Nchi ya Vikosi kazi na tume

mulambakao

Member
Jul 13, 2011
28
3
Kama vile hatuufahamu ukweli!

Kuanzia kwenye maswala ya kijamii, siasa, michezo, taaluma n.k, mambo yako wazi kabisa mfanao, umeme kuzimika Taifa mwishoni mwa mashindano ya Kagame-unda tume, katibu mkuu wa wizara fulani kafanya madudu fulani-unda tume, madaktari wamefanya nini na nini-Temeke, Amana, Muhimbili, M/nyamala etc. Mara ukumbi fulani wa starehe (watoto wamepoteza maisha kwa kukanyagana, kukosa hewa -unda tume, (umeme,madini to mention a fraction)Tume zina majina ya majaji, watu maarufu wote nchini 'angalau Tume iliyoongozwa na Mwakyembe!

Haya tuunde vikosi kazi, mfano mabomu Mbagala, G/mboto madawa ya kulevya (naona sasa wanataka kuunda timu nje ya tume na kikosi kazi'i don't know if they are watchdogs within'), na majibu 'results' na repoti zinazotokana na hizo tume (kwanza sijui kama zinakuwa archived, nafikiri nyaraka hizo zitajaza ukumbi) je zinafanyiwa kazi? Je, tunajifunza lolote kutokana na hizo repoti?

Wakati mwingine labda tungeweza tu kunukuu repoti fulani ambayo ina mazingira yanayofanana na kuhitimisha (conclude) Na hizo tume, timu, vikosi kazi vinatumia rasilimali muhimu ambazo zingeweza kutuletea afueni katika maisha ya kila siku.

Je hili linaonekana kweli?

Bila kujua, inawezekana kabisa kuna tume/timu/kikosi kazi kinachochunguza/shughulikia JF naomba kutoa hoja
 
mbaya zaidi nyingi za tume zinaongozwa na majaji ila zikishamaliza uchunguzi zinapelekwa kwa mahakimu.
mahakama hazina kazi,
polisi hawana maana ,
takukuru inamaliza hela za watanzania.
ningependekeza tume zikimaliza kazi washukiwa wafunguliwe milango ya lupango,hakuna haja ya kurudisha tena kesi nyuma.



na hapo ndi[po umaskini wetu ulipolalia.
 
Poleni sana wafiwa na wale wote walioathirika na ajali hii mbaya ya majini. Poleni wananchi wote na wale wote wasio na hatia kwa kupata mshtuko, wasiwasi na huzni kwa kitendo cha kupotelewa na ndugu zetu, watoto, jamaa na jirani zetu.

Ajali nyingi zinazotokea Tanzania zinaepukika sana. Chanzo cha ajali zetu nyingi ni uzembe, rushwa, na kujua sana. Ni nani asiyejua kwamba lori sio salama kubeba watu na watoto, ni juzi tu mjini Igunga nimeshuhudia malori yakibeba watu wakubwa na watoto na viongozi wengi wa juu wa serikali na vyama vya siasa wakishuhudia bila kujali wala kukemea eti kisa ni mashabiki wa vyama vya siasa. Ni nani asiyejua kwamba lazima chombo cha abiria kiwe kime faulu vigezo vyote vya usalama kabla havijatumika. Nania asiyejua kuzidisha abiria au mizigo kwenye ndege, gari, meli, boat nk huhatarisha usalama wa usafiri wa chombo husika.

Je ni kweli tunahitaji tume ili mamlaka ya udhibi usafirishaji ifanye kazi yake? Kweli tunahitaji tume kujua meli iliyojaa kupita kiasi na nzee ambayo labda ilishatolewa kwenye matumizi? kweli tunahitaji tume kwa meli ambayo hata wamiliki hawajui kulikuwa kuna watu wangapi wakati tayri tumeopoa watu zaidi ya 800 kabla ya mizigo? Kweli hii ni mara ya kwanza kutokea? Ni nani anajua uwezo wa kivuko cha kigamboni? kweli haya huzingatiwa ama mpaka kizame tuitishe tume.

Nakumbuka MV Bukoba tulijifanya tumejinza, nakumbuka ajali ya treni dodoma tulijifanya tumejifunza, nakumbuka ajali za barabarani kila siku ambazo tumeweka pamaba traffic wakijitahidi kukusanya rushwa ili kuwagawia wakubwa zao.

Kwa nini wasife hao wana siasa wanafiki wenzao wakapa uchungu tunaoupata, kwanini wasife hao wanasiasa wanafiki wenzao wakajua wao hawapo mbinguni inaumiza sana kuletewa usanii wa tume kwenye maisha ya wasio na hatia wala kujua.

Hatuhitaji tume kwa mambo yalio bayana, kilicho tokea Nungwi ni uzembe, rushwa, na uongozi mbovu. Hakuna haja ya tume kula fedha za walipa kodi mnowau hizo fedha wapeni hao waliobakia yatima na waliopoteza ndugu na watu wanaowategemea. Usalama wa Raia Tanzania ni sifuri hakuna wala hakuna kiongozi anayejali, wote ni wanafiki, waongo na wanakera sana. Waonaona ni mtaji wa kuombea misaada tunapopoteza maisha. OOh bara bara zetu mabya, ooh hatuna meli nzuri oohh hatuna hospitali na dawa. Mbona sote hututumii hivyo hivyo???.


