Nchi inayumba kama gari lenye dereva mwanafunzi (learner) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nchi inayumba kama gari lenye dereva mwanafunzi (learner)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bakari Maligwa, Nov 12, 2011.

 1. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Tanzania inayumba kiuchumi, kijamii na kisiasa! Hakuna shaka yoyote kwamba, kama gari, basi dereva anayeliendesha ni "mwanagenzi" na mwenye "leseni" ya "learner" inayomfanya afanye majaribio mengi akiwa barabarani! Hakika, analiendesha gari pasipokuwa na maarifa, ustadi maadili ya aina yoyote. Angalia:
  1. Uchumi binafsi na wa jamii umeparaganyika: maisha magumu kwa kila sekta na hali ya "shilingi" inaporomoka kila siku;
  2. Siasa inaendeshwa kwa "ubabe" na matumizi makubwa ya nguvu za kipolisi;
  3. Jamii imesambaratika na kwa sehemu kubwa hakuna utu na heshima kwa sehemu kubwa ya watu kwa vile kila mmoja anaangalia "tumbo" lake: uchoyo; uroho; uchu na ulafi umekuwa sehemu ya maisha ya wanasiasa wetu wengi;
  4. Uongozi wa nchi umeachwa shelabela ilhali hakuna "uwajibikaji" kwa taasisi za juu zinazoongoza nchi katika kuelekeza uchumi, jamii na siasa; na
  5. Wananchi wa kawaida wanaendelea kuchoka na kuamua kuchukua mkondo wa "liwalo" na "liwe" na hapa ndipo tunapoweza kushuhudia kuanguka kwa mujtamaa wa maisha ya amani na utulivu yaliyozoeleka kwa miaka takriban 50 sasa.
  Dereva aliyekabidhiwa gari anaendesha kana kwamba hajui anapolipeleka gari! Anasukuma siku zake ilhali akijua kwamba gari si salama mikononi mwake na kuna kila dalili kwamba gari limemshinda! Usukani unamyumbisha; gear (gia) anashindwa kupangua; na giza limeanza kuingia hata taa za gari haziwaki; badala ya kutazama mbele anatazama usukani...kuna dalili mbaya kwamba kama hakuna jitihada za makusudi za kulinusuru gari linalokwenda mwendo wa kusuasua tunaweza kushuhudia "ajali" mbaya kwa gari hili! Mwenyezi Mungu aepushe; japokuwa si laana kuomba "ajali" itokee isipokuwa kuna dalili ya "ajali" mbaya ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. TAFAKARI; CHUKUA HATUA!
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bora dereva mwanafunzi!!
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  dereva mwenyewe licha ya uanafunzi kalewa basi balaa tupu
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  wewe kwa nini nchi isiyumbe ikiwa watu kama ngeleja na riz1 wanao behave kama anabalehe ndio viongozi, hakuna umeme miaka yote ila hakomi kumchafua mwamvita na jaunary? aache majungu alete umeme. january rais wetu 2015 aende huko akajisafishe masaburi. baba zima linasambaza email feki ili january anyamaze baada ya kuonekana hafai. too low for ngeleja
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ngoja magamba wakusikie!
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Hebu weka wazi kidogo juu ya hili mkuu, nahisi kuna dalili za ukweli
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  katiba mpya ndio mwisho wa unyanyasaji ktk tanganyika yetu!
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  gari haiendi mbele kabisa mkuu. dereva hana hata uwezo wa kununua mafuta ili gari isonge mbele na badala yake anamalizia yote, hivyo muda si mrefu gari itaanza kupiga vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, then inazima kabisa. We hii nchi hata familia ya mkuu wa kaya ni viongozi, je ni kwa katiba ipi? angalia Mkuu si Mkuu, Mkewe si mkewe, Makamu wa Rais si Makamu; unajua nini? NI SAFARI TU NDANI NA NJE YA NCHI ILI WAKIMALIZIE HATA YALE YALIYOTUNZWA NA WALIOWATANGULIA. Hakuna wa kumshauri mwenzake ni mashindano ya safari tu bila kujali gharama. HAKIKA NCHI HAINA DEREVA NA NCHI INAZIDI KUANGAMIA.
   
 9. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Hiyo njia huyu dreva anapita hakuna trafiki wamsimamishe? au kwa nini abiria wasimnyanganye funguo kunusuru maisha yao maana wamelipia nauli?
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaaani dereva kalewa halafu anaendesha huku anakula matambuu na anaperuzi ukurasa wake wa fesibuku kwenye simu yale ya kihanjani
   
 11. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Uhuru1.

  Nimefuatilia post zako asilimia kubwa una deal na ngeleja ,mwavita na January.Hata kama thread haiendani utalazimishia kumwongelea ngeleja.Sitaki kusema kwamba ngeleja hana mapungufu yake makubwa katika uongozi hadi kutusababishia giza hadi leo,lah. Wasiwasi wangu ni kwamba unazo personal misunderstanding na ngeleja na unazileta hapa JF.Kama niko sahihi basi utakuwa unakosea.Masuala binafsi usiyalazimishie huku.Nakumbuka ulisema katika moja ya post yako kwamba ngeleja alikutaka na mkatoka nae.I think that is more personal.

  Jaribu kuwa focused kujadili mada husika ku avoid biasness.
   
 12. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Dereva kanywa value lakini dereva katukomesha mwee! Desember soon acount nil na kila siku job na mshahara mzuri pesa haina samani kabisa vitu bei juu laki kama buku. Ha ha ha baba miraji kiboko aisee! Then yupo kimya tu magogoni.
   
 13. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #13
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tangu lini mwendesha guta akalipeleka li scania wajemeni? Tulieni tu, ombeni mungu, halafu ndo amekaribia Senkenke.
   
Loading...