Nchi inamshinda JK - Heche (Mkiti wa BAVICHA)

Nchi inamshinda JK - Heche (Mkiti wa BAVICHA)

ngurati

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
221
Reaction score
240
Wanajanvi,
Nimeona kwenye facebook wall ya Heche Mkiti wa BAVICHA Taifa ikiwa na maneno yafuatayo. Nawasilisha.

BAVICHA tunasikitishwa na hali ya nchi.Hakuna umeme wala mafuta,utawala wa Rais Kikwete umeshindwa kutatua matatizo ya watanzania.Kama waTZ waliamua kununua majenereta ili kukabiliana na tatizo la mgao wa umeme, sasa hamkuna hata mafuta ya kuendeshea hayo majenereta.

Alipohojiwa na BBC akiwa Afrika Kusini alisema tatizo la umeme ni mvua na mabwawa kukauka na yeye sio Mungu hawezi kuleta mvua.Je Tatizo la mafuta nalo ni mvua?

Watanzania kuna kila sababu ya kutafakari upya hatma ya nchi yetu.
 
Kwa moyo wa unyenyekevu namwomba Rais JK atoe hotuba na kutangaza hali ya hatari kwa wauza mafuta waliokaidi amri
halali ya serikali yake.

Mh,Rais hali ni mbaya mno wafanyabiashara ya mafuta bado
wameitunishia misuri serikali,raisi wangu usipofanya hivyo
usitulaumu wananchi kwamba hatukukupa taarifa.

Mh Rais wananchi wamefikishwa pabaya na ubutu wa serikali
yako,biashara sasa hazifanyiki,umeme ni wa mgao mafuta ya
kuendesha majenereta hakuna,nauli zimepanda,muda si mrefu
bidhaa na hasa vyakula vitaanza kupungua sokoni kama si
kukosekana kabisa.

Mh Rais watu wanakutazama wewe na kukupima usikivu wako
leo sijui siku ya ngapi upo kimya labda upo bize na ugeni lkn
kumbuka kuangalia watu wako.Usipotoa tamko hawa wauza mafuta wataigarimu serikali yako.TAFADHARI HUTUBIA TAIFA
WANANCHI WANATESEKA, WAPATE MAFUTA.

Asante.
 
Wanajanvi, <br />
Nimeona kwenye facebook wall ya Heche Mkiti wa BAVICHA Taifa ikiwa na maneno yafuatayo. Nawasilisha.<br />
<br />
BAVICHA tunasikitishwa na hali ya nchi.Hakuna umeme wala mafuta,utawala wa Rais Kikwete umeshindwa kutatua matatizo ya watanzania.Kama waTZ waliamua kununua majenereta ili kukabiliana na tatizo la mgao wa umeme, sasa hamkuna hata mafuta ya kuendeshea hayo majenereta. Alipohojiwa na BBC akiwa Afrika Kusini alisema tatizo la umeme ni mvua na mabwawa kukauka na yeye sio Mungu hawezi kuleta mvua.Je Tatizo la mafuta nalo ni mvua?<br />
Watanzania kuna kila sababu ya kutafakari upya hatma ya nchi yetu.
Ujumbe mzuri, ngoja niende nje ya mada kidogo. Huyu bwana anaishi kwa kaka yake pale mori hadi sasa hajaweza kupata nyumba ya kuishi. Vipi kiongozi mkubwa kama yeye aendelee kufugwa na kaka yake?
 
Ni kweli kabisa.Sidhani kama rais wetu anaguswa na mtatizo yanayotuzunguka wananchi wake.He is very happy with his tours.Bado tuna idadi ya watu wengi wanaotuangusha kwenye kupata raisi mwenye uwezo.

1.The connected.Hawa watafanya kiva wanaloweza hata kama ni kuua kuhakikisha bado wanakuwa ndani ya system na wanaendelea kufaidika.

2.Wasiolewa kwa sababu ya kunyimwa elimu au fursa za elimu inayokidhi kutambua haki za raia na wajibu wa serikali kwenye suala la huduma na maendeleo.Hili kundi ndilo nguzo ya huu utawala mbovu.Kundi la kwanza linajitahidi kutumia nafasi yake kulihadaa kundi hili ambalo ndo la wadanganyika haswa.