Ukisikiliza hadithi za waliokoka na maiti za watoto wadogo wale wasio na hatia muda meli iliyotumia kuzama umbali kutoka ufukweni hakuna neno unaweza kutumia zaidi ya UZEMBE NA SERIKALI ISIYOJALI WATU WAKE. Viongozi hawa linapokuja swala la kushinda uchaguzi wako tayari kununua meli 50 kwa idadi ya fedha wanazotumia ili waje watuue kwa neno tutaunda tume. Hakuna mwenye haja ya tume zenu. Kwani ile ya MV Bukoba haikuwapa majibu enyi wanafiki na wasaliti wa wananchi wenu. Natamani hizi ajali zingehamia kwenye ma VX yenu ndio mngejua uchungu wa maneno matamu yasiyorudisha roho ya mwanadamu.

Wananchi wanahitaji vyombo salama na mazingira salama, wanahitaji mamlaka zinazotimiza wajibu wake, wanahitaji uwajibikaji kwa mujibu wa sheria. Kama llile boti lingekuwa na vyombo vya usalama vya uokoaji, kama bandari ya Zanzibar na Pemba ingekuwa na vyombo vya uokoaji na mawasiliano. Kama Boti lile lingebeba kutokana na uwezo wake kama kila mmoja angetimiza wajibu ndio ajali inaweza kutokea ila sio kuuwa watu wetu wengi hivi.

Hakuna jipya serikali inaweza kutuletea zaidi ya ngonjera na kusubiria maafa mengine yatokee wajifanye wanaogopa kuangalia maiti zetu. Ni maghorafa mangapi yametuua na wamefanya nini? huwa wanalipuka kama moto wa kifuu halafu wanapatwa na ganzi. Ni nani amabye hajaona sumu ya maji ya Barricks yanavyowafanya wale watu wa Mara mpaka waanze kufa kama nzige ndio utawaona viongozi wetu wanafiki wakijifanya kushtuka.

Hatuwezi kuendesha nchi kwa tume, wapi usalama wa taifa, wapi takukuru, wapi polisi, wapi mamlaka zinazohusika, wapi wabunge, wapi madiwani, wapi ma dc, wapi wakuu wa mikoa, wapi Raisi na mawaziri. Hawa wote wanakula kodi zetu bureeeeeeeeeeeee kabisa leo mnataka tume. come on
 
Ajali za hapa nchini zote ukichunguza utakuta kuna elements za crime ndani yake. Huwa najiuliza, hivi jeshi la Polisi kazi yake ni nini? Hivi hawa viwavi wannapokwenda Moshi kwenye chuo chao huwa wanajifunza kusimamia mechi za ligi kuu uwanja wa taifa, kuomba rushwa na kubambika kesi?

Kwenye nchi zinazoongozwa na serikali tukio lolote la ajali iwe kubwa au ndogo lazima Polisi ifanye uchunguzi na kisha sheria ifuate mkondo wake. Lakini katika nchi kama hii ambapo serikali imewekwa mfukoni na wauza unga, wezi na washenzi wa aina zote tume ndiyo kitu cha kupata ufumbuzi wa mambo. Hapa tunahitaji mapinduzi tu.
 
Jambo likitokea fasta fasta address the NATION na unda TUME, by the time TUME inamaliza kazi yake wananchi watakuwa wameshasahau kwani muda huo kutakuwa na jambo jingine tena litakalowa keep busy wasikumbuke hili kwani litakuwa limeshapita na siku zinasonga, bila kufanya hivyo huwezi kuongoza nchi.

 
Kazi ya polisi huijui auu........si KULIPUA MABOMU YA MACHOZI NA MAJI YA WASHAWASHA......
Ajali za hapa nchini zote ukichunguza utakuta kuna elements za crime ndani yake. Huwa najiuliza, hivi jeshi la Polisi kazi yake ni nini? Hivi hawa viwavi wannapokwenda Moshi kwenye chuo chao huwa wanajifunza kusimamia mechi za ligi kuu uwanja wa taifa, kuomba rushwa na kubambika kesi?

Kwenye nchi zinazoongozwa na serikali tukio lolote la ajali iwe kubwa au ndogo lazima Polisi ifanye uchunguzi na kisha sheria ifuate mkondo wake. Lakini katika nchi kama hii ambapo serikali imewekwa mfukoni na wauza unga, wezi na washenzi wa aina zote tume ndiyo kitu cha kupata ufumbuzi wa mambo. Hapa tunahitaji mapinduzi tu.
 
Tangia 2005-2011 kuna "Tume" ngapi zimeundwa kufuatilia masuala mbali mbali yaliyotusibu hapa Tanzania?

Na Je, kuna tume ambayo ilikwisha toa taarifa au mapendekezo na yakafanyiwa kazi?

Mwenye kufahamu tafadhali...

Nawakilisha
 
Back
Top Bottom