Nchi inamhitaji sana Dr. Magufuli

Nchi inamhitaji sana Dr. Magufuli

Magufuli hafai kuwa kiongozi wa nchi hii atuhitaji mtu atakaye mlinda jakaya na ilani chama cha mapinduzi kwani toka nchi hii imepata Uhuru kumeshakwepo na ilani ngapi ambayo imeshindwa kutatua Matatizo ya wananchi?
Hatutaki kuongozwa na fisadi siye tunamtaka magufuli huyo fisadi wenu pelekeni monduli akaongoze baraza wazee wa kimila.
 
Habari wakuu

Hii nimeipata mahali nikaona vema kushare hapa

Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari.

Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu. Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k.

Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA. Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi.

Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongoza nchi mara moja. Mtu huyu ni Edward Lowassa.

Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa. Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara. Tuangalie mifano:

Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA!
Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.

Ndg.Makufuli amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA.
Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA.
Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa, hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA. Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA.
Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumziko ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA.

UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala. NITAMPIGIA LOWASSA.

Eeh bwana eeh! Nachelea kusema kua Magufuli ni SPECIAL FAILURE!
 
Umenena mkuu. Hata mimi binafsi sijawahi kuona mtu wa aina ya Magufuli. Ndiyo mtu anatufaa kwa nyakati hizi. Wapinzani wanasema tatizo ni mfumo lakini mi naangalia mtu binafsi kuliko chama maana kiongozi ndo ata determine mfumo uwe vipi. Kama ungekuwa mfumo Magufuli naye angekuwa fisadi tofauti na wengine ambao wamehamia upinzani na kudai ufisadi wao ulikuwa unatokana na mfumo. Kama mtu mmoja kafanya kazi kwenye mfumo huo na hakuweza kuwa fisadi lakini mwingine kawa fisadi huwezi sema sababu ni mfumo bali.mtu mwenyewe.
 
mpaka sasa hatujasikia kauli za kijasiri toka kwa makufuli juu ya kushuhulikia mafisadi na rushwa. rushwa na ufisadi ndio matizo kubwa linaloisumbua Tanzania zaidi tumemsikia akimsifia Rais tu
tunataka tusikie kauli yake dhidi ya mafisadi katiba Mpya escrow

Ogopa kiongozi ambaye hajui watanzania wanataka nini na wanahitaji nini mpaka aelekezwe na chama. Hata kwenye hyo ilani ya chama hana alichochangia zaidi ya kutembelea kwenye mawazo ya wenzake.
 
Lowassa kafanya makubwa katika nchi hii wakazi wa shinyanga watamkumbuka kwa kuwaletea maji toka ziwa Victoria hadi shinyanga
 
Sawa Dr Pombe hana shida..Lakini akishinda itakua tu business as usual tu..Kina vijanaa January, Rizi na nani watapewa uwaziri, mafisadi watalindwa, umaskini utadumishwa..

Tatizo sio Magufuli shida iko ndani ya ccm yenyewe. Na Magufuri akiingia madarakani atafuata misingi ile ile ya watu wale wale waliotoka ndani ya ccm. Hata ukusikiliza hotuba zake anasema nitafuata ilani ya chama cha mapinduzi na kuyaenzi yote ya mhe Jakaya kikwete sasa hiyo ndio nini? Hatutaki hatutaki tena ccm.
 
Mimi nadhani wamejitahidi kuchukua hatua. Kumbuka akina Dr Nchimbi na wenzio wapo wapi. Hili lilikuwa ni sakata la Operesheni TOKOMEZA . Sakata la ESCROW nalo liliondoka na wengi. Huko nyuma akina Zombe, Mramba, na wengine walishughulikwa. Nadhani ipo haja ya kuangalia upya suala la kusema CCM wanalindana.

Enough is enough. sera za kulindana na ufisadi ndio umewakatisha tamaa wananchi wengi.
Mtu akiboronga ofisi hii anahamishwa ofisi nyingine tu.
No. hakuna cha Magufuli wala makomeo, tunahitaji CHANGE period.
 
Kifupi ni kwamba kuendelea kuitetea ccm ni kama kuhalalisha ujinga wao wa kuihujumu NCHI yetu.CCM wamefanya Nchi hii uongozi wake kuwa ni wa watu wenye pesa tu, masikini hata angekuwa na uwezo kiasi gani hawezi kuwa kiongozi siku hizi..Hivi kuna sababu yoyote ya msingi kuwauzia watanzania mafuta ya taa shs 2000? kuna sababu yoyote ya kuwauzi watanzania sukari shs 2000? kama unaipenda ccm na wewe una matatizo. mimi naiombea kifo chema

Mkuu umemaliza yote umeufanya moyo wangu uwe na Amani
 
sawa, magufuli ni mchapa kazi ila tatizo lipo kwenye chama anacho fungamana nacho, hapo tuuuu. Hivi unamkumbuka profesa muhongo? Ubaya wake upo wapi zaidi ya kufungiwa nira na ccm?. Mkuu tafadhali acha kuitetea ccm, nina kila sababu za kuwakataa ccm kwani wamenihujumu mimi binafsi na pia wameihujumu jamii kwa ujumla ambayo mimi ni miongoni mwayo.

