Hakuna mkuu duniani na mbinguni ila ni mungu pekee ambaye amemteua Jakaya mrisho kikwete kuliongoza taifa letu hili lenye upendo, udugu, amani na mashirikiano. taifa ambalo lina demokrasia watanzania leo wapo huru kutoa maoni yao, kupinga, kukosoa serikali yao tofauti na huko nyuma watz ilikuwa ni dhambi kumsema Rais, au kumpinga, kukosoa. Nmshukuru mungu nimekuwepo katika tawala zote nne za nchi hii, mbali na utawala wa kwanza ambapo demokrasia ilikuwa hakuna kabisa,awamu ya pili mzee huyu atakumbukwa kwa kuasisi mfumo wa vyama vingi na alitoa ruhsa kwa kila mtu kufanya atakalo ilimradi usivunje sheria ya nchi. awamu ya tatu, huyu ameondoka na doa nadhani halitaweza kuondoka katika kumbukumbu ya kichwa chake, pale tu ulipomalizika uchaguzi wa mwaka 2000, alipiga marufuku ya mikutano ya kisiasa akitaka aachiwe atekeleze ilani ya chama chake, ndipo cuf walipoitisha maandamano ya kupinga uchaguzi wa znz na kauli ya Rais ya kuzuia shughuli za kisiasa, januarv 26 na 27/ 2001 na kuuliwa watu zaidi ya 75.awamu ya nne, lakini utawala huu umekuza demokrasia kwa kiasi kikubwa mno, watu wanasema Rais wetu ni legelege si legelege vunja sheria ndio utajua kuwa ni legelege au si legelege ndio maana viongozi wa dini walishushiwa ufunuo kuwa jakaya ni chaguo la mungu leo nimesadiki maneno yao kwa kuwa ni kiongozi mwenye hekima na busara japo kuna watu wanataka kuchafua sifa ya taifa letu hawataweza kwa taifa hili lipo mikononi mwa mungu. Tunamuombea dua mungu ampe afya na nguvu ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kila siku