Nchi Inavyoliwa

Nchi Inavyoliwa

Siku inakuja ambapo Ikulu itauzwa kwa wageni ili wajenge hoteli kwa ajili ya kuendeleza utalii na kupata fedha. Siku hiyo haiko mbali.

Tanzania: British Firm Says Revenue From Gas Due After 10 Years: Everywhere eaters from outside decide fate of this country's economy, where are the leaders!? are they involved in a way? For whose advantage? What about tomorrow? Where is their hope for tomorrow? Do they think of Siera Leon, Mali, e.t.c? What do they expect when the citizens will wake up to reclaim their rights? Do they have brains? Does their brains work? Do they think about tomorrow? name it ...
 
Nasikia ijumaa wiki hii atakuwa tegeta eneo la magereji (wamiliki hawana hati) akifungua saccoss!!!????? (raisi anafungua saccos?) kwenye ofisi feki. Halafu akiondoka anawaacha wananchi wakimsema.
 
Nimependa sana hii article.
Kama nchi ingekuwa na investigative journalist kama huyu jamaa bila kujali hata kama ana maslahi ndani yake, atleast wananchi wangekuwa wanalishwa habari zenye nyama ambazo ni muhimu katika ustawi wa jamii.

Waandishi wengi Tanzania hawapendi kuhangaisha miili na fikra zao kutafuta habari, wengine hata bila aibu wana copy & paste kile kinachotokea hapa Jamii Forum (JF). Cha kushangaza magazeti mengi nchini yanaweza yakabeba habari moja inayofanana kwenye Kurasa zote za mbele.

Kuhusu habari. Inasikitisha kuona watu wasio wazawa wa nchi wanakuwa na VOICE & POWER zaidi ya wazawa, inafikia mpaka wanaogopwa na mamlaka ya nchi!!. This is absurd.

Kwenye nchi zao, huwezi kukuta kitu kama hii. Only in Tanzania.

Lakini kuna watu tumewakabidhi madaraka ya kusimamia rasilimali zetu. Kidogo kidogo tutagundua tumeuzwa kwa mwekazaji fulani.
 
Pole sana Binti Tanzania najua mumeo anakutesa kwa sana, lakini nakuomba ukipata nafasi ya kumchagua mume mwingine hapo 2015 usikubali kumrudia tena huyu mume asiyejua majukumu yake.
 
Imeandikwa na EDMUND MIHALE, Dar es salaam | Jumanne, Februari 26, 2013

Raia wa Uswisi, Dk. George Hess, anatuhumiwa kujimilikisha na kuuza ardhi ya ufukwe wa Amboni uliopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, kinyume cha sheria.



Dk. Hess, anayeishi nchini Kenya, kupitia tovuti yake ya ambonibeach.com, amejitangazia ‘Jamhuri’ katika eneo hilo, kuwa ndiye mmiliki pekee Tanzania mwenye ufukwe, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999.

Sheria ya Mipango Miji namba 7 ya mwaka 2008 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, inakataza mtu yeyote kumiliki ufukwe wa bahari bali fukwe zinapaswa kumilikiwa na umma. Lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni kuhakikisha fukwe hazihatarishi amani, ulinzi na usalama wa raia.


Pia sheria hizi zinalenga kupunguza uharibifu wa mazingira na kuwapa wananchi fursa ya kutumia fukwe za bahari kwa burudani, michezo na mambo mengine yenye tija nchini.


Mbali ya hilo, Dk. Hess pia kupitia tovuti hiyo, ametangaza kumiliki ardhi na kuiuza kinyume cha Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu cha 20 (1), kinachokataza wageni kumilikishwa ardhi ikiwamo ya maeneo ya ufukweni.


“Kuepusha mkanganyiko, mtu asiye raia [wa Tanzania] hapaswi kupewa ardhi isipokuwa kama ni kwa malengo ya uwekezaji chini ya Sheria ya Uwekezaji ya Tanzania ya mwaka 1977,” kinasema kifungu hicho na kuongeza:
“Ardhi iliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji chini ya sehemu ndogo ya kwanza ya sheria hii inapaswa kutambuliwa, kutangazwa katika gazeti la Serikali na kukabidhiwa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambacho kitatengeneza utaratibu wa haki ya mwekezaji kuitumia ardhi hiyo kuzalisha [si kuimiliki]”.

