Nchi inaendeshwa na 'KITENGO'?


Pats like yangu mkuu well said
 
Fikiria mtu na akili zake timamu anatetea hilo zimwi kitengo eti kina haki ya kuwachagulia wananchi viongozi kwa sababu wananchi wanaweza kumchagua mtu hatari. Swali ni hatari kwa nani?

Kuna dai kwamba chama tawala CCM kimetekwa na wenye nguvu lakini hatujiulizi hao wenye nguvu ndio akina nani? Zipo nyakati nyingi tu viongozi wetu wa kitaifa tuliowachagua tumesikia wakilalamika, hatujiulizi wanamlalamikia nani.

Kama Raisi analalamika, Waziri Mkuu analalamika, Katibu Mkuu wa chama tawala analalamikia utendaji wa serikali iliyoundwa na chama chake...wananchi tueleweje? Katiba yetu imempa nguvu ya kimungu Raisi wetu, kwa nini alalamike?

Oh mara wasaidizi wangu wananiangusha, anawabadilisha, Haijakaa muda na hao wapya anaanza kuwalalamikia eti wanamuangusha, anawabadilisha. Muda si muda mambo bado hayaendi anaanza tena kulalamika, kulikoni wananchi wenzangu?

Tunamchagua Raisi kwa imani kubwa kwamba sasa tumempata kiongozi mzuri lakini haichukui muda mambo yanarudi kule kule. Mifano ipo tangia Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete...ni nani huyo anawachezesha mchakamchaka, je ni kitengo?

Hayati Mwalimu alimpigia debe Mkapa, akatembea nchi nzima akimnadi kama mtu safi lakini haikuchukua muda, tukajikuta tunatoka kapa. Mwalimu akaahidi kumpinga uchaguzi utakaofuata...je ni kitengo kilichoamua asiuone huo uchaguzi?

Cha ajabu licha ya kuwa na kitengo tumewashuhudia wezi na matapeli makubwa ya dunia yakipata hifadhi nchini na kuzidi kuneemeka kupitia rasilimali zetu.

Licha ya kuwa na kitengo tumeshuhudia matapeli wa kimataifa wakiivamia nchi yetu na kuingia mikataba mibovu ya kupora mali asili zetu kuanzia wanyama, madini hadi mimea.

Imefikia mahali ni kama nchi haina serikali, nchi haina katiba, nchi haina utawala wa sheria na vyombo vya dola viko tu kulinda maslahi ya wageni na maslahi ya wahamiaji haramu.

Ni kama vile vyombo vya usalama vipo tu kupambana na wananchi na si kuwalinda wao na mali zao. Vyombo vya kutoa haki navyo vinalalamika havina nguvu ya kupambana na wahalifu.

Ni kama vile nchi imetekwa na nchi haiko tena mikononi mwa wananchi na matakwa ya wananchi hayapewi tena uzito wala kipaumbele na serikali ni kama haiwatumikii tena wananchi.

Ni kama vile serikali haikuwekwa madarakani na wananchi bali imewekwa na hao inaowatumikia...kitengo? Kama Mtanzania hawezi kumchagua kiongozi anayemtaka kwa sababu kitengo hakikubali, je kweli tuko huru?

Kama Mzee Ngombale Mwiru, kada maarufu wa CCM aliyeitetea CCM wakati wa kiangazi na mvua, usiku na mchana leo yamemkuta na analalama kuhusu kitengo, lazima tujiulize maswali kadhaa!

Viko vifo vingi tu vya kutisha vimetokea nchini visivyo na maelezo, je ni kitengo kinanyamazisha wakosoaji?
Tumeshuhudia kila kunapotokea mtafaruku, kiongozi mkuu wa nchi anakuwa hayupo nchini, je nani huyo anaachiwa utekelezaji?


Hapana Watanzania, hii ni karne ya 21 na teknolojia inatupa fursa ya kutoka gizani. Mambo ya gizani tusiyape nafasi hivyo tujiulize. Kwa nini tuchague kiongozi tukiamini ni msafi halafu baada ya kitambo kidogo tu anaanza kucheza ngoma ya wengine?
 


