoka wapi, sijui,
ilibatizwa jina na nani, sijui
nilizaliwa tanzania,
nilizaliwa afrika
nilizaliwa duniani
nlizaliwa na mwanadamu
kwa hiyo;
mimi ni mtanzania
mimi ni mwafrika
mimi ni mdunia
mimi ni mwanadamu
maana ya tanzania, najua
maana ya afrika, najua
maana ya dunia, najua
maana ya mwandamu, najua
nawauliza wazanzibari,
nini maana ya zanzibari,
nani aliipa jina zanzibari,
kwa nini wajivunie uzanzibari?
Kwa nini wasijivunie utanzania?
jina ni jina tu, hata kesho likibadilika na kuwa JAMHURI YA SOKWENYIKA kwa mfano, it doesnt make any difference. mimi nilizaliwa Tanzania kwa maana ya the land of Tanzania. any time and under proper condition, the same land can be called any other name,
watu wa dunia ya leo wanatazama mbele sio nyuma.
watu wanajiuliza juu ya uraia wa nchi mbili au zaidi, sisi tunajiuliza uraia wa nusu nchi!
watu wanazungumza namna ya kuvutia uwekezaji wa kimataifa, uondoshwaji wa masharti ya visa, sisi tunazungumzia kichefuchefu cha neno "bara" kwenye utambulisho wetu, tunataka turejee kwenye nchi mbili na kurudisha masharti ya passport na visa
watu wanahangaika na mazungumzo ya ushirikiano/uundwaji wa shirikisho, soko la pamoja, ushirikiano katika masuala ya sayansi na tekinolojia, umoja wa forodha, sarafu moja nk sisi tunazungumza namna ya kuvunja muungano!.
jambo la msingi la kujiuliza ni je, tunapiga hatua kimaendeleo au tunarudi nyuma? tunakwammishwa na jina hili tanzania, au ni kitu gani kinatukwamisha tusiendelee kwa kasi tuliyotazamia? kama hatupati maendeleo tunayohitaji kwa kasi tunayotazamia, je, tatizo ni nini, ni jina la Tanzania?
tusijidanganye wapendwa. watoto na wajukuu zetu watatuthamini zaidi sisi na mchango wetu kama watakuta nyumba nzuri, barabara (na miundombinu mingine) nzuri, katiba nzuri, sheria nzuri, jamii iliyostawi vizuri, amani, maelewano mazuri ya kimataifa, maelewano mazuri ya kijamii nk hata kama tutakuwa bado tunabeba utambulisho wa "Tanzania". kinyume chake, hata tukirudia utambulisho wetu wa "Tanganyika" lakini tukakosa haya mambo niliyoyataja, watoto wetu watajuta kuzaliwa "Tanganyika".
tusipoteze dira ya maendeleo, tukageukia jina kama mwarobaini kwa kisingizio cha "jasiri haachi asili" ama uzalendo nk. tusipoangalia tutapoteza muda mwingi sana kwenye cheap politics za majina tukaacha kando masuala muhimu ya maendeleo na hakika tutachekwa na wenye akili
Nasikia mara ohhhh, wabara wanatuonea, wabara wanatudharau. Sisi si wabara, ni watanganyika bana!
Muungwana haachi asili. Nia yangu si kuanzisha thread ya kupinga muungano, bali sipendi kuitwa mbara na ndio maana ninasema sisi sio wabara, ni watanganyika. Ukisema Tanganyika ni jina la kikoloni, basi kataa pia majina ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Tanga na mengine mengi yanayopatikana katika ramani iliyochorwa na mkoloni.
Alisema kama wao "Wanzanzibari watawakataa Watanganyika na kujitenga, hawatabaki salama wataendelea kujibagua kiasi cha kuwa na wapemba na wa unguja. Na ikitokea hivyo basi Tanganyika itabaki salama." Ila na sisi Watanganyika tukiwakataa wale na kujitenga pia hatutabaki salama, ndiyo itatokea sasa wao wasukuma na sisi ni wanyamwezi. Na na dalili za awali zimeoneshwa na uvccm,baada ya kumtenga Masauni sasa wanasema Rais si lazima atoke Kaskazini, hii ndiyo dhambi ya kubaguana, Muundo wa muungano ndio unaotubagua mpaka tunapata Mzanzibari na M bara, na mswada hautaki tujadili muungano na unatutisha kuwa tutatupwa jela 2yrs, na sisi wengine tunataka kuwepo Jamhuri ya Tanzania itakayokuwa na serikali moja tu, na tukikubaliana hivyo kelele zote zitakwisha.nyeyerere alitabiri hivyo tu ? hata bara alitabiri itakuwa wanyamwezi na wamakua na wachanga na wamasai
nendeni tu ndugu yangu na nchi yenu makijipange upya tutaungana tena mkipata maendeleo mnayo yataka sawa hapo tutaweza kuishi bila manung'unikohata wamasai ,wanyamwezi, wasukuma na wengineo wanatanua tu zanzibar...usimuonee choyo mtu anadai haki yake just do the same dai haki yako ...taka kuwepo kwa katiba ya tanganyika na rais wa tanganyika na bunge la tanganyika na baadae ndio tuanze mambo ya muungano
Jamani hebu nisaidieni hapa.....ni mkoloni gani alieipa mipaka yetu jina la Tanganyika?