Tayari, Dk Hess ameuza viwanja tisa kwa watu mbalimbali kutoka nje ya nchi na wenyeji wapo waliojenga nyumba na wanaishi. Mmoja wa watu waliouziwa viwanja hivyo ni raia wa Zimbabwe mwenye asili ya Kireno, Martin Perela, na tayari amejenga nyumba na anaishi katika eneo hilo.

Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa Dk. Hess pamoja na sheria hiyo kukataza wazi, yeye anamiliki hati ya ardhi katika eneo hilo. Hati ya mwanzo ya miaka 99 aliyopewa wakati wa ukoloni ameikabidhi kwa kampuni ya Amboni Plantation Limited shamba la mkonge la Kigombe.
Ramani ya shamba hilo hadi sasa inaonesha kuwa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 12,000 lina hati moja na lilianzia katika Kijiji cha Kilale na kuishia Bahari ya Hindi.

Baada ya kuuza shamba hilo kwa kuligawa vipande viwili, alikabidhi hati kwa Amboni Plantation Limited, hivyo ambonibeach.com ikabaki bila hati.
Mbali ya ufukwe huo, uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa wageni wamekuwa wakimiliki fukwe nyingi katika maeneo mbalimbali ya nchi, hususan katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam ambako wameuziwa na wenyeji.Akizungumza na JAMHURI, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, alisema hana taarifa kuhusu umiliki na mgogoro wa shamba hilo.

Anasema hajawahi kuona au kusikia kuhusu mabadiliko ya matumizi ya shamba hilo, lakini ameahidi kufuatilia katika makabrasha ya Wilaya ya Muheza.
“Ninavyojua suala hili limevuka mipaka haliwezi kujadiliwa katika ngazi ya mkoa au wilaya hadi taifa, naomba uwasiliane na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, watakupa majibu,” amesema Galawa.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, amesema hataweza kushughulikia suala hilo kwa kuwa ana majukumu mengine.
“Hivi nani aliyekupa hizi habari? Bwana mie sina habari na hilo kwa sasa naangalia vipaumbele vya maji, elimu na kilimo kwa kuwa wananchi hawajaleta malalamiko yao kwangu.“Mie silijui wakileta nitalishughulikia na kutoa majibu lakini wasiliana na DED (Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya) atakuwa na majibu,” amesema Mgalu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Ibrahm Mtovu, alipoulizwa alimtaka mwandishi kumpigia simu saa 9 alasiri, lakini alipopigiwa siku ya Jumanne muda huo, alipokea simu na kukata mawasiliano.
Alipopigiwa siku ya Ijumaa, Mtovu alipokea simu na baada ya mwandishi kujitambulisha alimtaka apige baada ya dakika tano.

Baada ya dakika 10 Afisa Ardhi wa Wilaya Muheza, Selemani Kanunge, alipiga simu na kuiambia JAMHURI kuwa mgogoro huo upo na ni wa muda mrefu.
Amesema suala hilo limefanyiwa kazi na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kupitia vikao vya Kamati ya Ardhi. Waligundua suala hilo baada ya kusoma katika mtandao kuwa Dk. Hess anauza viwanja katika Ufukwe wa Amboni, wakamsimamisha na viongozi wa wizara wakafanya ukaguzi.

Amesema walimweleza utaratibu na akapeleka maombi katika Baraza la Ardhi la Wilaya na yakafanyiwa kazi kisheria.
Kanunge amesema walipeleka maombi yake kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kaskazini, Doroth Wanzala, naye akatoa kibali cha ardhi hiyo kupimwa.Hata hivyo, amesema suala hilo bado lina mkanganyiko mkubwa kutokana na Dk. Hess kukataa kupima viwanja hivyo kwa ramani iliyoidhinishwa na wizara, badala yake anatumia yake.Kanunge amesema Dk. Hess amekataa kupima viwanja hivyo kama inavyotaka ramani ya wizara, kwa kuwa haimruhusu kumikili ufukwe hivyo naye akatoa masharti kuwa atavipima mara tu akiruhusiwa kumiliki ufukwe.