Mkuu na wengine wengi
nimejaribu sana kueleza hapa main issue sio Lowassa lakini naona hamuelewi kabisa

Hebu tu assume 'kitengo' walimkata Lowassa na tu assume kuwa ni uamuzi sahihi..

swali bado linabaki pale pale....Kitengo walitumia vigezo gani kumchagua Magufuli
na kuwakata Pinda,Bilali,Mahiga,Mwele,Mwandosya,Sitta,Mwigulu,Kigwangala,na wengi wengine wote?

Hivi unafikiri wanachama wangechagua kwa uswa kati ya majina yote hayo Magufuli angepita?
na Usiseme Kitengo hakihusiki sababu nimetaja gazeti la RaiaMwema limeripoti Kitengo kumfanyia kampeni
Magufuli...na hata kura alizopata Asha kutoka Nec kura 280 kufika mkutano mkuu zimepunguzwa hadi 50...

Hilo ndo swali.....Kitengo kawapa nanimamlaka ya kuwachagulia watu Rais?
 

Huduma ya kitengo nje ya ccm ni kuzuia mikutano, kupandikiza na kuwalipa mamluki ndani ya vyama kuvuruga ustawi wa vyama (ZZK) kushauri kitengo jinsi ya kuiba kura, kununua wapinzani n.k.
 


CCM ni chama dola ukisikia wanasema sisi wajamaa, ujue ndiyo ktk mambo kama haya huu ndiyo mfumo wa Kikomunist nasikitika hata Mzee Kingunge kasahau.

CCM walishikwa woga sana ktk Katiba mpya pale walikua wameshikwa bara bara, lakini bahati haikua yetu tulitaka kupata kila kitu na Wahenga walisema mtaka yote kwa pupa..............

Lazima tujiulize kwa nini kuna Kamati ndogo ya maadili na Kamati ya Usalama na Maadili ambayo Mwenyekiti wake ni Mwenyekiti wa Chama ambaye ni Rais wa nchi, lakini pia hatujawahi kujenga hoja ya kupinga vikao vya CC kukutana Magogoni!

Kwa mtazamo wangu kama CCM watashinda uchaguzi wakapata Wabunge wengi, tuwashinikize Katiba pendekezwa ipigiwe Kura ya ndiyo hivyo hivyo ilivyo kwa sababu hakuna njia nyingine.

Najua tutakua tumerudi nyuma miaka 5 lakini ndiyo gharama hakuna njia ya mkato, kwani uwezekano ni mdogo upinzani kushinda kwa Katiba hii ya 1977

Swala la waandishi pia ni tatizo hawana uthubutu wakumtaka Waziri au Mkuu wa Nchi ili kufanya nae mahojiano, mpaka anajipangia mwenyewe kuongea mwisho wa mwezi akitaka.

Tujitahidi tukishindwa tusikate tamaa lakini kasoro kubwa kwetu ni MATUSI, KEJELI, UDINI, UKANDA na UJUAJI ukiangalia wengi wa wachangiaji uelewa wao ni mdogo kila mtu aheshimiwe au akikosea aelimishwe tutasonga mbele vinginevyo naiona miaka mingi ya CCM kuendelea kutawala.
Ole wetu kama tutamucha Comred Kinana aanze kufanya kile alichoahidi Mwanza.
 
Duh!

Kutoka 2015!

Zaidi ya miaka 5 ilopita.
 
Apatikane mtu ayachapishe vizuri maoni haya na kuya-laminate vizuri halafu yakagawiwe (hata kama ni kwa lazima) kwa viongozi wote wa upinzani. Na walazimishwe kuyasoma na kuyaelewa vizuri.

Bila kuwa na katiba mpya (mf. ile ya Warioba), tume huru ya uchaguzi na taasisi zingine huru kama mahakama, haki ya nani urais wataishia kuwa wanausikia kwenye TV tu na kila mwaka yatakuwa yale yale...."wanashindwa", wanalalamika kuwa wameibiwa kura, wanatukana na hata kupuyanga kwenda kushtaki huko kwa akina Amsterdam lakini hakuna kitakachobadilika.

Kuanzia sasa nguvu zote zielekezwe kwenye kupata katiba mpya...na mengine yote yatafuatia. Kama siyo hofu ya kupoteza hela za ruzuku, kusema kweli hata haja ya kushiriki chaguzi hizi hakuna...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…