Mkuu mimı sıkubalıanı nawe ila nakupongeza namna ulivyojibu hoja kwa hoja bila jazba wala matusi km walivyo wengi wa wafuasi wa Ukawa.Utakuwa nı msomi mzuri,ama mcha Mungu mzuri ama mtu mzima mwenye hekima na km kijana wewe n hazna ya taifa.Ufuasi sı uadui wala ugomvi.
 
Familia ya jk na watu wachache wanamuitaji Mapombe watanzania tuliobaki hatumtaki kabisa mtu huyu
 
Siyo sahihi ccm ilikuwa inaharibiwa na Lowasa na kundi lake la mafisadi ila kwa kuwa fisadi ameondoka sasa ccm ni njema kabisa.

Kumbe akina Chenge,Tibaijuka na mafisadi wenzao wote wameondoka CCM?.
 
Enough is enough. sera za kulindana na ufisadi ndio umewakatisha tamaa wananchi wengi.
Mtu akiboronga ofisi hii anahamishwa ofisi nyingine tu.
No. hakuna cha Magufuli wala makomeo, tunahitaji CHANGE period.

Wengi wanaounga mkono Lowasa ni wale watuhumiwa wa makosa tofauti ya jinaı.Ndio wanamchangia hela kuhakıkısha anaingia Ikulu.Unadhani ataweza kuwachukulia hatu ikiwa moja ya mambo anayo mlaumu Kikwete nı kukosa uaminifu wa kuwalinda marafiki zake walipopatwa na matatizo serikalini?
 
Hakuna mwenye tatizo na utendaji wa Magufuli ni Mtendaji mzuri wa kutenda kile ambacho ana agizwa na boss wake.

Ndiyo maana aliweza kufanikiwa vizuri kiutendaji katika wizara alizozipitia kwa kuwa viongozi wake walikuwa wanamsimia vizuri, akiwepo Lowassa mwenyewe ambaye alikuwa waziri mkuu wake.

Na kwa sasa mafanikio ya Magufuli ni kuungana na Lowassa UKAWA,ili aje ampe kazi ya kuhakikisha kila mwananchi ana miliki nyumba na siyo kufanya kazi ya kuhakikisha kila Mwalimu ana pata laptop.

Hahahahaaaa hapo tena waungane haaa sijui.
 
Ninakubaliana na wewe kuwa tunamhitaji Mh. Magufuli, lakini tunamhitaji kama waziri wala si kama Rais.

Tumshauri baada ya kumchinja na vichinjio vyetu Oct 25th basi ajiunge ukawa tumpe ubunge wa bure halafu tumpe wizara moja.
Nchi inahitaji CHADEMA kwa muda huu halafu Magufuli na wengine kama yeye ni kwa ziada tu
 
Cha muhimu achague watu wapya kabisa ambao hawana mawaa! Wale wote ambao wanajifanya wana uzoefu mkubwa ndani ya chama na Serikalini wenye hulka ya kujipendekeza wasipewe nafasi ya Uwaziri au ushauri wowote katika Serikali ya Mh.Magufuli - narudia akitaka kufanikiwa akae mbali na kundi hilo hatarishi.

Kwani hao atakao wachagua atawapeleka ofisi ipi. Nani amekuambia atapita? raisi ni Lowasa.
 
mpaka sasa hatujasikia kauli za kijasiri toka kwa makufuli juu ya kushuhulikia mafisadi na rushwa. rushwa na ufisadi ndio matizo kubwa linaloisumbua Tanzania zaidi tumemsikia akimsifia Rais tu
tunataka tusikie kauli yake dhidi ya mafisadi katiba Mpya escrow

Akiweka hayo wazi hatapewa nafasi.Anatakiwa awe mpole ıla akishapewa rungu ana wachenjıa.Ndivyo Mwanawasa alivyomchenjıa Chiluba na kote dunianı.Magulı ana kila dalilı ya kuwa hvyo ndo maana ulisıkia wengi wakıdaı hakijui Chama!!Lowasa kwa swala la kupambana na ufisadi sahau kabisa.Km waelewa vzuri ajenda yake ya kuchukia umasıkini nı kwamba pambana na umasikini hata km unaiba,unakula rushwa alimradi umefanikiwa.Na msingi wa hayo yote ni hatua ambazo Kikwete alichukua kuteleza maagzo ya Bunge kwa kutengua teuzi za baadhi ya mawazirı na hata akina Mramba et al kufkishwa mahakamanı.
 
Back
Top Bottom