Nchi ya Zanzibar kufutika kwenye uso wa Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi ya Zanzibar kufutika kwenye uso wa Dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, Jun 26, 2010.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nchi ya Zanzibar huenda ikafutika kwenye uso wa Dunia kama nchi iliyoungana na Tanganyika na kubaki kama mikoa ya Tanzania. Hii ni kwa sababu jina linalotakiwa kuzitambulisha nchi mbili zilizoungana (Tanganyika na Zanzibar) yaani Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) au United Republic of Tanzania (URT) limeanza kutotumika katika sehemu muhimu za utambulisho wa nchi hasa yanayohusiana na muungano. Mfano kwenye sarafu, linatumika "shilingi ya Tanzania" badala ya "shilingi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" au "Tanzanian Sh". badala ya "United Republic of Tanzania Sh." (URT. sh.), kama ilivyo kwa "United States dollar" (US $), "United Kingdom Pound" (UK pound). Pia jina la ramani, huitwa Ramani ya Tanzania badala ya "Ramani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Timu ya Taifa huitwa "timu ya taifa la Tanzania" badala ya "Timu ya Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Na sehemu nyingine nyingi ambako jina la URT lingetumika badala yake Tanzania ndilo hutumika.

  Wazanzibari amkeni mhakikishe utambulisho unaotumika ni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) au United Republic of Tanzania mahali popote pale ambapo maslahi ya nchi mbili huru zilizoungana yanawakilishwa la sivyo you will be forgotten forever!
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hivi kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kulikuwapo na jina Tanzania? Tanzania limietokana na nini? Kama ukitamka Tanzania manake umetamka Tanganyika na Zanzibar, sasa hiyo muuungano unayotaka itamkwe kila mahali ni kwajili y nini? Wewe mwenzetu unaishi dunia gani, usiyelijua hili? By the way malalamiko haya yalikuwa yaanzishwe na watu wa Tanzania bara ambao jina lao la Tanganyika lilipotea kabisa, huku watanzania visiwani wakibaki na jina lao la Zanzibar. Hivi muungano ukivunjika, bara kutaitwa nini? Nisingeshangaa kama hoja hii ingeletwa na mtu wa bara, on my suprise watu wa Zanzibar ndo mnakuja nayo hii. Wewe bwana ni mchokozi.
   
 3. bona

  bona JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  global warming is gonna help us settle this issue, its just a matter of time!
   
 4. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Jina lililochaguliwa kuwakilisha nchi mbili hizi baada ya kuungana ni Tanzania na wala si vinginevyo. Mbona unapenda u-mimi?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Highfallutin' hyperbolics of hued hogwash and hyped hot hullaballoo hijacking the hall like hyponychon.
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  duh! hapa hata OBAMA mwenyewe inabidi akatafute dikshineri hehehe haki ya nani nimeelewaga hizo buluu tu.
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Tanganyika ndio Tanzania kwahiyo Zanzibar inatawaliwa Tanganyika
   
 8. doup

  doup JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  hivi Tanganyika isinge ungana na Znz mpaka leo hii ingeendelea kuitwa Tanganyika?
   
 9. doup

  doup JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180

  tafadhali usiombee hayo
   
 10. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  Obama utakuwa unamuonea..tufanye malkia Eliza.kabisa....duh najuta kusoma shule za kina Kayumba
   
 11. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,124
  Likes Received: 23,733
  Trophy Points: 280
  Kama hujanyaka kitu hapo basi inabidi urudi shule~Ha ha ha!.:dance:
   
 12. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hivi wewe uliyeleta hii posti ni nani Mtanzani, Mzanzibari, au Mzanzibara? nataka kujua tu.
   
 13. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mimi nimemwelewa point kubwa hapa ni kukuza jambo ndicho mwandishi anachosisitiza
   
Loading...