Nchi inamhitaji sana Dr. Magufuli

Nchi inamhitaji sana Dr. Magufuli

Ndugu zanguni mnyonge mnyongeni lakini haki
yake mpeni,kwa hatua ya kuwa waziri wa kawaida amefanya mengi yasiyo yakutafuta,na hapo hajawahi gusa uwaziri mkuu kama huyo mwenzake ambaye alipaswa kuwa na rekodi kubwa zaidi,kwa hiyo kwa mtazamo wangu magufuli ni safi zaidi ya lowassa na anakazi za tunu alizofanya,huyo mwingine binafsi sioni jipya toka kwake kabisa,I am going to vote for magufuli
 
Naomba uniombe samahani kwa kashifa kuhusiana na kichwa cha habari katika uzi wako huu na maelezo yako kabla sijakuripoti kwa invisible.
 
Magufuli ni mtendaji mzuri ila hafai kuwa Rais ana maamuzi ya kukurupuka ambayo yanaweza yakaingiza nchi kwenye matatizo makubwa.

Magufuli ana takiwa awe chini ya mtu ambaye atakuwa ana muagiza kutenda,na atakaye kuwa ana mfunga break ili asiweze kufanya uharibifu.
 
Mengi wameyafanya ya kijinga lakini hili la kuongeza bei ya mafuta ya taa kuzuia wezi ? Aisee ondokeni kuweni wapinzani mtajua mahitaji muhimu kwa Watanzania ni yepi,mwakyembe kazuia madawa ya kulevya JNA na pembe za ndovu na wezi wa makontena bandarini mkaona hafai mkamtoa mkamuweka Sitta kwa ajili kuendeleza biashara haramu. Wananchi walikua na kilio cha muda mrefu na walijua ipo siku mabadiliko yatakuja hata mwaka haujapita upepo umebadili mwelekeo hii ccm Nje katika sanduku la kura labda kwa mengineyo..
 
CCM inamuitaji zaidi Dr. JP Magufuli ili wamalize tofauti zao ndani ya chama.
Watanzania wanahitaji mabadiliko nje ya CCM.... Na huu ndiyo wakati wa kuyasukuma hayo mabadiliko...

Kama mkoloni mzungu aliondoka miaka 54 ilopita na maisha yaliendelea.... Maisha yatawezekana vile vile bila CCM mkoloni mweusi...

NO MAGUFULI NO CCM!!!
 
Ndugu zanguni mnyonge mnyongeni lakini haki
yake mpeni,kwa hatua ya kuwa waziri wa kawaida amefanya mengi yasiyo yakutafuta,na hapo hajawahi gusa uwaziri mkuu kama huyo mwenzake ambaye alipaswa kuwa na rekodi kubwa zaidi,kwa hiyo kwa mtazamo wangu magufuli ni safi zaidi ya lowassa na anakazi za tunu alizofanya,huyo mwingine binafsi sioni jipya toka kwake kabisa,I am going to vote for magufuli

Hakuna mwenye tatizo na utendaji wa Magufuli ni Mtendaji mzuri wa kutenda kile ambacho ana agizwa na boss wake.

Ndiyo maana aliweza kufanikiwa vizuri kiutendaji katika wizara alizozipitia kwa kuwa viongozi wake walikuwa wanamsimia vizuri, akiwepo Lowassa mwenyewe ambaye alikuwa waziri mkuu wake.

Na kwa sasa mafanikio ya Magufuli ni kuungana na Lowassa UKAWA,ili aje ampe kazi ya kuhakikisha kila mwananchi ana miliki nyumba na siyo kufanya kazi ya kuhakikisha kila Mwalimu ana pata laptop.
 
mahwahwajr

Habari wakuu

Hii nimeipata mahali nikaona vema kushare hapa

Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.

Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu. Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k.

Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA. Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi.

Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongoza nchi mara moja. Mtu huyu ni Edward Lowassa.

Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa. Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara. Tuangalie mifano:

Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA!
Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.

Ndg.Makufuli amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA.
Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA.
Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa, hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA. Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA.

Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumziko ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA.

UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala. NITAMPIGIA LOWASSA.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi na nilishaandika tena baada ya kuzungumza na wazee waliojaa busara na wengine walishafanya kazi ofisi nyeti wao wanasema hii " tunawaadhibu ccm wachache October kwa kuwa wao wameshindwa kuwaadhibu wenzao wengi ambao ni mafisadi" hata magufuli wajaongea chochote kuhusu hawa mafisadi.
 
mahwahwajr

Hvi kile kivuko chakavu alichonunua kilikua na kuwahadaa watanzania kwamba ni kipya lini kitaanza kufanya kazi au ndio kishakua makazi ya ndege na na mzinga wa nyuki? Je tunamhitaji ili aje kutununulia meli ya bukoba chakavu au kule kigoma kwenye ziwa tanganyika?
 
Last edited by a moderator:
Huo upande mwingine nao ni vilevile...
Btw, mimi sioni tatizo yeyote kupewa uongozi kama anastahili. Suala ni je, akipewa uongozi anawatumikia watu?
Cha muhimu achague watu wapya kabisa ambao hawana mawaa! Wale wote ambao wanajifanya wana uzoefu mkubwa ndani ya chama na Serikalini wenye hulka ya kujipendekeza wasipewe nafasi ya Uwaziri au ushauri wowote katika Serikali ya Mh.Magufuli - narudia akitaka kufanikiwa akae mbali na kundi hilo hatarishi.
 
Huo upande mwingine nao ni vilevile...
Btw, mimi sioni tatizo yeyote kupewa uongozi kama anastahili. Suala ni je, akipewa uongozi anawatumikia watu?

Atawatumikiaje watanzania wakati ilani ya ccm haimruhusu zaidi ya kupiga madili ya wizi?
 
sawa, magufuli ni mchapa kazi ila tatizo lipo kwenye chama anacho fungamana nacho, hapo tuuuu. Hivi unamkumbuka profesa muhongo? Ubaya wake upo wapi zaidi ya kufungiwa nira na ccm?. Mkuu tafadhali acha kuitetea ccm, nina kila sababu za kuwakataa ccm kwani wamenihujumu mimi binafsi na pia wameihujumu jamii kwa ujumla ambayo mimi ni miongoni mwayo.
Siyo sahihi ccm ilikuwa inaharibiwa na Lowasa na kundi lake la mafisadi ila kwa kuwa fisadi ameondoka sasa ccm ni njema kabisa.
 
Magufuli hafai kuwa kiongozi wa nchi hii atuhitaji mtu atakaye mlinda jakaya na ilani chama cha mapinduzi kwani toka nchi hii imepata Uhuru kumeshakwepo na ilani ngapi ambayo imeshindwa kutatua Matatizo ya wananchi?
 
Back
Top Bottom