Nchi inamhitaji sana Dr. Magufuli

Nchi inamhitaji sana Dr. Magufuli

Mimi nadhani wamejitahidi kuchukua hatua. Kumbuka akina Dr Nchimbi na wenzio wapo wapi. Hili lilikuwa ni sakata la Operesheni TOKOMEZA . Sakata la ESCROW nalo liliondoka na wengi. Huko nyuma akina Zombe, Mramba, na wengine walishughulikwa. Nadhani ipo haja ya kuangalia upya suala la kusema CCM wanalindana.

Kumbuka hili lilikomaliwa na bunge yaani bunge ndio wakomae mawaziri wawajibishwe? Rais haoni wana kosa?na mara nyingi zikitokea tuhuma zinazowahusu mawaziri anakuwa yuko nje ya nchi na akirudi wala hashughuliki nao. Haaa too much sasa.
 
Ccm must goooooo hata angekuwa magufuli, Rose migiro,makamba hatuna tena muda hata mwaka mmoja wa kujaribisha ccm, tuna vitambulisho tu vya kupumzisha
tena m
 
Sawa, Magufuli ni mchapa kazi ila tatizo lipo kwenye chama anacho fungamana nacho, hapo tuuuu. Hivi unamkumbuka profesa muhongo? Ubaya wake upo wapi zaidi ya kufungiwa nira na CCM?

Mkuu tafadhali acha kuitetea CCM, nina kila sababu za kuwakataa CCM kwani wamenihujumu mimi binafsi na pia wameihujumu jamii kwa ujumla ambayo mimi ni miongoni mwayo.

Muda wa kuwaadhibu ni sasa vinginevyo tuwaache watutawale milele. Chama ni kikubwa kuliko magufuli, hivyo bado kumchagua magufuli ni kuichagua CCM ileile na hakuna kitakachobadilika.
 
Ndugu wanabodi,

Mjadala mkubwa hivi sasa nchini kwetu ni juu ya nani atakuwa kiongozi mkuu na kwa sasa mazungumzo yanawalenga zaidi watu wawili kwa maana ya Dr John Pombe Magufuli wa CCM na Mh Lowassa kwa upande wa UKAWA. Kwa bahati mbaya sana na kwa kusaidiwa na vyombo vya habari ambavyo kwa maoni yangu naona haviitendei haki nchi yetu, sasa hatujadili nini nchi yetu inahitaji na/au ni kiongozi mwenye qualities zipi tunahitaji ili kutoka hapa tulipo na kwenda mbele zaidi.

Mjadala sasa umekuwa juu ya mahudhurio ya watu kwenye mikutano na sio issues. SAD!!

Nimepata bahati ya kutafiti kazi za mgombea wa CCM Dr Magufuli hasa akiwa Wizara ya Ujenzi. Kwa maoni yangu huyu bwana ni MCHAPA KAZI hodari sana, sana. Sikumbuki kama tumewahi kupata kuwa na waziri mwenye uwezo mkubwa wa kiutendaji kama wa mheshimiwa Magufuli katika miaka ya hivi karibuni.

Tukiondoa ushabiki na madai ya mabadiliko ilhali nchi yetu inahitaji transformation, namuona Dr Magufuli akitufaa na kutuvusha kwenda hatua ya juu zaidi. Video hii hapa nchi ni ushuhuda wa namna bwana huyu alivyo mtendaji hodari.




Transformation inayotakiwa ni pamoja na kuwaonesha CCM kwamba huwa kuna kushindwa kwenye uchaguzi, siyo watu wanalewa madaraka mpaka wanadiriki kusema hata kwa goli la mkono watashinda.

CCM inatakiwa kushindwa mwaka huu halafu iparaganyike na kuvunjika vipandevipande ili platform ya siasa ijengeke upya. Tumechoka na urithishanaji wa uongozi, baba akiwa Mbunge, mtoto naye lazima awe mbunge
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa, lakini tatizo kubwa na la kipekee ni kwamba Magufuli bahati nbaya sana anagombea uraisi kupitia chama cha CCM ambacho wananchi kwa sasa wamekichoka mno na lazima wakitoe madarakani 25.10.15 maana magufuli akishinda kupitia CCM ataturudisha hukohuko tuliko umizwa kwa miak 54
 
Kaka, i can feel your pain, lakini nchi yetu inwahitaji viongozi wa aina hii. Mimi wala siitetei CCM. Hili timbwili linaloendelea sasa hivi lazima limeinyoosha CCM kama kweli unadhani imewatenda vibaya wananchi wake. Nchi yetu inamhitaji sana Dr Magufuli
i don't trust ccm, with alot of refferences.
 
