Nchi ni lazima iendeshwe kwa mujibu wa Katiba ya nchi

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Katika awamu 3 za uongozi, nchi ikiwa katika mfumo wa vyama vingi, ni wazi kabisa kuwa serikali ya awamu ya 5 ndiyo iliyoonyesha kuwa yenyewe haitaki kuendesha nchi hii kwa mujibu wa Katiba ya nchi na badala yake imekuwa ikiendeshwa kwa kuzingatia matamko ya Rais wa nchi, hata kama matamko hayo yanavunja Katiba ya nchi waziwazi, watendaji wa serikali hii ya awamu ya 5 wamekuwa wakiyatekeleza kikamilifu!

Ingawa kwenye utawala bora unaozingatia sheria, kigezo kikubwa huwa kinakuwa namna serikali hiyo inavyoheshimu utawala wa Power separation ya mihimili 3 ambayo ni Executive ( Mhimili wa Urais) Judiciary( Mhimili wa mahakama) na Legislature( Mhimili wa Bunge)

Mfumo huo wa Power separation umewekwa kwa lengo la kila mhimili ufanye shughuli zake bila kuingiliwa na mhimili mwingine, lakini wakati huo huo mihimili hiyo ifanye kazi katika kike kitu kinaitwa checks and balance.

Kwa Bahati mbaya kwenye utawala wa serikali ya awamu ya 5, ni kama hautaki kuzingatia hiyo kitu inayoitwa Power separation na badala yake mhimili mmoja ambao ni Executive ndiyo unaojiona wenyewe uko supreme zaidi ya mihimili hiyo mingine 2 ambayo ni Bunge na Mahakama.

Nitatoa ushahidi ni kwanini naamini mhimili wa Executive unajiona ndiyo supreme na unaamua kuiingilia mihimili hiyo 2.

Mara tu serikali ya awamu ya 5 ilipoingia madarakani iliamua kufuta Bunge Live kwa madai kuwa wakati huo wa vikao vya Bunge vinapoonyeshwa Live, watu wanakuwa makazini , kwa hiyo kwa kuwa serikali hii ina kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, kwa hiyo ni muhimu wakati huo wananchi wakawa wako kazoni , badala ya kuwa pembeni za luninga zao na kuangalia Binge Live!

Hata hivyo wananchi tulishangazwa na kuona sababu iliyotolewa na serikali kuwa ni uongo, baada ya kushuhudia shughuli nyingi anazofanya Rais muda huo huo wa kazi, vyombo vya habari vya luninga vikirusha matukio hayo Live!

Hata hivyo baadaye zilipatikana habari kuwa Rais aliwahi kusema kuwa ni yeye mwenyewe aliyepiga Stop Bunge kuonyeshwa Live!

Kwa maana hiyo huo ni ushahidi tosha kuwa mhimili wa Executive umevunja Katiba ya nchi kwa kuuingilia mhimili mwingine wa Bunge!

Vile vile katika awamu hii ya 5, ingawa mihimili 2 yaani Bunge na Utawala yote ina viongozi wake kamili ambao ni Rais kwa upande wa mhimili wa Utawala na Spika kwa upande wa Bunge, lakini kwa upande wa mhimili wa Mahakama tumeshuhudia kwa Mara ya kwanza tokea mfumo wa vyama vingi urejee nchini mwaka 1992, mhimili huo ukiongozwa na Kaimu jaji Mkuu kwa zaidi ya miezi sita sasa!

Hali hiyo inaonekana ni mkakati madhubuti unaosukwa na mhimili wa utawala kutaka kuidhibiti mhimili wa mahakama.

Tumeshuhudia pia kauli mbalimbali za Rais zinazoonyesha kuwa yeye anaamini kuwa mhimili wake wa utawala uko juu ya mihimili mingine.

Tuliwahi kushuhudia akitamka kuwa mhimili wake ndiyo uliojichimbia chini zaidi....

Tuliwahi pia kumsikia akitamka kuwa kwenye utawala wake hataiangalia sana Katiba ya nchi inasema nini, Bali yeye jukumu lake kubwa ni kuinyoosha nchi!