Na pia najua kabla hawajaja wakoloni mababu wa mababu zetu walikaa kwenye mipaka hii hii,,,hivi kuna mwenye Idea ilikuwa inaitwaje hapo awali? kabla ya kuitwa Tanganyika ......
Ila pamoja na kuitwa na mkoloni bado naweza jivunia nalo maana ni jina lenye maneno ya kiswahili "Tanga" na "Nyika" na lina tafsirika kwa lugha yangu.....
Mimi ni Mtanganyika na kama muanzisha Thread nachukia kuitwa M-bara......na ndugu zetu wa Zanzibar hawawezi kutuita Watanzania, huishia kutuita wabara kama tunavyowaita wazanzibar au wavisiwani.....
Hii thread yako inaleta maswali mengi na kuhoji uelewa wako juu ya muungano na maendeleo. Kama wewe sio anti-union naomba unijibu swali hili. "Kwa nini unapinga nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja yenye serikali mbili?
mkuu endelea kuwaelishima hawa watu ungwana pasipo haki hakuna .ubarikiwe sana .tuvunje muungano tukajipange upya tutarudi wote tunajua umoja ni nguvu utengano ni udhaifuIngawa hujajibu swali langu (post no. 47) nashiwishika kuhoji uelewa wako wa pro-union na anti-union. Nikija na sera ya kutaka nchi yetu iongozwe na serikali za majimbo utaniita anti-union? Watu wanaoshadadia muundo wa mungano wa sasa ni unionist wa aina gani pasipokuwapo na union?
Mimi sio anti-union bali ni unionist wa ukweli mwenye kutaka muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar; na hata ikiwezekana kuongeza Somalia ni sawa. Kumbuka hata Marekani ni muungano wa nchi 50 ambazo zina-exist, na zina mipango thabiti ya maendeleo. Sasa unapokuwa na muungano wa nchi mbili ambapo moja hai-exist ina maana gani. Huu muungano wenu wa 'Tanzania bara na Zanzibar umetoka wapi?'. Kumbuka hii sio thread ya muungano (maana ipo nyingine). Hapa nilitaka kumkumbusha mzanzibari akitaka kuni-distinguish, asiniite mbara bali mtanganyika. Mbona unapotea kwa kuleta hotuba ndefu ya maendeleo huku ukisahau asili yako? Mimi nina asili, na asli yangu ni Tanganyika.
Mushirikishwe zanzbar kwani nchi yenu ? Hapa kwani mulipiga kura kumchagua mualishi au rais ? Hii ni nchi kama mchi nyengine,ina maamuzi yake bila ya kumshirikisha mtu yoyote,kwa hiyo basi munachotakiwa nyinyi,murudishe nchi yetu itoeni ndani ya koti la muungano,tungeni katiba yenu,rais wenu,bendera yenu,bunge la sheria lenu,mufanye mutakavyo hatutowaingilia juu yahilo,Kilicho wazi ni kuwa Zanzibar (hata ikiitwa Tanzania Visiwani) imefanya mabadiliko ya Katiba yake ambayo yamezingatia mahitaji na maslahi yake ki-muungano. Isikubalike kuwa Tanganyika (hata ikiitwa Tanzania Bara) isifanye mabadiliko ya Katiba yasiyozingatia mahitaji na maslahi ya watu wake. Kuwa na uwakilishi wa 50/50 katika kila jambo ni kupuuza milioni 40 ya watu, huku umuihimu ukipewa kwa idadi ya nchi zilizoungana (nusu kwa nusu eti kwa sababu ni nchi 2 zimeungana). Kuchelewa kufanya mabadiliko ya ki-Katiba kusiwe ni udhaifu ambao Zanziba wanataka kuutumia sasa. Wa-Tanzania Bara hawakuhusishwa na mabadiliko ya Katiba Zanzibar. Lilichukuliwa kama ni swala na Ki-siasa zaidi (CCM na CUF).
Hii ndilo kosa ambalo CCM kwa kufahamu au kwa kupuuzia, haikulifanya zaidi. Na CCM isihusike sasa kufanya mabadiliko. Si swala la Rais wa kisiasa, ni swala la wananchi ktk ujumla wao, itikadi zao, imani zao, taaluma zao. It's not a political thing but rather socio-economical !!