Wanzala hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Majibu ya viongozi wa wizaraAkizungumza na JAMHURI, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Albina Burra, amesema hajui mabadiliko hayo ya ardhi.“Mie sijui lolote kuhusu eneo hilo, sijapewa taarifa au dondoo zozote - ziwe za maneno au barua - kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya shamba hilo.“Ninachoona mie ni kama wewe. Kuna mambo yanaendelea tu, naona nyumba zinajengwa na wala hakuna mchoro wowote uliopita kwangu, ili kupata majibu hebu muone Kamishna wa Ardhi, anaweza kuwa na majibu,” amesema Burra.

JAMHURI iliwasiliana na Kaimu Kamishna wa Ardhi, Bramsiden Sichone, ambaye naye alisema hana taarifa kuhusu suala hilo hadi atakapofanya utafiti na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mtu ambaye angesaidia katika suala hilo.
Akizungumza na JAMHURI, mtumishi huyo wa wizara ambaye hakuta jina lake litajwe gazetini, amesema mgogoro huo ni mkubwa kutoka na kila kiongozi kupata kigugumizi kuushughulikia.“Hapa hakuna kigugumizi kuzungumzia suala hili.

Hii ni nchi yetu lazima tuoneshe uzalendo. Hapa kuna matatizo makubwa, hakuna kilichofanyika kule katika kupanga mipango miji kuna mambo matatu ya kufanyika.
“Kwanza unapima eneo zima, pili kujua viwanja vinakaaje na mwisho upimaji wa viwanja vyenyewe hapa hakuna kilichoafanyika.“Sijui tunapata wapi ukakasi wa kusema hayo huyo bwana kakiuka sheria ya ardhi katika umiliki wala kubadilisha matumizi ya ardhi kinyume na sheria, kama ulivyoeleza mwanzo iko wazi kabisa.“[Sheria inasema] watu wasio raia hawatapewa ardhi isipokuwa kupitia TIC.

Si hivyo tu, hata kampuni za kigeni hawaruhusiwi kununua ardhi kutoka kwa wanakijiji bila kupata kibali kutoka TIC bali wanatakiwa kuwasiliana na Kituo cha Uwekezaji.
“Hata hawa TIC ni wateja wetu kama mteja mwingine. Wanakuja hapa na kununua ardhi kutoka kwetu, wao ndiyo wanawakodishia wawekezaji kwa muda maalumu utakaopangwa. Wakishindwa wanatakiwa kurudisha TIC,” amesema.Amesema sheria na sera za ardhi zinatamka wazi halmashauri ina mamlaka ya kugawa ardhi hadi ukubwa wa eneo la ekari 500 ikizidi hapo ni kazi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, chini ya Kamati ya Ardhi ya Taifa inayoongozwa na Kamishna wa Ardhi Taifa.“Ninalifahamu suala hilo, ndiyo kuna makosa makubwa, ndiyo maana umeambiwa uje kwangu kwa kuwa wanajua nalifahamu,” amesema.

JAMHURI imewasiliana na Meneja wa Amboni Beach, Steve Kabwoya, ambaye amekiri kuuza viwanja katika eneo hilo la ufukwe.
“Tumesitisha kuuza viwanja kutokana na mwanasheria wetu wa mwanzo kutudanganya kuwa tuna haki ya kuuza viwanja katika eneo hilo. Baada ya kubaini hilo tukasitisha, lakini sasa tumeamua kuwekeza katika hoteli,” amesema Kabwoya.

Amesema jambo hilo kwa sasa limesitishwa baada ya kubaini kuwa jambo hilo ni kosa kisheria. Hata hivyo, alipoulizwa ni viwanja vingapi vilivyouzwa hadi sasa katika eneo hilo, alidai kuwa swali hilo ni gumu kwa sasa na kwamba anayetakiwa kulijibu ni bosi wake Dk. Hess, aliyedai kuwa amesafiri kikazi.