Kaka, i can feel your pain, lakini nchi yetu inwahitaji viongozi wa aina hii. Mimi wala siitetei CCM. Hili timbwili linaloendelea sasa hivi lazima limeinyoosha CCM kama kweli unadhani imewatenda vibaya wananchi wake. Nchi yetu inamhitaji sana Dr Magufuli

Hakuna timbwili la kuwznyoosha ccm linaloendlea zaid wakae pemben kdg ata kwa miaka mitano nafikr hyo nd itawanyoosha,hatuwez kumpa mtu mmoja alaf waumie weng bora tuwape wengi aumie mmoja
 
Kwanza pole sana ndugu.
Pili naomba kuchangia ktk mawazo yako kuwa unachokisema ni sahihi kwa asilimia kadha na kwa asilimia zingine si kweli kwamba eti tatizo ni chama kama chama. Chama kama chama naamini ukisoma makablasha yao naamini utakuta wameandika maandishi mazuri sana kama hivyo vyama vyetu vingine. Tatizo ninaloliona mie ni sisi watu wenyewe na wala sio mfumo tu. Ebu jipime nafsi yako mwenyewe ujiangalie. Suala la mtu kuitumia ofisi ya umma kama mradi wake au suala la mtu kuomba rushwa hili sio tatizo la mfumo bali ni tatizo la nafsi zetu kwa level ya mtu mmoja mmoja. Ivi Lowasa alivyopiga isue ya Richmond unataka kuniambia aliipiga na watumishi wote wa umma?
Je unata kuniambia wewe ukiombwa rushwa ni tatizo la mfumo au ni tatizo la huyo anayekuomba?

Naomba nimalizie kwa kusema kuwa tatizo sio chama cha mapinduzi bali tatizo ni sisi wenyewe.
Mfano: ivi kuna mtu hajui mchango wa Dr Slaa kwa cdm? Mbowe kamfanyia nini? Pale wa kulaumiwa ni cdm yote au ni mbowe?[/QUOTE
mkuu, mfumo huundwa na mtu mmoja mmoja, mmoja anapo haribu na wengi wakashindwa kumkemea, kwanini tusiseme ni tatizo la mfumo?
 
Huo upande mwingine nao ni vilevile...
Btw, mimi sioni tatizo yeyote kupewa uongozi kama anastahili. Suala ni je, akipewa uongozi anawatumikia watu?

Kama kiongoz anatoka ndan ya ccm,sahau ishu ya kuwatumikia wananchi,kma kwel walikuwa na nia ya kutmikia wananchi ile miswaada ya ges na mafuta wasingeipeleka vle kama walivyofanya
 
Siyo sahihi ccm ilikuwa inaharibiwa na Lowasa na kundi lake la mafisadi ila kwa kuwa fisadi ameondoka sasa ccm ni njema kabisa.
ndugu, uchafu na tuhuma za lowasa zinatofautiana vipi na za hawa? chenge, kikwete, tibaijuka, kinana,.............
 
Kwanza pole sana ndugu.
Pili naomba kuchangia ktk mawazo yako kuwa unachokisema ni sahihi kwa asilimia kadha na kwa asilimia zingine si kweli kwamba eti tatizo ni chama kama chama. Chama kama chama naamini ukisoma makablasha yao naamini utakuta wameandika maandishi mazuri sana kama hivyo vyama vyetu vingine. Tatizo ninaloliona mie ni sisi watu wenyewe na wala sio mfumo tu. Ebu jipime nafsi yako mwenyewe ujiangalie. Suala la mtu kuitumia ofisi ya umma kama mradi wake au suala la mtu kuomba rushwa hili sio tatizo la mfumo bali ni tatizo la nafsi zetu kwa level ya mtu mmoja mmoja. Ivi Lowasa alivyopiga isue ya Richmond unataka kuniambia aliipiga na watumishi wote wa umma?
Je unata kuniambia wewe ukiombwa rushwa ni tatizo la mfumo au ni tatizo la huyo anayekuomba?

Naomba nimalizie kwa kusema kuwa tatizo sio chama cha mapinduzi bali tatizo ni sisi wenyewe.
Mfano: ivi kuna mtu hajui mchango wa Dr Slaa kwa cdm? Mbowe kamfanyia nini? Pale wa kulaumiwa ni cdm yote au ni mbowe?

Na mm naomba nichangie ktk mawazo yako,kwanza unapotosha umma kuhusu suala la richmond,umeshikilia maelezo ya wakat huo pasipo kuangalia hali halis,mkuu kasema hakuna kitu kinachofanyika bila ya yeye kutoa maelezo so ilo suala linamgusa yy mja kwa mja,pia el kasema yy hausik bdo ww umekarir tu,unakuja na mada ya kutoulaum mfumo bali ni sis ukitolea mfano wa kutoa rushws,jiulze kama kungekuwa na maslah mazur kwa watendaj na utekelezaj wa sheria ayo mambo yasingekuwepo!mfumo ndo tatz
 
Nchi haimuhitaji Magufuli ambae yupo chooni choo kinanika na hawezi kukisafisha choo hata kidogo
 
Ni kwel mkuu,ni mchapakazi,muadilifu,mfuatiliaji,n.k lakini kura yangu kwa Lowasa basii
 
Ni ukwel usiona shaka kuwa Dr. Magufuli anafaa sana kuwa Rais.
Yule ambaye baadhi ya watu wanamshabikia hafai kwa kuwa amezungukwa na wanamtandao ambao ni wachafu kimaadili. Hata yeye pia sio muadilifu pamoja na kuwa watu wengi wanamshabikia.
Tunatakiwa kujenga nchi chini ya mtu ambaye anafuata na kusimamia sheria na kanuni za nchi.
Katika hili Tanzania inamuhitaji sana mtu kama Dr. Magufuli ili aongoze nchi iweze kusimama kwenye maadili ya uongozi
 
Watu wengi wanashabikia Ukawa kama wanavyoshabikia timu za mpira
Uongozi wa nchi ni tofauti na hayo
Hata wenzetu wa nchi za ulayana marekani huangalia mtu na wala sio chama.
Vijana muamuke na kujitambua
 
Back
Top Bottom