Hivi Rais unawezaje kuinyoosha nchi bila kufuata Katiba ya nchi?

Hivi uapishwaji wake wa kutakiwa aitii na kuilinda Katiba ya nchi kabla ya kushika madaraka ya Urais ilikuwa sawasawa na kusema ilikuwa kama formality tu?

Hivi Rais anawezaje kumpongeza Spika kwa vitendo vyake vya kuwanyanyasa wabunge wa upinzani na kuwatimua Bungeni ambao huwa wanatekeleza kikamilifu wajibu wao wa kibunge wa kuisimamia serikali huku wabunge wenzao wa CCM wakiamini kuwa wajibu wao mkubwa Bungeni ni kuikingia kifua serikali yao?

Hivi inawezekanaje Jeshi la Polisi liendelee kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani huku wwkiruhusu mikutano ya kisiasa ya chama tawala cha CCM wakati Jeshi hilo la Polisi likijua wazi kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inabainisha wazi kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi vya siasa na vyama hivyo vinatakiwa kufanya shughuli zao vikiwa huru?

Kama kweli serikali hii ya awamu ya 5 ina nia ya dhati ya kuleta maendeleo ya nchi ni lazima ifanye shughuli zake kwa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi ambayo inaeleza kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama na Katiba hiyo hiyo Ibara ya 18(1) inatoa Uhuru wa kila mwananchi kutoa maoni yake bila kuingiliwa na chombo kingine chochote.

Inashangaza pia kwa wanaccm kutomuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye katika hotuba yake aliyoitoa mwaka 1995 alibainisha wazi kuwa Rais ambaye hataki kuongoza kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda na kuitii kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa hili, Rais wa aina hiyo HATUFAI.

[HASHTAG]#hatunyamazi hadi tuwe wafu#[/HASHTAG]
 
Kwa Bahati mbaya watendaji wengi wa serikali ingawa wanajua wazi kuwa wao ni watumishi wa Umma ambao hawatakiwi kujiegesha na chama chochote cha siasa, lakini kiuhalisia watendaji hao huwa wanafanya kazi utadhani wameajiriwa na ofisi ya Lumumba!
 
Nchi inaendeshwa kama gari bovu lililokatika usukani, ambapo hatujui dereva anatupeleka wapi
By Mzee Mwinyi
 
Katiba ilikuwepo vizuri sana na ilitumika vibaya...kila kiongozi alikuwa anafanya anavyotaka yeye Katika ofisi ya umma.Mpaka wengine wakawa miungu watu ktk ofisini zao.

Sasa Dr Magufuli ameamua kuwarudisha kila mmoja kwenye reli kwa nguvu zote.

Na Tanzania bila kiboko mtu haendi.Ndiyo anachopambana nacho Dr Magufuli.
 
Naheshimu mawazo yako Mkuu

Sasa nikuulize swali dogo tu, kama Katiba ya nchi haina umuhimu huo kama unavyotaka kutuaminisha, ni kwanini basi inakuwa ni jambo la lazima kwa Rais yeyote kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuliongoza Taifa letu, anaapa ili ailinde na kuitii Katiba yetu ya nchi?
 
Kuwepo kwa katiba ni jambo moja,kuilinda na kuitetea ni jambo lingine.

Katiba inaweza kuwepo tena nzuri na viongozi wakaikanyaga pia.

Issue ya katiba ni maadili,nidhamu,moyo,uzalendo wa wanainchi ktk kufuata na kutekeleza sheria,taratibu na kanuni walizokubaliana kuishi toka ktk mioyo yao au hiyo Katiba.
 
Tatizo kubwa ni wananchi sisi , tukiamua uyu mbabe hawezi kufanya anachofanya ila bahati mbaya tumejawa na ushabiki , ujinga, uchama, uzalendo wa kinafiki, ubinafsi na ujinga, kama tungekuwa tunaipenda nchi yetu uyu jamaa angefuata katiba na sio utashi wake kwa kivuli cha katiba , tusibili miaka 50 ijayo watoto wa wajukuu zetu wanaweza hawana haya matatizo
 
Back
Top Bottom