Yaliyoandikwa kwenye mtandao
Tanga ni mkoa wa pili kuwa na bandari kubwa nchini Tanzania na ndiyo makao makuu ya raia huyo wa Uswisi anayemiliki Amboni Sisal Properties Ltd (ASPL).ASPL inamiliki mashamba matatu ya katani ya Kigombe, Pongwe na Magoroto ambayo yanajishughulisha na kilimo na utalii. Shamba la Kigombe huzalisha tani 2,000 za katani kwa mwaka na ni moja ya mashamba makubwa nchini Tanzania.

Linauza nusu ya mkonge safi ya daraja la 3L na 3S katika maeneo 20 tofauti duniani.
Katika wavuti wa kampuni hiyo, anajinadi kuwa anamiliki kiwanja cha ekari 360 za uwanja wa gofu wa kwanza Tanzania kwa uzuri na wenye makazi. Eneo hilo linafikika kirahisi kwa gari kutoka Tanga kwani muda wa dakika 40 kufika Pangani.

Anaendelea kujinadi kuwa barabara za Tanzania Bara kwenda Kenya ni nzuri na unaweza kuendesha gari kwa saa 10 kutoka Pangani hadi Nairobi na Mombasa hadi Pangani ni saa tatu.
Anasema kutoka Moshi hadi Pangani hutumia saa 4 na Pangani kwenda Arusha saa 5 na kutoka Dar es Salaam hadi Pangani ni saa tano na kujinadi kupitia mtandao huo kuwa ni karibu mno kutoka katika uwanja wa ndege wa Tanga, Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Anasema katika eneo hilo atajenga uwanja wa ndege kwa kiwango cha moramu na utaruhusu ndege ndogo kutua.
Kusini mwa shamba la Kigombe kutaendelezwa wastani wa mashimo 71, na viwanja 18 vya kuchezea gofu ambavyo vyote vitabuniwa na Tommy Fjastad. Uwanja wa gofu ndiyo utakaokuwa pekee wenye nyumba zilizojengwa katika viwanja vya nusu au ekari moja zitakazokuwa zinatazamana na Bahari ya Hindi.

Katika tovuti hiyo, Dk. Hess amsema kutakuwa na huduma za hoteli, uwanja wa ndege binafsi, viwanja vya tenisi, maduka makubwa, klabu za usiku, bwawa la kuogelea na mengineyo.
“Nchi imebarikiwa kuwa na wanyamapori wengi, ina jiolojia ya ajabu: kreta, volcano,” anajinadi.Maswali kwa ajili ya kuuza viwanjaKatika mtandao wake ameweka maswali na majibu ya kuvutia wateja wafike kununua viwanja kama ifuatavyo:-Swali: Wapi viwanja vilipoJibu: Kilomita 35 Kusini mwa Tanga kwenda pwani ya Barabara ya Pangani.

Swali: Ni jinsi gani unaweza kufika resort?
Jibu: Kwa kutumia gari kutoka Tanga dakika 40, Mombasa (saa 3), Kilimanjaro (saa 5), Dar es Salaam (saa 5).Swali: Viwanja vilivyoendelezwa ni vipi?Jibu: Ekari 360 kwa ajili eneo la gofu na ekari 200 vilivyopo ufukweni mwa bahari, ambavyo ni kwa ajili ya makazi ndani ya ekari 12,000 za zao la mkonge na za kilomita 8 ufukwe binafsi.Swali: Ni viwanja vingapi vinapatikana katika eneo la makazi?Jibu: Kunakadiriwa kuwa na viwanja 30 katika eneo la uwanja wa gofu na viwanja vikubwa kwa ajili ya makazi 50 ambayo yanakuwa kati ya ekari 3-5 mbele ya ufukwe wa bahari.Swali: Kama nataka kujenga nyumba ni kiasi gani cha fedha kitakachotumika?Jibu: Gharama za ujenzi wa nyumba, Tanzania ni dola za Marekani 40 kwa mraba wa futi moja.Swali: Kama nitanunua kiwanja na kujenga nyumba naruhusiwa kupangisha?Jibu: Ndiyo. Timu ya manejimenti itakusaidia kupangisha au kutoa mkataba wa kupangisha kwa watalii au watu binafsi.Swali: Nani atakayejenga nyumba yangu?Jibu: Unayo nafasi ya kununua ramani ya nyumba ya kuanzia vyumba vitatu au vinne kutoka kwa mkandarasi wetu au kuijenga mwenyewe.Swali: Kama nina mkandarasi wa kujenga nyumba yangu mwenyewe ni gharama kiasi gani nitatumia hadi kukamilisha nyumba?Jibu: Gharama za ujenzi Tanzania ni dola za Marekani 40 kwa mraba wa futi moja.Swali: Je, kuna zuio la kuunda mchoro wa ramani ya nyumba niitakayo?Jibu: Ndiyo. Nyumba lazima iwe aina ya ‘bungalow’ ikiwa na mapambo ya asili.Swali: Je, naweza kununua nyumba bila kuhusisha uwanja wa gofu?Jibu: Ndiyo unaweza kununua uwanja wa ufukwe kwa haki utakayo.
...mnashangaa hii!!!....hii mbona ndogo!!..nendeni Zanzibar mkaone fukwe na hotel zake zinavyomilikiwa na wageni(wazungu)....Ukiona mtu mweusi kule labda awe mchuuzi...au mlinzi..au mfanyakazi wa hotel......wanaokula nchi kule woote wazungu....utafikiri haupo TZ.......unbelievable yaani.....Naskia Karume aliuza sana ardhi kwa wageni(wazungu)wakati wa utawala wake.....na bado anapokea 10% sasa.....ndo maana hata siasa za majitaka za ccm hazifagilii.....Mnabisha...fanyeni utafiti.....nendeni beach za zenj......mtashangaa...
 
