Nchi itapata hasara gani tukifuta bunge?

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
1,198
Reaction score
2,868
Baada ya kufuatilia mjadala wa bunge walipokuwa wanajadili azimio la kukodisha bandari nimejikuta nawaza kama Kuna hasara yoyote tutaipata kama taifa tukiamua tulifute bunge

Najaribu kufikiri kama kushauri tu wanashindwa, kama kutoa maoni mbadala wanashindwa, watapata wapi courage ya kukosoa au kusimamia serikali? Pigia mstari kusimamia serikali au liite ku - supervise the government halafu tafsiri kwamba anayesimamia ana elements za u Boss! Yaani hili bunge ndo liwe Boss Kwa serikali!!!! Vichekesho Kwa kweli

Msiniulize maswala ya matakwa ya Katiba au mambo gani gani ya kimataifa Wala protokali gani sijui mifumo ya nchi upuuzi gani

Najaribu tu kuwaza maana sioni faida ya hawa watu zaidi naona watu wazima wakijidhalilisha mbele ya watoto na wajukuu zake.

Hizi fikra za kishetani zimegoma kutoka labda mniombee
 
Hakuna hasara yeyote tutakayopata watanzania zaidi tutapata faida ya pesa za bunge kuelekezwa sehemu nyingine kama shule,hospital n.k.Kwa tz sijawahi kusikia mswaada wowote unaoletwa na serikali ukapingwa bungeni hata kama unamapungufu.mfano tumeona mkataba wa gesi ya mtwara,richimond,escrow n.k.zote hizi takataka zilisifiwa sana huko bungeni lakini mwisho tunaanza kulia na kusaga meno.
 
Sio Bunge la Tanzania tu,Mabunge duniani kote hayana umuhimu basi tu ni mifumo ya dunia imewekwa hivyo but kiuhalisia kuwa at the end Serikali na watendaji wake huwa wana take control ya kila kitu
 
Uongo, Marekani pesa haitolewi kwa serikali, hakuna mpango au mkataba wa nchi bila kupitishwa na mabunge yote mawili.
Sio Bunge la Tanzania tu,Mabunge duniani kote hayana umuhimu basi tu ni mifumo ya dunia imewekwa hivyo but kiuhalisia kuwa at the end Serikali na watendaji wake huwa wana take control ya kila kitu
 
Sio Bunge la Tanzania tu,Mabunge duniani kote hayana umuhimu basi tu ni mifumo ya dunia imewekwa hivyo but kiuhalisia kuwa at the end Serikali na watendaji wake huwa wana take control ya kila kitu
Siyo mabunge yote.bunge la marekani liliigomea serikali kuingia mkataba wa kihuni na Dp world ambao sisi tumeingia
 
Tunaweza kuliondoa Bunge la aina hii, tukawa tunakusanyika Nchi nzima chini ya mwembe ili kutunga sheria zetu lakini swali ni tuwe tunakusanyika mkoa gani? na usafiri utakuwaje au tuwe natembea kwa miguu?

Imagine milioni sitini chini ya Mwembe sijui kama kuna mkataba utafungwa zitakuwa ni ngumi tu.
 
Kwakuwa wakwenu waligaragzwa mchana kweupee, ndio maaana unaona bungee halina .maana.
 
Mkuu umefika Mbali Hata Saa100 akijiuzulu Mbona Hakuna hasara
 
Kwakuwa wakwenu waligaragzwa mchana kweupee, ndio maaana unaona bungee halina .maana.
Kwenye ukoo wetu hakuna mwenye kujihusisha na haya mambo ya kuongea huku nafsi, mdomo, mwili na utashi vikibishana na kusononekea maneno yanayotoka kinywani
 
Mi Nadhani taasisi ya elimu Tanzania ifutwe ,vyuo vikuu vyote vifutwe ni bora tubakiwe na veta tu............maana hivyo vingine sielewi........unajiita una degree harafu unakunya kunya tu.........bora tuwe kama Sudan tu kutakuwa na kueshimiana ...mliopo vyuo hakuna mnachokijua kazi kuchezea kodi tu mbwa nyinyi..........wasomi wote mabwege
 
Bila machafuko, hili bunge kibogoyo litaendelea kuwepo sana, na litapitisha mambo ya hatari kama haya.
 
Sio Bunge la Tanzania tu,Mabunge duniani kote hayana umuhimu basi tu ni mifumo ya dunia imewekwa hivyo but kiuhalisia kuwa at the end Serikali na watendaji wake huwa wana take control ya kila kitu
Bunge la Uingereza ulishalifuatilia? Wale ni vichwa acha kabisa...
 
Wabunge wengi waliwazumgumza wa Tanzania kama watu wasio na elimu, uelewa wa mambo na maarifa, na hili ndilo hawa watu huwaona wananchi ni kama nyumbu, wakimalizia na tule tumisamiati twa English wanajikuta ma genius na watu wa kipekee wenye hadhi kuliko wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…