Nguvu na juhudi kubwa bado vinahitajika kulipunguza kundi la pili ili kuungana kwa pamoja na kulipindua kundi la kwanza.
 
Hakuna mkuu duniani na mbinguni ila ni mungu pekee ambaye amemteua Jakaya mrisho kikwete kuliongoza taifa letu hili lenye upendo, udugu, amani na mashirikiano. taifa ambalo lina demokrasia watanzania leo wapo huru kutoa maoni yao, kupinga, kukosoa serikali yao tofauti na huko nyuma watz ilikuwa ni dhambi kumsema Rais, au kumpinga, kukosoa.

Nimshukuru mungu nimekuwepo katika tawala zote nne za nchi hii, mbali na utawala wa kwanza ambapo demokrasia ilikuwa hakuna kabisa,awamu ya pili mzee huyu atakumbukwa kwa kuasisi mfumo wa vyama vingi na alitoa ruhsa kwa kila mtu kufanya atakalo ilimradi usivunje sheria ya nchi.

Awamu ya tatu, huyu ameondoka na doa nadhani halitaweza kuondoka katika kumbukumbu ya kichwa chake, pale tu ulipomalizika uchaguzi wa mwaka 2000, alipiga marufuku ya mikutano ya kisiasa akitaka aachiwe atekeleze ilani ya chama chake. Ndipo CUF walipoitisha maandamano ya kupinga uchaguzi wa znz na kauli ya Rais ya kuzuia shughuli za kisiasa, Januarv 26 na 27/ 2001 na kuuliwa watu zaidi ya 75.

Awamu ya nne, lakini utawala huu umekuza demokrasia kwa kiasi kikubwa mno, watu wanasema Rais wetu ni legelege si legelege vunja sheria ndio utajua kuwa ni legelege au si legelege ndio maana viongozi wa dini walishushiwa ufunuo kuwa Jakaya ni chaguo la mungu leo nimesadiki maneno yao kwa kuwa ni kiongozi mwenye hekima na busara japo kuna watu wanataka kuchafua sifa ya taifa letu hawataweza kwa taifa hili lipo mikononi mwa mungu.

Tunamuombea dua Mungu ampe afya na nguvu ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
 
Nchi ilimshinda tayari sasa imshinde mara ngapi na wewe Heche mi nshamchoka huyu jamaa kiukweli kila ck mtakuwa mna2ambia hivihv! Nchi imemshinda,asikii matatizo ya wananchi, sasa kama 2meshindwa cha kufanya sahizi 2subiri2 uchaguzi ujao Mungu ausaidie 2wape Adhabu kali! Na adhabu yenyewe ni kutowarudusha hawa jamaa kwenye Dola.
 
Kwa kifupi, nchi yetu haina rais!
Nakumbuka nilipokuwa mdogo, Dingi na maza walipokuwa safarini, hapo home kila m1 wetu alikuwa bosi. Hakuna wakutoa amri maana haitafuatwa! Ndio ninavyoiona TZ ya sasa!
Hatuna raisi!
 
Ujumbe mzuri, ngoja niende nje ya mada kidogo. Huyu bwana anaishi kwa kaka yake pale mori hadi sasa hajaweza kupata nyumba ya kuishi. Vipi kiongozi mkubwa kama yeye aendelee kufugwa na kaka yake?

Kiongozi mkubwa ndio nini? Nawe Kafugwe na Dada yako kwa sababu ni kiongozi mdogo kimawazo..................
 
Hivi wewe unayemtetea kikwete, mwenzetu waishi shimo gani.? Acheni unafiki kikwete nchi IMEMSHINDA, mwenye raha labda ni, jambazi, fisadi au muuza madawa ya kulevya!
 
Acheni kukurupuka. Nchi imemshinda wapi? We huoni anavyofuturisha watu kila siku?

Dogo Rizi alishawatahadharisha kwamba watu wanaishi kimjini mjini hapa... Nchi nzima imekuwa ujanja-ujanja tu kuanzia kwa Prez
 
Back
Top Bottom