Good question. Enzi za Mwinyi walisema serikali ilikuwa likizo. Sijui hizi enzi za Kikwete tuziiteje?

likizo ya uzazi. Serikali ifike wakati ione haja ya kutimiza haja za wananchi
 
Imeandikwa na EDMUND MIHALE, Dar es salaam | Jumanne, Februari 26, 2013



Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, amesema hataweza kushughulikia suala hilo kwa kuwa ana majukumu mengine.“Hivi nani aliyekupa hizi habari? Bwana mie sina habari na hilo kwa sasa naangalia vipaumbele vya maji, elimu na kilimo kwa kuwa wananchi hawajaleta malalamiko yao kwangu.“Mie silijui wakileta nitalishughulikia na kutoa majibu lakini wasiliana na DED (Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya) atakuwa na majibu,” amesema Mgalu.

Nimeipenda sana para hii hasa hapo kwenye red coz, wananachi sjui watalima hewani au mbinguni ikiwa ardhi haitakuwepo, haya ndio matokeo ya teuzi za kupitia UVCCM. Dah, Ngoja niongeze miaka mingine ya kukaa ukimbizini maana hom kunatisha jamani, kwa majibu haya!!!
 
Tatizo la Tanzania ni kwamba hatuna serikali. Waarabu wanakuja wanajichotea wanyama. Wazungu wanakuja na kujitwalia maeneo makubwa ya ardhi. Wahindi wanaleta ndugu zao na kuwaajiri kwenye viwanda vyao na migahawa.

Wakisha pata 10% basi wanalala na kutalii ughaibuni!!
 
twala twaliwa, tumekopa trion 19 wajanja wanazirudisha kwa kujisevia ardhi.
 
Unategemea nini unapokuwa na Sampuli ya Raisi ambaye ni fast jet kutwa kiguu na njia kuhudhuria mazishi ya kila mtu ambaye vioo vya luninga vitamwonyesha wacha iliwe mpaka tutakapouzwa sisi wenyewe tuta tia akili
 
Vitu vya wendawazimu vilivyoshindikana vyote ambavyo havikubaliki sehemu nyingine vinawezekana hapa petu kweli kazi tunayo.
 
Utashangaa kusikia kuwa Ikulu nayo ilishauzwa na kuna mtu anakula rent kila mwezi pale. Kila kitu Tanzania kinawezekana.
 
Maana ya umma ni nini?

mimi na wewe kupitia serikali. Au una maana nyingine? Au una maana ya public? Umma ni kwamba hata masanja Maslakulangwa yule mchungaji apate access siyo hadi awe mpangaji wa Se Cliff ndio aogelee ufukweni!
 
Back
Top Bottom